KWA UTEKAJI NA MAUWAJI RAIS SAMIA AUNDE TUME YA UCHUNGUZI

 


Adeladius Makwega-MBAGALA

Julai 26, 2017 aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Paul Makonda alifanya tukio la ajabu kidogo kwa kuwapokonya Uafisa Elimu Kata Walimu 12 Jijini Dar es Salaam, baada ya walimu hapo kutoa maelezo ambayo Mkuu wa Mkoa huyo wakati huo hakulidhishwa nayo. Miongo mwa waliokumbwa na kadhia hiyo wakati huo ni Afisa Elimu Kata ya Mbagala Mwalimu Pindi.

Kwa hakika tukio hilo lilileta maneno mno, kwa watu wa Mbagala kuwa inakuwaje rais anawateua viongozi wenye roho za namna hiyo? Wanafanya maamuzi tu bila ya kujiuliza mara mbili mbili? Hata kufahamu mipaka ya nafasi zao? Haya yalikuwa maswali lakini kwa upande watu wasiofahamu miongozo ya elimu na taratibu za uendesha wa mambo ya Elimu kwa Tanzania walishangilia.

Mwanakwetu wakati tukio hili linatokea alikuwa Tanga na hata alipokwenda nyumbani kwao Mbagala aliuliza kwa kina Juu ya Mwalimu Pindi kilichomkuta na shule aliyopangiwa kufundisha baada ya tukio hilo.Nadhani itakuwa hekima kwa Mwanakwetu kumfahamisha zaidi msomaji wake juu ya Mwalimu Pindi namna wanavyofahamiana na Mwanakwetu.

“Kwa mara ya kwanza nilimfahamu Mwalimu Pindi kupitia marehemu Mzee Gonga ambaye alikuwa kada wa CCM Mbagala kwa Mangaya mapema ya 2005 kabla ya Uchaguzi Mkuu ambapo Mwanakwetu alipokwenda Mbagala kwao akitokea Iringa Vijijini–Isimani Sekondari wakati wa msiba wa jamaa mmoja alikutanishwa na Mzee Omari Idd Waziri na wapambe kadhaa juu ya majina ya wana CCM waliokuwa wakitaka kugombea ubunge kwa jimbo la Kigamboni akiwamo marehemu Yusufu Manji ambaye aliwahi kuwa Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu(Mikwemeni) ambapo marehemu Manji ni miongoni mwa koo zenye ardhi miaka mingi eneo hilo. Hapo yalizungumzwa mengi lakini Mwanakwetu alikuwa hakubaliani na siasa za Manji, baadaye Mwanakwetu alikata vikao vyao na alirudi Iringa kazini na baadaye kujiunga na Chuo Kikuu cha Tumaini Iringa. Katika kura za maoni CCM alishinda Yusufu Manji lakini Benjamin Mkapa akapindua Meza na kumchagua mshindi wa tatu Mwichumu Abudul rahaman Msomi na baadaye ndugu Mwinchumu kuwa Mbunge wa Jimbo la Kigamboni kutoka kwa Frank Magoba wa CUF.”

Sasa nakuomba msomaji wangu turudi katika kikao cha Julai 25, 2017 cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,hoja ambayo ilifanya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kufanya maamuzi hayo ni maelezo ya Dada wa Mwanakwetu Mwalimu Pindi kuwa pesa waliyokuwa wanapokea jukumu lake ni lilikuwa na kufanya wawe kama walivyo(HAIBA) ambapo hoja hiyo ilikubaliwa hadharani na walimu hao 12 japokuwa kuna kundi waliogopa kuusimamia huo ukweli. 


 Mwalimu Pindi

Kwa faida ya msomaji wa Mwanakwetu naomba ufahamu haya; Oktoba 20, 2014 Ndugu George G Yambesi akiwa ni Katibu Mkuu Utumishi alitoa waraka wenye karatasi tatu uliopewa jina WARAKA WA WATUMISHI WA SERIKALI NA. 3 WA MWAKA 2014-MSHAHARA NA POSHO ZA MADARAKA KWA VIONGOZI WA ELIMU.

“Madhumuni ya barua hii ilikuwa ni kuanisha sifa zinazohitajika katika ngazi mbalimbali za uongozi wa elimu, ngazi za mishahara na posho za madaraka kwa viongozi wa elimu katika ngazi mbalimbali za uongozi nchini.”

Kwa wale waliobahatika kuusoma waraka huu kama watakuwa na kumbukumbu nzuri kama za Mwalimu Mwanakwetu watakumbuka kuwa Ndugu George Yambesi alieleza kuwa,

“Posho ya madaraka kwa viongozi wa Elimu katika ngazi ya shule ya Msingi, sekondari na Vyuo itakuwa kama ifuatavyo; Mkuu wa Chuo Cha Ualimu atalipwa Posho ya Shilingi 300,000/ = kila mwezi, Mkaguzi wa Elimu Kata atalipwa posho ya Shilingi 250,000/=, Mkuu wa Shule ya Sekondari atalipwa Posho ya Shilingi 250,000/= na Mkuu wa Shule ya Msingi atalipwa posho ya shilingi 200,000/=.”

