ICT4RD YAKUMBUKWA NA TEHAMA MKOA WA MARA


Adeladius Makwega-Bunda-MARA

Kitengo cha Tekinolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Cha Mkoa wa Mara Agosti 28, 2025 kimefanya ziara ya kukagua iliyokuwa Miradi ya ICT4 RD kwa Wilaya ya Bunda ambapo ni miongoni mwa miradi iliyofanya vizuri kwa ICT miaka 10 iliyopita  kwa mkoa wa huu, shabaha ni kuangalia namna ya kuihusisha tena.

“Mradi huu uliweza kumsaidia mwalimu mmoja kufundisha shule kadhaa, huku wanafunzi wakimfuatilia mwalimu huyu kupitia tekinolojia hii, Shule ya Sekondari Guta, Shule ya Sekondari Chitengule na shule zingine kadhaa zilinufahika lakini sasa vifaa vyake vimechakaa.

Nina matumaini makubwa na shabaha yangu kuwa mradi huu kama utahuishwa unaweza kusaidia kupunguza shida ya uhaba wa walimu na gharama kubwa ya kuwatawanya walimu katika shule kadhaa hususani walimu wa masomo ya sayansi.”

Wakikagua mradi huo, mwandishi wa makala haya aliambatana nao alishuhudia minara kadhaa ambayo ilisimikwa mwaka 2013, bado ipi imara kabisa huku minara hiyo ikitumia vziuri kwa mawasiliano mengine ya sasa ikiwamo Redio za Kijamii na mitandao mingine. Akizungumza katika ziara hiyo Mkuu wa Kitengo hiki Mkoa wa Mara Ngobai Mwisarya alisema;

“Teknolojia ya Habari na Mawasiliano inachangia kwa kiwango kikubwa katika maendeleo ya maeneo ya vijijini, kwa kutoa upatikanaji wa taarifa muhimu kuhusu kilimo, uvuvi, afya, na elimu, kuwaunganisha wazalishaji wa vijijini na masoko, na kukuza ujasiriamali. Inaboresha miundombinu, inaongeza tija ya kilimo kupitia mbinu zinazotokana na takwimu, inaimarisha huduma za kijamii, na kuwezesha usimamizi bora wa rasilimali asilia.”

Akiitazama hali hii Ndugu Mwisarya alisema kwa sasa changamoto za mapungufu ya miundombinu na matatizo ya mtandao bado zipo, TEHAMA ina uwezo mkubwa wa kuboresha maisha, kuchochea ukuaji wa kiuchumi, na kujenga jamii za vijijini zenye ustahimilivu na endelevu kimataifa , huku halmashauri zinaweza kutumia TEHAMA kama chanzo kikubwa cha mapato na kwa sasa hakuna linaloweza kufanyika utakwepa TEHAMA.

 

Historia inadokeza kuwa mradi huu ulianzishwa mwaka 2013 chini ya ufadhili wa UNDP, Chuo Kikuu cha KTH nchini Sweeden na Shirika la Fraunhofer kutoka nchini Ujerumani. Ziara hii ilijumuisha maafisa kadhaa kutoka Kitendo cha TEHAMA Mkoa wa Mara na pia maafisa kutoka halmashauri husika.

Wakati ziara hii inafanyika wananchi wa Wilaya ya Bunda walikuwa wakiendelea na kazi zao kama kawaida ikiwamo kilimo, uvuvi, ufugaji na wanafunzi wakifanya mitihani ya kufunga shule mwezi wa Septemba.

makwadeladius@gmail.com

0717649257














































 

0/Post a Comment/Comments