Adeladius Makwega-MBAGALA.
Ilikuwa ni majira ya asubuhi ya siku hii, huku wafanyakazi wakiwahi kazini kwao, maana wanatakiwa kila mmoja moja unusu juu ya alama awe amekaa katika viti vyao, kuanza kutoa huduma kwa wateja. Geti la taasisi hii lilikuwa kuukuuu likifunguka kwa tabu, pengine kwa kukosa girisi. Msimuliaji akitazama akisema ingekuwa nyumba yake angeweka mafuta ya nazi, maana nayo ni kilainishi.
Mdau huyu aliingia getini, muda huo huo sawa na wenzake, kwa bahati nzuri getini hapo kulikuwa na watu kadhaa ambao walikuwa wakisafiri safari ndefu hivyo walikuwa wamejikusanya. Huyu mdau alipoingia tu akawasalimu kundi la wale jamaa ambao waliketi wakingoja kusafiri wakajibu salaam. Kisha huyu ndugu akaondoka zake lakini akabaini kuwa katika kundi la wale ndugu mmoja miongoni mwao anahitaji kuongea naye, akafika alipokwenda, akakata shauri na akampigia simu na huyu ndugu akamfuata na kuongea naye jambo fulani, walipolimaliza ndugu huyu akasema,
“Nitakupeleka Chimbo(sehemu inayouza nguo) moja la mashati mazuri sana ya kila rangi, maana wewe mara zote nakuona unavaa mashati meusi, natamani niwenakuona unavaa mashati ya kila rangi.”
Jamaa anayeambiwa maneno haya akasema sawa kisha ndugu huyu akaagana naye na kuwahi safari ile. Huyu jamaa alipobaki peke yake akawa anatafakari akisema huyu anayetaka kunionesha Chimbo la kununua mashati hivi anajua kuwa ninayo mashati mengi? Jamaa huyu akajiuliuza swali lingine vipi kwa mke wa Nyagali Mdude ambaye mumewe alichukuliwa na jamaa wasiojulikana na kupelekwa kusikujulikana huku akiachiwa michirizi ya damu iliyomwagika kutoka kwa mwili wa ndugu huyu wakati wa kumkamata nyumbani kwake, hivi akiamua kuvaa nguo nyeusi atakuwa hana nguo za kuvaa au moyoni mwake ana majonzi ya kupotelewa na mumewe?
Vipi kwa mke wa Ali Mohammed Kibao aliyetekwekwa katika basi, akapelekwa kusikujulikana na baadaye mwili wake kukutwa umeharibiwa na akiwa mfu, hivi mama huyu akiamua kuvaa kaniki akiomboleza msiba wa mumewe atakuwa hana khanga zingine za kuvaaa? Vipi kwa wazazi wa kijana Shadrack Chaula aliyepotea na hajulikania alipo hadi leo kama wazazi wake wakiamua kuhudhunika na kuamua kuvaa nguo nyeusi wakilia juu ya mtoto wao na kuamua kuvaa nguo nyeusi, je kufanya hivyo kuna maana hawana nguo zingine za kuvaa? Na wanatakiwa kuonesha chimbo linapouzwa nguo zenye rangi mbalimbali?
Ndugu huyu alicheka tu na kuendelea na shughuli zake.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Mwanakwetu akiwa anatafakari kisa hiki huku akijiuliza na huu mtindo mpya wa uvaaji wa nguo nyeusi ambao sasa unashika kasi na kila mmoja akiwa na lake moyoni, kama alivyovaa Balozi Humprey Polepole alipokuwa akizungumza na Watanzania mara baada ya kubwaga manyanga ya ubalozi wa Tanzania kule CUBA.
Mwanakwetu siku ya leo anatumia kisa hii cha uvaaji wa nguo nyeusi unaoendelea huku akitilia maanani juu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) chenye dhamani na ajenda ya Ulinzi na Usalama katika ilani yake je viongozi wa ngazi ya juu wa chama hiki je wanachukizwa na matukio haya ya utekaji, udhalilishaji na mauwaji? Na je CCM Taifa kinavyooneka kinachukua hatua sitaki kupambana na hali hii ?Je Watanzania wako salama kiasi gani huko tuemdapo?
Vipi kwa wanachama CCM waliowahi kuwa na dhamana kama Wakuu wa Kamati za Ulinzi na Usalama walichukua fomu na kutia nia ubunge kupitia CCM, kitendo cha Kamati Kuu kuwarejesha kupigiwa kuwa kwa wajumbe kuna maana gani kwa Watanzania? Mwanakwetu katika hili akistaajabu Kamati Kuu ya CCM Taifa kurejesha jina la aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Jumaa Zuberi Homera ambapo akiwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kinaja Shadrack Chaula na Kijana Mdude Nyagali hawajulikani walipo?
Msomaji wangu maswali ni mengi au ni yale yale ya malalamiko ya marehemu Kingunge Gombale Mwiru juu ya Kamati ya Maadili ya CCM Haina Maadili? Haya ni Mwanakwetu juu ya tafakari yake katika hili.
Mwanakwetu upo?
Kumbuka
“Girisi Mafuta ya Nazi.”
Nakutakia Siku Njema.
0717649257
Post a Comment