PENTEKOSTI ITUKUMBUSHE UMOJA -KADINALI TAGLE

 


Adeladius Makwega-Bunda MARA

Mkuu wa Propaganda Fide ya Kanisa Katoliki inayojihusisha na Uinjilishaji wa watu, Kadinali Luis Antonie Tagle, amesema kuwa Jumapili ya Pentekosti itumike kutukumbusha umoja na ushirika baina yetu, maana kwa sasa dunia imegawanyika na Kanisa litumika kuujenga umoja huo, kwa sasa hofu inatumika kama silaha kubwa Ulimwenguni.

 

“Ndugu zangu wapendwa, inawezekana kwa mataifa mbalimbali ya ulimwengu kuelewana, ikiwa tu watu wengi zaidi watazungumza kwa uvuvio wa roho, wakiongozwa na roho ya kweli, ya ushirika na kuleta kwa kila mmoja lugha ya ushirika badala ya migawanyiko.Katika somo la pili kutoka Waraka wa Kwanza wa Mtakatifu Paulo kwa Wakorintho, tunaona kazi ya ushirika wa Roho Mtakatifu ndani ya jumuiya ya Wakristo, hapa tuna Bwana mmoja Yesu Kristo na sote tulibatizwa katika roho moja, hivyo ndani ya jumuiya ya Kikristo hakuna tofauti kati ya Wayahudi au Wagiriki, Mtumwa au Mtu huru, Tajiri au Maskini. Haya yote yazidishe ushirika wetu katika Roho Mtakatifu na Roho Mtakatifu atatugawia jumuiya karama mbalimbali ambazo hazipaswi kuwa za kushindana sisi kwa sisi bali karama hizo  zinapaswa kufanyia kazi katika ushirika wetu, kwa manufaa yetu sote. Ndugu zangu wapendwa, jumuiya zetu za kikristo, familia, zetu, parokia zetu, majimbo yetu yote yawe na lugha ya ushirika hasa kwa huu ulimwengu uliogawanyika, dunia tayari imegawanyika lakini ikiwa bado kanisa limegawanyika basi tunaongeza mgawanyiko. Katika Jumapili hii ya Pentekosti tupokee karama ya Roho Mtakatifu katika maisha yetu, katika jumuiya zetu ziwe ya matumaini na tuwe ya lugha yenye nguvu ya ushirika.”


 

Mahubiri ya Kadinali tagle yaliibua pia hali halisi ya uwoga wa mwanadamu wale hapa duniani, 

“Kumbukeni Mitume walivyokuwa chumbani, walijifungia kwa sababu ya kuwaogopa Wayahudi, ndugu zangu wapendwa adui mmoja wa ushirika ni kuwaogopa wengine, tunapoogopa kitu au jambo fulani tunajifungia na hakuna tena fursa ya ushirika.Ndiyo maana tunaona katika ulimwengu wetu wa leo, lugha ya hofu inatumika mara nyingi, watu wengi waovu wanapanda mbegu ya hofu na hiyo ndiyo silaha yao kubwa ya kutuangamiza, lakini sisi wenyewe tunapokuwa na hofu, tumejifungia ndani Bwana wetu Yesu Kristo yeye hupenya katika milango hiyo, hubomoa kuta hizo na badala yake hutusalimu kwa amani na utulivu, badala ya hofu tunapokea baraka zitokazo kwa Bwana Mfufuka, amani ya Bwana ni kubwa kuliko hofu zetu.Bwana mfufuka anatuhakikishia kuwa hatuna cha kuogopa, yeye ni mshindi wa dhambi na mauti, hii ni lugha nyingine ya ushirika inayotoka kwa Bwana Mfufuka.” 

Hayo yamesema katikaJumapili ya Pentekosti kupitia runinga ya Word Expose inayorusha hewanimahubiri ya Kadinali Tagle ambaye pia ni Askofu wa Jimbo la Albana huko Roma Italia. Akimalizia mahubiri yake Kadinali Tagle aliupigilia msumari wa mwisho katikla hili, 


 

“Katika Jumapili hii ya Kipentekoste, tunatakiwa kuifahamu tena na tena karama hii ya Baba, kwa njia ya Yesu Kristo na  Roho Mtakatifu, asemaye nasi lugha ya ushirika na katika lugha. Ninapotaja lugha simaanishi maneno tu , bali hata mitazamo, ishara, maamuzi, vipaumbele, vitendo vinavyohitajika hasa siku hizi, ambapo dunia inaonekana ina mwelekeo wa kugawanya tu, hakuna ubinadamu na kuna lugha nyingi za migawanyiko, hivyo Jumapili hii na mwaka ujao tuwe mawakala wa lugha ya ushirika.”

Wakati haya yakiendelea katika kuta, marufaa na Altare za Kanisa Ulimwenguni hapa Mkoani  Mara tangu Bunda, Musoma , Rorya, Tarime, Serengeti na Butiama hali ya hewa ni nzuri, huku mwandishi wa makala haya ameshuhudia wananchi wakiendelea na shughuli zao za kila siku, ikiwamo uvuvi, kilimo, ufugaji na uchimbaji wa madini.

Nakutakia Jumapili Njema ya Pentekosti.

makwadeladius@gmail.com

0717649257



















 

0/Post a Comment/Comments