UKISHAIPA KISOGO DUNIA

 


Adeladius Makwega-MBAGALA

“Kijiti Aliniambia , Ondoka Mama Twende, Laiti Ningelijua , Ningekataa Nisiende, Kijiti Unaniua, Kwa Peji Moja ya Tende

Kiitikio

Kwa Peji Moja ya Tende, Kwa Peji Moja ya Tende, Kijiti Unaniua Kwa Kokwa Moja ya Tende

Jaji Amekasirika, Kitini Alipoketi Kasema Bilali fulu , Mashahidi wa Kijiti,Takufunga Sumaili, Na Kei Binti Subeti

Kiitikio

Na Kei Binti Subeti , Nakei Binti Subeti,Takufunga Sumaili, Na Kei Binti Subeti…”

Haya ni Mashairi na Viitikio vya Wimbo Kijiti wa Marehemu Bi Siti Binti Saad aliyezaliwa huku Zanzibara mwaka 1880 na kufariki Augosti 1950 , Mashairi na Viitikio hivyo ni kama vilivyohifadhiwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar. Kwa Walio wengi wimbo huu wanaufahamu kwa jina lake la Kijiti kama Ulivyoimbwa na  na Fatuma Binti Baraka (Bibi Kidude) yaani ambaye kwa hakika yeye kizazi kikubwa  cha Watanzania cha sasa kinamfahamu lakini wimbo huu kwa asilini ni Bi Siti Binti Saad.


 

Wimbo huu uliimbwa na Muimbaji Maarufu wa wakati wa Utawala wa Sultaan huko Zanzibar ambapo kulikuwa na matukio makubwa ya mauwaji ya watu wasio na hatia ambapo wimboni Mgeni aliuwawa na Mwenyeji wake  anayefahamika kama KIJITI.

Ukiusikiliza wimbo huu wenye mashairi kadhaa yote unaeleza namna huyu mgeni alivyopokelewa hadi anauwawa na beti za mwisho ambazo ni mbili  huku waimbaji wengi wa sasa wanaourudia wamekuwa wanazikwepa kuziimba ambazo zinaezelezea namna huyu Kijiti alivyopelekwa mahakamani mbele ya Jaji na kuhukumiwa.

Kwa hakika Mwanakwetu anatambua kuwa Taarabu kwa muda mrefu imekuwa ikitumika kama  burudani kubwa kuwaburidisha MABWENYENYE kama vile SULTAN lakini jambo jema linaoneshwa hapa ni kuwa  Bi Siti Binti Saad japokuwa alikuwa jirani na MABWENYENYE hakuonea aibu kulisema tabaka tawala  kwa baadhi ya vitendo ilivyokuwa inavifanya wakati huo na ndiyo maana hapa anapinga mauwaji anapinga  dhuluma ya nafsi za watu .

Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?


 

Kwa  sasa Tanzania ina shida  ya matukio ya kikatili, udhalilishaji na hata mauwaji ambayo yanalitesa taifa hili la Afrika ya Mashariki na kiu ya Watanzania wengi hawa wauwaji na watekaji wakamatwe na ili mahakama ije kutimiza wajibu wake. Waimbaji na wasanii wapo lakini ni waimbaji wangapi wanaliona hili na kulikemea?

Kibaya zaidi Tanzania inao utajiri mkubwa wa kazi za sanaa kama vile nyimbo na mashairi mengi yanayopinga matukio kama haya  je Chombo gani cha habari kimejaribu hata kuzicheza  nyimbo hizo kuonesha kuwa kipo pamoja na jamii yeye shida hiyo kwa sasa?


 

Makala ya Mwanakwetu siku ya leo yanalikumbusha hilo kwa vyombo vya habari tumieni hizi nyimbo.Wasanii wengi wanadhani nyimbo hizo ni za Sultan peke yake, hilo siyo sahihi nyimbo hizo ni za jamii nzima wanaofanya kazi za sanaa wajifunze katika wimbo huu wa KIJITI wa Bi Siti Binti Saad. Wasaniii msitunge nyimbo ambazo Ukishaipa KISOGO DUNIA  Hakuna Atakayeweza Kuikumbuka.

“Yule bwana/Yule bibi Kafa Mufilisi, maana ata alichokuwa akiimba hakina maana yoyote ile  si duniani wala akhera.”

Mwanakwetu Upo?

Kumbuka ,

“Ukishaipa Kisogo Dunia.”

Nakutakia Siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257

0/Post a Comment/Comments