Adeladius Makwega-MBAGALA
“Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya picha Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) ambaye pia ni Askofu wa Jimbo Katoliki Lindi, Mhashamu Wolfgang Pisa, wakati alipowasilisha salamu za pongezi kutoka kwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Baraza hilo, kwenye makazi ya Askofu, Mtanda mkoani Lindi, Julai 3.2024.”
Mwanakwetu yu nyumbani kwake Juni 22, 2025 ameutembelea ukurasa mmojawapo wa mitandao ya Kijamii wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na akukutana na picha hiyo ya Julai 3, 2024 kama ilivyodokeza karibu mwaka mmoja uliyopita.
Mwanakwetu akaupitia ukurasa huu na kisha kuuona Waraka wa TEC wa Juni 19, 2025 wenye kichwa
“Maboresho ya Liturujia Nchini Mwetu.”
Mwanakwetu akausoma huu waraka mara mbili, kisha akausoma mara ya tatu alafu akairudia tena na tena aya hii,
“Hakutokuwa na hotuba za kupongezana, isipokuwa mwadhimishaji atatambua kwa kifupi uwepo wa wageni wa Kidini, serikali, Kiimamii na Waalikwa wote bila kuwapa nafasi ya kuongea, kutoa hotuba wala kusalimia …”
Mwanakwetu akiwa anasoma aya hii , aya hiikicheko kikamtoka, hapa hapa akakumbuka mwaka wa 2007 akiwa anasoma Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa. Wakati huo Mwanakwetu alikuwa Makamu wa Rais wa Serikali ya Wanachuo hiki, siku chache wanachuo walikuwa na malalamiko mengi na migono ya chini kwa chini, mikopo imechelewa hivyo Serikali ya Wanachuo ilikuwa inalifanya kazi jambo hilo na hata Rais wa Wanachuo hao wakati huo huyu Antipas Zeno Mngungusi (Mbunge wa Malinyi-Morogoro mwaka 2020-2025) alikuwa amekwenda Bodi Mikopo Dar es Salaam kulitatua hilo.
Mwanakwetu nikawa na jukumu la kupitia katika madhehebu ya dini kuwaomba jamani msigome, tupo katika chuo cha dini, kwanza tufanye mazungumzo tukishindwa katika mazungumzo na mimi mwenyewe nitawaogoza katika mgomo, kwa hiyo baada kupitia katika madhehebu ya dini hali hiyo ikatulia na baadaye serikali ikatoa mikopo hiyo na kero kuisha.
Kumbuka Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa ni mali ya Kanisa la Kiinjilili la Kilutheri Tanzania, kwa hiyo kunakuwa na ibada moja kubwa sana ya Walutheri baadaye inakuja ibada ya Misa ya Wakatoliki ambao hakukuwa na waamini wengi na huku wanavijiji kando ya eneo wanaingia kusali na wanachuo.
Kwa desturi Mwanakwetu nilikuwa nasali Kigangoni Mtwivila ambapo wakati huo walikuwa wanajenga kanisa lao lakini mara nyingi nilikuwa nasali Jimboni Kihesa maana walikuwa na misa nyingi.
Siku moja nimetoka nyumbani, nilipokuwa nakaa Mtwivila nikasema nikasali Chuoni na Ibada ya Misa, Misa ya Wakatoliki ilikuwa saa tatu, nikaingia Kanisa nikasali vizuri, wakati wa kukomunika Viongozi wa Wakatoliki wakaniona na ulipofika wakati wa matangazo Katibu wa Wakatoliki akasema jamani pia leo tunaye Kaka yetu Adeladius Makwega ambaye ni Makamu wa Rais wa Serikali ya Wanachuo.
Hapa WanachuooWakatoliki na Waamini wanageuka nyuma kusubiri Mwanakwetu nikatoe ujumbe, nikiwa katika kiti nilichokaa nikasimama nakuomba samahani ,jamani naomba niongelea hapa hapa wala nisiisogolee katika marufaa na altare,
Waaamini wanasikiliza Mwanakwetu ananini?Mbona mara zote anakuja mbele kutoa neno alilonalo!
“Jamani eeeh samahanini sana, leo nimekuja Kanisani kama Mlei tu, Sijakuja kama Kiongozi, sina chochote cha kusema asante sana, Tumsifu Yesu Kristo.”
Waamini wakajibu milele Amina nayeye Mwanakwetu kuketi na tamati Baba Padri Ulungi alimalizia misa kwa kutoa baraka .
Baada ya Ibada ya Misa hii kwisha walihudhuria Misa hii wakawa wanamtania Mwanakwetu kwa maneno yake mwenyewe ibadani.
“Jamani naombeni niongelee hapa hapa, Nimekuja Kama Mlei jamani Leo Nimekuja Kama Mlei tu.”
Kweli baada ya utani huu wa Bwenini alikwenda Bwenini na Kijiji alikwenda Kijijini.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Kwa hakika Kanisa Katoliki limeshatoa mwongozi wake ambapo wababa wamekti na kuliamua hilo hivi sasa, kitabu kimefungwa.
Katika kisa hiki kumbuka namna Mwanakwetu alivyokuwa akizunguka katika Ibada na Misa Chuoni katika madhehebu mbalimbali kuwaomba na kuwasihi wanachuo wenzake wasigome na kwa kuwa alikuwa akiongea mbele ya madhabahu ya Bwana hakupata upinzani, somo lilieleweka vizuri sana, hapakuwepo na kuzomewa wala nini, mwishoni Padri au Mchungaji alisisitiza hilo kuupigia msumari wa mwisho na mambo yalikuwa mazuri.
Huo ulikuwa mchango mkubwa sana wa dini katika hali ngumu kama alivyojifunza Mwanakwetu akiwa kijana mdogo Chuo Kikuu ambapo serikali ilinufahiki. Ndiyo kusema kwa sasa manufaa haya kwa wale wanufahika kama Mwanakwetu wakati huu kwa Kanisa Katoliki hayapo tena na ndiyo basi tena.
Siku ya leo jaania Juni 22, 2025 Kadinal Luis Antonie Tagle Mkuu wa Propaganda Fide ya Kanisa Katoliki Inayojihusisha na Unjilishaji wa Watu Ulimwenguni amegusia hili,
“Tunaendelea na mtazamo wetu wa waraka wa urithi wa Baba Mtakatifu Leo wa XIII, katika vipindi viwili vilizopita tuliangazia waraka wa Rarum Novarum ambao ulitufundisha kutambua hadhi ya tabaka la wafanya kazi mbele ya ajenda za kibepari, pia tulibainisha msisitizo wake juu ya mazungumzo baina ya dini na hoja kwa pamoja zinapaswa kukamilishana na ambapo Kanisa na Serikali lazima kwa pamoja tuukamilishe mfululizo huu, kwa ushirikiano mzuri. Ibada za Baba Mtakatifu Leo XIII kwa Rozari Takatifu ya Bikira Maria aliyebarikiwa ilisababaishwa apewe jina la Baba Mtakatifu wa Rozari.”
Kwa hiyo msomaji wangu ukiona mambo tofauti ujue ni hatari sana.
Mwanakwetu upo?
Kumbuka
“Leo, Nimekuja Kama Mlei.”
Nakutakia Siku Njema.
0717649257
Post a Comment