Adeladius Makwega-MBAGALA
Ni siku nyingine, wakati mwingine nakualika tena msomaji wangu katika makala ya katuni siku ya leo, kumbuka haya ni Makala ya Katuni ambapo huchaguliwa katuni nne na katuni moja baada ya nyingine inaelezewa namna ilivyo, kisha inaelezewa maudhui ya katuni hiyo kwa jicho la Mtayarishaji Wetu.
Kuyaanza makala haya Mwanakwetu anaikamata katuni ya kwanza ambayo inaonesha mti mmoja mkubwa uliojaa ndege juu yake, huku anakuja mkataji wa mti huo, nao ndege mtini wengine wakiruka. Katuni hii imechorwa na Alwatan Masoud Kipanya. Kwa kuitazama vizuri katuni hii Mtayarishaji Wetu analinganisha hali hii na tukio la kupigwa Mkasi Usajili kwa Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Dkt. Josephart Gwajima.
Kwa maudhui yanayojengwa na katuni hii yanaonesha kuwa kitendo cha Kanisa hilo Kupigwa Mkasi ni sawa na kile kitendo cha Wayahudi cha Nitampiga Mchungaji wa Kondoo na Kundi Litatawanyika, hapa pengine Askofu Dkt. Gwajima akiwa kama Mti wa Kanisa lake ndiyo basi tena kanisa hilo litakuwa limekufa.
Mwanakwetu kwa katuni hii hana imani hiyo ya kanisa hilo kufa, huku akiamini kuwa uwepo wa Kanisa lolote kiimani huwa chini ya kiongozi wao siyo mwenye mwili na damu bali Kiongozi Mkuu wa Kanisa ni Yesu Mwenyewe, yeye ndiye mwenye Kanisa lake.
Mwanakwetu sasa anaikamata katuni ya pili iliyochorwa na tena na Masoud Kipanya ambayo inamuonesha jamaa kipanya kakaa katika Marufaa huku akibwabwaja, nayeye kama kawa bwabwajaji akiropoka jamani eehe tunaitaka Marekani iache haraka sana kukandamiza uhuru wa kujieleza.
Tunafuatalia kwa karibu kinachoendelea. Katuni hii kwa hakika Mwanakwetu anaona inatumia Mabalagha, kuzungumza kinyume ambapo katika kazi ya Sanaa Mabalagha inaweza kusaidia kufikisha ujumbe na kupunguza kesi kwa wanahabari na hata kwa kazi sanaa maana kinachozungumzwa kwa mtazamaji au msomaji anatambua si hivyo maana kimeandikwa kivingine.
Mwanakwetu anaikamata katuni ya tatu ambayo imechorwa na Alwatan Masoud Kipanya katika Katuni hii kunaonekana pipa moja kubwa likiwa na ngazi tatu na kuna kijana mdogo anachukua maji anajaribu kuyaweka katika pipa hili refu lakini kazi hiyo inakuwa ngumu.
Mtayarishaji wetu anaitazama katuni hii kwa umakini mkubwa na anadhani kinachoonekana huyu kijana anayechota maji na kuyaweka katika pipa kubwa ni vyama vingine vya siasa vya Tanzania kama vimebaini kuwa msimamo wa CHADEMA kuelekea uchaguzi Mkuu wa 2025 ni sahihi, hivyo basi vinatamani kuongeza nguvu katika Pipa Kubwa lililowazidi Kimo kwa kuyajaza maji kwa tabu kidogo.
Mwanakwetu sasa anaikamata katuni ya nne na ya mwisho ambayo imechorwa na Said wa Michael wa Shirika la Utangazaji la Ujerumano DW KISWAHILI, katuni hii anaonekana Waziri wa Fedha wa Tanzania Mhe Mwigulu Nchemba akiwa na begi kubwa la bajeti huku vijana kando wandesha bodaboda wanajiuliza jamani mnasikiliza bajeti iliyosoma Juni 12, 2025 Bungeni Dodoma?
