WANAWAKE MKOA MARA VINARA KUREJESHA MIKOPO

Adeladius Makwega-Musoma MARA

Katibu Tawala Mkoa wa Mara, ndugu Gerald Msabila Kusaya Juni 30, 2025 amefanya uzinduzi wa MTAKUWW



A ambao ni Mpango Mkakati wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto kwa kimkoa .

Akizungumza katika Uzinduzi huo ndugu Kusaya amesema kuwa,

“Mkoa wa Mara ni miongoni mwa mikoa nchini Tanzania yenye changamoto hii, sisi kama mkoa wa Mara lazima tuwe vinara wa kupambana na matukio haya na tutapambana, kwanza kuwawezesha akina mama wapatiwe asilimia 10 huku ninawaagiza wakurugenzi watendaji katika Halmashauri zote za mkoa wa Mara kuhakikisha lengo hili linafanikiwa kwa asilimia 100.”

Ndugu Kusaya alisema kuwa wanawake wa mkoa wa Mara ni vinara wa kurejesha mikopo kwa wakati na serikalia itaendelea kushirikiana nao begabega .

 

Katibu Tawala Kusaya aliagiza kila Halmashauri ya Mkoa wa Mara kutenga bajeti ya kujenga nyumba salama ili kuwasaidia mabinti wanapopata changamoto za unyanyasaji wapate fursa ya kuhifadhiwa hapo.

Sambamba na hili ndugu Kusaya alisema kuwa wazazi wa mkoa wa Mara wahakikishe chakula cha mchana kinapatikana shuleni maana hadi sasa chakula cha mchana kinapatikana kwa asilimia 54 tu hivyo kila mzazi achangie chakula cha mchana shuleni.

 

Wakizungumza katika uzinduzi huo baadhi ya washiriki kutoka Halmashauri zote za mkoa huu miongoni mwao ni Bi Jesca Msamba ambaye ni Afisa Ustawi Kiongozi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bunda amegusia hili,

“Ninafuraha kuona jitihada za Serikali katika kuendeleza mapambano ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto nchini nzima. Sisi Wilaya ya Bunda tumejipanga vizuri kuhakikisha shabaha hii ya Serikali inafanikiwa, tukiwa na jamii salama bila ukatili.”

Kwa upande wake Deogratius Mungure ambaye ni mwalimu ya Shule ya Msingi Nyarigamba A ambaye pia ni Mkalimali wa Lugha ya Alama aligusia na hili,

“Jamii ya Kitanzania inahitaji elimu ya kutosha juu ya ukatili wa kijinsia hasa watoto wenye ulemavu, maana yake yapo matukio kadhaa wanayofanyiwa watoto wenye ulemavu ambayo hayaripotiwi.”

Awali akizungumza wakati akimkaribisha Mgeni Rasmi na Katibu Tawala Mkoa wa Mara Bi Neema Ibamba ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Mara aliwapongeza washiriki wa uzinduzi wa mpango mkakati huu kuja na kushiriki shughuli hii pia alimshukuru sana Katibu Tawala Mkoa wa Mara Ndugu Kusaya kukubali kuzindua mpango huu.

 

Shughuli hii pia ilihudhuliwa na viongozi kadhaa wa taasisi za dini, vyama vya kijamii na vyama vya siasa kutoka wilaya zote za mkoa wa Mara.

makwadeladius@gmail.com

0717649257










 

 

 

 

0/Post a Comment/Comments