WATUMISHI MKOA WA MARA MSIWE NA VITAMBI

 



Adeladius Makwega-Musoma MARA.

“Binafsi ninapenda watumishi wangu wote wa Mkoa wa Mara wa siwe na vitambi, wawe wanafanya mazoezi, mazoezi ni muhimu kwa afya zetu, hata mimi hapa naona kama kitambi kinaninyemelea, nataka nimgawie mtu hiki kitambi…”

Haya ni maelezo ya Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Alfred Mtambi Agosti 29, 2025 mbele ya Viongozi wa Timu Michezo ya Mkoa wa Mara iliyoingia ofisini kwake kuaga kuelekea Mkoani Mwanza katika mashindano ya SHIMIWI ambayo ni Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali ambayo yatadumu mkoani Mwanza kwa siku karibu dazeni na unusu.

“Mwende huko Mwanza nataka mkirudi tuwe na tunafanya mashindano ya RAS MARA na Wilaya zetu , leo Serengeti, kesho Bunda, siku Nyingine Tarime, Butiama , Musoma na Rorya,  mimi ninacheza sana Volleball.”

Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mara Timotheo Gamba ambaye ni Mwenyekiti wa kikosi hiki amemwambia Mkuu wa Mkoa wa Mara kuwa kwa hakika wanakwenda kushindana huko Mwanza na wana hakika kurudi na vikombe kadhaa hilo ni wajibu wao.

“Tumejianda vizuri na wechezaji wetu wako katika hali nzuri, tunarajia kuondoka muda si mrefu kuelekea Mkoani Mwanza, Mhe Mkuu wa Mkoa kwaheri.”

Akiwaaga wanamichezo hao wanaokaribia 50, Kanali Mtambi aliwatakia safari njema, huku akiwakumbusha kuwa michezo ina faida tele za kiafya. Akizungumza mara baada ya kikao hiki Katibu wa Wanamichezo hao ndugu Hashim Ujonjo amesema kuwa ratiba ya safari yao imekaa vizuri, wanatarajia kupita kwa Chifu Josephart Wanzagi ili kumuaga na kupata baraka zake kisha kuelekea Mwanza.

“Tumejipanga vizuri, kila kitu kipo tayari na mara zote tunapokwenda kushiriki huwa tunatoka hapa na vyakula vyetu ili tuweze kubaki na afya njema tukiwa mashindanoni. Kamati ya ufundi imeweka mambo yote sawa.”

Kwa hakika Mkoa wa Mara ni miongoni mwa mikoa inayofanya vizuri katika mashindano ya SHIMIWI kila mwaka, hata wakati viongozi wa SHIMIWI wanazungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mara, meza yake ilikuwa imepambwa na vikombe kadhaa walivyoshinda miaka ya nyuma.

makwadeladius @gmail.com

0717649257




 














 

 

0/Post a Comment/Comments