Vijana wa bodboda wanasema tatizo muda, huku vikongwe wawili wamechoka wakimtazama namna Mhe Waziri Nchemba kama mzuka vile huyu alivyobeba begi kubwa lenye bajeti hii.Mwanakwetu kwa upande wake alifutalia bajeti hii kwa kina miongoni mwa yaliyosema yalikuwa haya,
“Mheshimiwa
Spika, katika bajeti ya mwaka 2024/25, Serikali ililenga kufikia malengo na
shabaha za uchumi na bajeti ambapo, mwaka 2024 Pato halisi la Taifa lilikua kwa
wastani wa asilimia 5.5 ikilinganishwa na lengo la asilimia 5.4. Aidha, katika
kipindi cha Julai 2024 hadi Mei 2025, wastani wa mfumuko wa bei ulikuwa
asilimia 3.1 ikiwa ni ndani ya lengo la wastani wa asilimia kati ya 3.0 - 5.0
katika muda wa kati. Vilevile, bajeti ilikuwa na malengo ya kisera ya kuongeza
uwezo wetu wa kuzalisha hapa nchini, hususan kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka
nchi za nje na zinazouzwa nje ya nchi ili kuongeza ajira na kuboresha mgawanyo
wa vipato kwa watanzania. Kutokana na utekelezaji wa sera hizo, nakisi ya urari
wa biashara ya bidhaa ilipungua kufikia dola za Marekani milioni 5,157.2 mwaka
2024.”
Mhe. Mwigulu Mchemba alitaja na hili,
“Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia mabadiliko hayo, sera za bajeti, mikakati ya kukusanya mapato pamoja na azma ya Serikali ya kudhibiti matumizi, Sura ya Bajeti inaonesha kuwa jumla ya shilingi168 trilioni 56.49 zinatarajiwa kukusanywa na kutumika katika mwaka 2025/26. Bajeti hiiinatarajiwa kugharamiwa na mapato ya ndani yashilingi trilioni 40.47, misaada shilingi trilioni 1.07 na mikopo ya shilingi trilioni 14.95. Kati ya mapato ya ndani yanayotarajiwa, mapato ya kodi ni shilingi trilioni 32.31, mapato yasiyo ya kodi shilingi trilioni 6.48, na mapato ya Mamlaka za Serikali za Mitaa shilingi trilioni 1.68. Aidha, mikopo inajumuisha shilingi trilioni 6.27 kutoka vyanzo vya ndani nashilingi trilioni 8.68 kutoka vyanzo vya nje.”
Mhe. Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba aliongeza na hili,
“Mhe Spika naomba nitumie fursa hii kuwashukuru wananchi wa jimbo la Iramba Magharibi walionia kura za kuwa Mbunge wao.”
Mwanakwetu kwa makala haya anampongeza sana Waziri wa Fedha Mhe Mwigulu Mchemba kwa kuisoma Bajeti hii vizuri, nakuomba nikuume sikio msomaji wangu Mwigulu Nchemba ni kiongozi makini sana na Wana Irambo Magharibi Mwanakwetu ninawaomba mumuunge mkono huyu jamaa arudi tena kuwa mbunge. Mhe Mwigulu Nchemba Mwanakwetu anakutakia kazi njema.
Basi msomaji wangu hadi hapo ndiyo natia nanga karika Makala ya Katuni, kumbuka nilikuwa na katuni nne; ile ya ndege juu ya mti na mkataji wa mti huo, ile ya mabalagha , katuni ya tatu ni hii ya pipa kubwa na katuni ya nne ni hii ya Bajeti Bungeni.
Kwa katuni hizo ndiyo na mimi nauufunga ukurasa huu wa Makala ya Katuni siku ya leo .
Mwanakwetu Upo? Kumbuka
“Pipa Kubwa Limewazidi Kimo.”
Nakutakia siku Njema.
0717649257
Post a Comment