Adeladius Makwega-Serengeti MARA
“Mwalimu Gerald Msabila Kusaya ndiye kiongozi anayesimamia watumishi wote wa umma na sekta binafsi hapa mkoani Mara, natambua wewe ni mchapakazi , wewe ni kiongozi wetu, Katibu Tawala Mkoa wa Mara Oyeee, Katibu Tawala Baba Lao!(Baba Lao) Wanamuweza Kweli?(Hawamuwezi), Wanamuweza Kweli (Ahaa Wapi) Hata Wakishindana naye! (Hawamuwezi) Mara Oyee(Oyee) Asante sana.”
Haya ni maelezo ya Ndugu Ismail Ali Ussi, Kiongozi wa Wakimbiza Mwenge wa Uhuru, mwaka wa 2025, akiwa Wilayani Serengeti, Mkoani Mara akifunga Kongamano la Vijana kutoka Wilaya nzima ya Serengeti, mbele ya Mkuu wa Wilaya hii Bi Anjelina Lubella huku akimpamba Katibu Tawala Mkoa wa Mara katika Viwanja Vya Right to Play Serengeti Mjini jioni ya Agosti 22, 2025.
Akiendelea kumtaja Katibu Tawala Mkoa Mara katika Hotuba yake , Ndugu Ussi aliongeza ;
“Uwepo wako hapa katika kufunga Kongomano la Vijana Wilayani Serengeti jioni ya leo limenipa faraja kubwa. Wewe ndiye unayefanikisha yote haya ukishirikiana kwa karibu na Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Alfred Mtambi tangu ngazi ya Mkoa hadi ngazi hii ya wilaya.”
Akizungumza katika hotuba yake ya kufunga shughuli hii mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Bi Lubella, Ndugu Ussi alisisitiza Vijana wa Kitanzania waishi maisha yao kwa kuzingatia maadili ya Kitanzania na kuepukana na rushwa, matumizi ya madawa kulevya na tabia zingine mbaya.
“Kama mtajikinga na haya yote nina hakika mtakuwa vijana wazuri na vijana muhimu katika ujenzi wa taifa la Tanzania ambapo taifa hili linawategemea sana vijana wake.”
Awali Mwenge wa Uhuru Uliwasili katika Mji wa Serengeti ambapo ilisomwa Risala la Utii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kisha zoezi la kufunga Kongamano la Vijana ndipo likafanyika.





Post a Comment