MADENI YOTE YALIPWE KWA WAKATI-KANALI MTAMBI

Adeladius Makwega-Butiama-MARA

Ni majira ya Mchana ya Juni 10, 2025, jua la kadili linawaka, Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Alfred Mtambi, anawasili Wilaya ya Butiama, umbali mchache sana na lilipo kaburi la muasisi wa taifa hili Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kushiriki Mkutano Maalumu wa Baraza la Madiwani, juu ya Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) 2023/2024.

“Ukumbi wa Halmashauri ya Butiama ukiwa na umbo mraba, umejazwa na Madiwani, Wakuu wa Idara, Kamati ya Ulinzi na Usalama katika kikao chenye ajenda tatu; Kufungua Kikao, Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na ajenda ya mwisho ya Kuahirisha Kikao, ajenda ubaoni, kikao kinaendelea huku Kanali Matmbi akiambatana na Katibu Tawala Mkoa wa Mara Gerald Msabila Kusaya.”

Akizungumza mwanzoni mwa Kikao hiki Katibu wa Baraza la Madiwani, ambaye ndiye Mkurugenzi wa Butiama, Bi Aziza Juma Baneti aliliambia Baraza hilo,

“Halmashauri ya Butiama imekuwa inapata hati safi kwa miaka minne mfululizo, hili ni jambo zuri, Butiama tunatembea kifua mbele, tunashangwe tele , huku tukipiga vigelegele kutokana na kufanya kazi pamoja na vizuri tangu Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Peter Nyerere, Madiwani Wote, Wakuu wa Idara na wananchi wote wa Halmashauri ya Butiama.”

Bi Aziza Baneti baadaye alimkaribisha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Butiama Mhe. Peter Nyerere yeye kwanza kabisa alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mara kwa kushiriki katika Baraza hili lenye Ajenda moja kubwa ya kujibu hoja 17 mezani na akasema kikao kitakwenda kwa haraka na kwa ufanisi zaidi na kikao kimefunguliwa.


 

Mweka hazina wa Halmashauri hii Bi Upendo Alphonce Mbuni alitoa majibu ya hoja zote, huku akisoma katika majedwali kadhaaa kwa ueledi mkubwa. Hoja ilitajwa na majibu ya menejimenti na baadaye Baraza la Madiwani liliulizwa, waheshimiwa tunakubalaina? Swali likaulizwa waheshimiwa tunakubaliana, majibu yalikuwa ndiyo na baadaye Mhe Nyerere alisema,

“Waheshimiwa madiwani hapa Mhe. Mkuu wa Mkoa amenielekeza kuwa ni vizuri tupitie hoja moja baada nyingine na majibu kwa hoja moja baada ya nyingine yasikike.”

Kwa hakika hili likafanyika vizuri na hapo ndipo Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Mtambi akashika usukani.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Mh Kanali Mtambi alishauri Majibu ya Hoja yawe vizuri na ya uwazi na kuhusu madeni ya madiwani, Kanali Mtambi alishauri kila kinacholipwa na Halmashauri kionekana na kile kinacholipwa na Serikali Kuu kionekana na hasa malipo ya madiwani ambao walimaliza muda wao na hata wa sasa wanaomaliza muda wao.


 

Kanali Mtambi alisema kuwa yeye binafsi anayo matumaini kuwa Halmshauari ya Butiama itaendelea kupata hati safi hili ndiyo shabaha yake.

“Ninawatakeni madiwani na Baraza Zima muandae mpango kazi wa maagizo na hoja zote za ukaguzi zinafanyiwe kazi.”

Kanali Mtambi aliagiza yafuatayo

“Kuanzisha vyanzo vipya vya mapato kisha kuvisimamia vizuri vyanzo vilivyopo, mapato yanayokusanywa yahikishishwe yanapelekwa benki kwa wakati, ununuzi wa  kazi, huduma na vifaa ufuate mfumo na wale watumishi waliokiuka taratibu za ununuzi wachukuliwe hatua, ununuzi wa vifaa vya afya ufanyike MSD na vifaa ambavyo havipo MSD ununuzi ufanywe kwa wale wanunuzi waliochaguliwa tu,

Baraza la Madiwani lisimimamie utaratibu mpya wa kutoa mikopo na kutenga asilimia 10 na kuhakikisha wanakusanya madeni yote ya nyuma ili kuendelea kutoa mikopo, waliokopa wote warejeshe mikopo kwa wakati.

Kitengo cha ufuatiliaji na tathimini kiimarishwe kwa fedha na rasilimali watu. Fedha za watendaji vijijini zitengwe shilingi 200,000 kila robo kwa kila kijiji ili ofisi zao zifanye kazi vizuri.Wahakikishe wanakamilisha hatua zote za mgawanyo wa mali katika ya Halmashauri ya Musoma na Butiama na ninatoa siku 30 liwe limekamilika. Halmashauri ilipe madeni yote halali ya muda mrefu kwa wazabuni, wakandarasi na madeni mengine. Baraza la Madiwani litakapo vunjwa Menejimenti ya Halmashauri ya Butiama ifanye kazi vizuri.”

Awali akizungumza katika kikao hiki Mkuu wa Wilaya ya Butiama mhe. Moses Ludovick Kaegele alitumia muda huu kuwapongeza watumishi kwa kufanya kazi kwa bidii zote na sasa hali ya Butiama ni nzuri na Butiama itaendelea kumuenzi Baba wa Taifa hili Mwalimu Julius Nyerere.


 

makwadeladius@gmail.com

0717649257


 











0/Post a Comment/Comments