MONIKA BINTI MNYENYEKEVU

 


 Adeladius Makwega-Musoma TANZANIA

Siku hii ilianza kwa anga la Mji huu kuwa na giza, wingu si wingu na mvua si mvua, huku Mwanakwetu Kigulu na Njia hadi Kanisa la Mtakatifu Agusitino , Parokia ya Mwisenge Jimbo Katoliki la Musoma. Kwa desturi ya hii Parokia, mara zote Misa zake huwa zinajaa waamini na ukiingia Kanisani mara baada ya Padri ameshaingia ni adimu kupata kiti cha kukaa, jambo hili likitoa tasfri yake kuwa Wakristo wa Jimbo la Musoma wanawahi Kanisani. Parokia hii wana misa mbili kila dominika misa ya kwanza 12.30 ya asubuhi hadi 2. 30 na ya misa ya pili saa 3.00 hadi saa 5.00 ya asubuhi.


 

Siku hii ni Agosti 31, 2025 ikiwa ni dominika ya 22 ya Mwaka C wa Kanisa, mandhari ni ile ile waamini wamejaa vitini, Padri moja Mtu Mzima jina lake halikufahamika akiwa mbele ya Altare anaiongoza misa hii, yalisomwa masomo yote matatu na badaye Padri huyu kutoa mahubiri yake ambayo aliyafungua kwa kisa hiki.

“Palikuwa na Vijana wa Watatu Amina, Juma na Monika walisoma pamoja tangu shule ya awali, Shule ya Msingi, Sekondari na baadaye Chuo Kikuu, vijana hawa wote mwenyezi Mungu aliwabariki sana kwa kuweza kusoma hadi kufikia ngazi ya Chuo Kikuu, huku familia zao zikiwa katika maisha yetu ya kimasikini, wazazi wakiuza hiki na kile. Kwa hakika Wakristo Wenzangu mara baada ya mtoto kusoma, tufahamu kuwa, mwanafunzi mwenyewe, wazazi, ndugu na jamii husika inahitaji kijana husika apate kazi ili kwanza aweze kuyaendesha maisha yake, pili aweze kusaidia jamii yake katika mambo mbalimbali ili kulijenga taifa lake. Kijana akisoma alafu hana kazi huo unakuwa mzigo kwa wazazi, mzigo kwa jamii na mzigo kwa taifa husika na kunakuwa hakuna maana kijana huyu kusoma.

Mungu mara zote ni mwema sana, akafungua milango wa Juma, Amina na Monika kusikia tanganzo la kazi kwa masomo waliyosomea. Hapa ni Mungu Bahati, hakuna kulaza damu kila mmoja alichukua karatasi na peni akaandika barua na kuambatanisha vyeti vyake, kila mmoja kutuma maombi yake na kufika taasisi iliyotangaza kazi hii. Taasisi ikafanya mchujo kwa waliomba nafasi hiyo na kisha majina matatu kukubaliwa yaitwe kwa mahojiano. Karani wa taasisi hii akapiga simu kwa wahusika wote watatu Juma, Amina na Monika na kuwajulisha muda wa mahojiano .

Siku ya mahojiano ilifika Amina aliwasili katika ofisi hii pakiwa kimya akingoja muda wa mahojiano, muda ukawa unakaribia kama kasoro dakika 45 hivi, akiwa kitini  anakagua vyeti vyake akaja mama mmoja mtu mzima akawa anafagia huku akimsogelea pale alipo jirani yake, mama huyu aksema naomba unisaidie kufagia? Amina kasema mama hapa nimebakiza dakika chache niingie katika mahojiano, siweza kuifanya kazi hiyo, itanichelewesha na kwanza siyo jukumu langu na mimi nimekuja kwa mahojiano ya Msaidizi wa Meneja.

Baadaye alikuja Juma alipopokelewa pahala gafla alikutana na mama yule mfagizi akafika akasema maneno yale yale Mwanagu nisaidie kufanya usafi  Majibu ya Bwana Juma yalikuwa sawa sawa na ya Amina. Mama yule mfagizi akaenda zake na baadaye kuwasili Monika mama mfagizi akifagia pahala alipo Monika na kumuomba amsaidia kufagia.  Dada Monika akaangalia muda kasema muda bado ngoja nikusaidie, Monika akafagia akamaliza na kisha mama huyu mfagiaji kuchukua vifaa vyake na kuondoka zake.

Muda wa mahojiano ulifika wakaitwa wote Amina, Juma na Monika wakaambiwa usaili umeshafanyika na aliyepata kazi ni Monika Binti Mnyeyekevu na yeye ni ndiye Msaidizi wa Meneja wa Kampuni hii tangu sasa, nyinyi weneine mmekosa kazi hii. Hapo akaitwa akaitwa Meneja wa Kampuni hii kuwasalimu Juma, Amina na Monika na hapo kila mmoja mchozi ulimtoka kumbe Meneja alikuwa ni yule Mama Mfagizi .Jambo hili liliwaumiza mno Juma na Amina na kazi hiyo wakawa wameikosa. Swali kwako ni hili, kama Meneja Anafagia! Sembuse msaidizi wa Meneja? Wajibu lazima ufagie.”

Msomaji wangu Kisa hiki kinatoa funzo gani kwa Wakristo wote Jumapili hii?


 

 Majibu ya haya anayo Kadinali Luis Antonie Tagle Mkuu wa Propaganda Fide ya Kanisa Katoliki Ulimwenguni inayojihusisha na Uinjilishaji wa watu.

“Katika injili ya leo, Yesu anaonekana akila chakula nyumbani kwa Mfarisayo ambapo anatoa somo juu ya Ufalme wa Mungu katika muktadha wa karamu arusini. Bwana Yesu anawashauri wasikilizaji wake, ‘Msikae mezani katika nafasi ya heshima. Nendeni mkachukue nafasi ya chini kabisa.’ Hii ni kuepuka mkanganyiko na aibu inayoweza kutokea.

Kwa maneno mengine, ndugu zangu, Yesu anatufundisha kwamba katika Ufalme wa Mungu, kila mmoja wetu ana jukumu maalumu na nafasi iliyowekwa tayari kwake. Tunaukaribia kwa unyenyekevu na bila majivuno, tukisubiri Bwana atuweke kwenye kiti ambacho ameandaa kwa ajili yetu.‘Wa-alikeni maskini, vilema, viwete na vipofu, nanyi mtabarikiwa kwa sababu ya kushindwa kwao kuwalipa. Mtalipwa katika ufufuo wa wenye haki, pale Bwana atakapoandaa karamu yake ya mwisho.’ Na hapa hapa Yesu anasema Hayo.”

Mwanakwetu Upo?


 

 Kumbuka

“Monika Binti Mnyenyekevu.”

Nakutakia Jumapili Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257








 

0/Post a Comment/Comments