KANALI MTAMBI APIGA MBIU YA KONGAMANO LA MADINI

 


Adeladius Makwega-Musoma MARA.

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi, Juni 2, 2025 amefanya mazungumzo na wanahabari na kueleza kuwa Serikali ya Mkoa huu na wadau mbalimbali wameandaa Kongamano na Maonesho Makubwa ya Madini, yakishirikisha wadau kutoka hapa nchini na nje ya nchi, shabaha ikiwa kutangaza fursa za sekta ya madini Mkoani Mara kwa sasa.


 

Akizungumza katika kikao hiki kilichotumia dakika 33 alisema kuwa,

“Maonesho haya yanafanyika kwa siku nne, yaani Juni 3, juni 4 , juni 5 na juni 6, 2025 Shule ya Msingi Mkendo, Manispaa ya Musoma yakiwa na kauli mbiu Tuimarishe Uwekezaji Katika Sekta ya Madini Mkoani Mara na tushiriki Uchaguzi Mkuu 2025 Kwa Ajili ya Maendeleo ya Taifa letu.”

Akizungumzia umuhimu wa Maonesha na Kongamano hili, Kanali Mtambi alisema ni kuimarisha uwekezaji katika madini ndani ya Mkoa huu na taifa la Tanzania kwa ujumla huku akiongeza na hili,

“Kwa mkoa wa Mara katika pato lake la mwaka ni trilioni 6 na katika pato hili asilimia 18 inatokana na sekta ya madini .”

Awali Kanali Mtambi akipiga Bisimilai ya mazungumzo yake mbele ya vipaza sauti, tepu rekoda na kamera kadhaa za wanahabari amevipongeza vyombo vya vyote vya habari kwa kushirikiana na Serikali ya Mkoa wa Mara na viendeleze umoja na ushirikiano huu mwema.

makwadeladius @gmail.com

0717649257


 







0/Post a Comment/Comments