Adeladius Makwega Musoma MARA
Ni majira ya Jioni ya Mei 7, 2025 Gari iliyosheheni madawani, inapiga honi katika geti la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara na kufunguliwa na kisha madawati kadhaa kushushwa katika ofisi hii ya Mkuu wa Mkoa wa Mara .
Mwanakwetu alipofuatilia alijibiwa kuwa Wananchi wa Wilaya ya Musoma Mkoani Mara wameendelea kuitikiwa Wito wa Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Alfred Mtambi wa kuondoa uhaba madawati mashuleni na kutengeneza kwa hiari yao na kuyakabidhi kwa Serikali madawati kadhaa ambapo jioni hii zinapokelwa pea mia moja za meza na viti kutoka kwa Waisilamu wa Mji wa Musoma.
“Mkuu wa Mkoa wa Mara amekuwa anasisitiza kuwepo mahusiano bora baina ya Serikali na taasisi kadhaa zikiwamo za dini,
Hongereni sana kwa kufanya jambo hili. Mkuu wa Mkoa amenielekeza nipokee madawati haya na anatoa asante sana.”
Akizungumza katika hafla hii fupi mbele ya Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mara Shekh wa Mkoa wa Mara Ustadh Kassimu Msabaha, alimpongeza Mkuu wa Mkoa Mara kwa kushirikiana nao katika kila jambo analohusishwa na anasema hilo ni jambo zuri na huo ndiyo utamaduni wa Watanzania.
Katika hafla hiyo risala ya makabidhiano iliyosomwa na Ustadhi Rashid Saad Kaema ilinadi kuwa
“Sambamba na pea hizo 100 za meza na viti, Waisilamu wa Mji wa Musoma tutaendelea kushirikiana na Serikali zaidi na zaidi na kadili na Majaliwa na Mwenyenzi Mungu.”
Akishukuru kwa Niaba ya Halmashauri ya Musoma Vijijini Afisa Elimu Taaluma Bi Easter Kakulima alisema,
“Tuna upungufu wa madawati 3548 na kwa hiki kilichofanywa na Waislamu wa Musoma wametuunga
mkono na tunawashukuru sana, Mungu awabariki.”
Mara baada ya makabidhiano haya lilifanyika dua la kuiombea nchi ya Tanzania, kumuombea Rais Samia na kuuombea uchaguzi Mkuu na dua hili liliongozwa na Sheikh wa Mkoa wa Mara Ustadh Kassimu Msabaha.
0717649257
Post a Comment