Kwa mujibu wa Waraka huu kama nakumbuka vizuri Mratibu Elimu Kata, Afisa Elimu Kata ulimtambua kama Mkaguzi wa Elimu Kata. Kwa faida tena ya  ya msomaji wa Mwanakwetu Waraka namba 3 wa Mwaka 2014 haukusema kabisa juu ya pesa hiyo itumike kama nauli au nini bali ni posho ya madaraka kwa wahusika hao. Hili linakuwa tofauti kwa wakuu wa Idara na Taasisi kupewa Posho ya Umeme, Maji na Simu. Ndiyo kusema majibu ya Mwalimu Pindi yalikuwa sahihi. Usahihi wake unakujaje?

“Hata baada ya Waratibu Elimu Kata baada ya kupewa Pikipiki nchi nzima Wakurugenzi Watendaji katika Kila halmashauri walitakiwa kuwapatia Waratibu Elimu Kata angalau lita 10 za mafuta kila mwezi ili waweze kuifanya kazi hiyo vizuri sambamba na hili shilingi 250,000/=.Ambalo ni jambo jema motisha ya Mratibu Elimu Kata hapa aonekana kama Afisa wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Kama pesa hiyo ikitumika kununua mafuta pikipiki Mratibu Elimu Kata akipewa lita 10 za Mafuta ay Mkurugenzi atalipa akipewa pesa ya mafuta ya Pikipiki.”

Katika kikao kile ndugu Paul Makonda mwenyewe na hata Katibu Tawala wake na hata Afisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam hata Wasaidizi wakati huo ilikuwa ni vigumu kuwa na uwezo wa kuukumbuka Waraka wa Watumishi wa Serikali Namba 3 wa mwaka 2014 juu ya Mishahara na Posho ya Madaraka kwa Viongozi wa Elimu, uwezo huo unahitaji ujuzi wa Utumishi wa Umma wa ngazi kubwa kama akina George Yambesi wenyewe ambao sasa wamestaafu tu. Kwa wale wanaofahamu nyaraka za Serikali zile Nyaraka za Elimu wanaweza kudhani kuwa Waraka huu ulikuwa miongoni mwa nyaraka za elimu la hasha hii ni Nyaraka ya Utumishi wa Umma ambao ulianza kutumika Julai 1, 2015 wakati Jakaya Kikwete na nduguye Mizengo Pinda wanakaribia kumaliza muda wao ofisini.


 

Mwanakwetu ninakumbuka hapa nilikuwa mwanahabari nikishiriki katika Matangazo ya Moja kwa Moja ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lile la 2015-2020, hiki kikiwa kipindi cha awali cha utekelezaji wa posho hizi yaani Juni 22, 2017 MHE. MUSSA Ramadhan SIMA-Mbunge wa CCM wa Singida Mjini aliuliza swali hili;

“Serikali imekuwa na dhamira ya dhati ya kuboresha maslahi ya Watumishi hususani Walimu kwa kutoa nyaraka mbalimbali ikiwemo Waraka wa Utumishi wa Serikali Na. 3 wa Oktoba 20, 2014 unaohusu mishahara na Posho ya Madaraka kwa Viongozi wa elimu (Responsibility Allowance): (a) Je, Serikali ina mpango gani wa kuanza kutekeleza waraka huo? (b) Je, Serikali ina mpango gani wa kutoa Posho ya Kufundishia (Teaching Allowance) ili kuleta ufanisi wa kazi?”

Swali hili na vipengele vyake lilijibiwa na Naibu Waziri wa TAMISEMI Dkt Seleiman Said Jafo kama ifuatavyo,

“Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mussa Ramadhani Sima, Mbunge wa Singida Mjini, lenye sehemu (a) na (b), kama ifuatavyo:-(a) Mheshimiwa Naibu Spika Serikali ilianza kutekeleza Waraka Na. 3 wa mwaka 2014 tangu Julai 1, 2016 kuhusu Posho ya Madaraka kwa Walimu Wakuu, Wakuu wa Shule na Waratibu wa Elimu Kata. Walimu Wakuu wanalipwa sh.200,000/= kila mwezi na Wakuu wa Shule na Waratibu Elimu Kata wanalipwa sh.250,000/= kila mwezi. Kwa mwezi mmoja, Serikali inatumia takriban shilingi bilioni 5.01 kwa ajili ya kulipa Posho za Madaraka kwa viongozi hao kwa ajili ya kuimarisha uongozi na usimamizi wa elimu.(b) Mheshimiwa Naibu Spika, posho ya kufundishia ilijumuishwa katika Mshahara wa Walimu ili kuboresha maslahi ya Walimu wanapostaafu. Hata hivyo, Serikali hivi sasa kupitia Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora inafanya mapitio ya kazi kwa watumishi wote nchini ili kuboresha maslahi kwa kuzingatia uzito wa kazi.”

Kwa kuwa jambo hili Mwanakwetu analifahamu sana naomba ifahamike hivi ;

“Pesa hizi za Posho ya Madaraka kwa utaratibu huwa zinaingia kila mwezi katika shule husika, huyu Mkuu wa Shule anaikuta katika akaunti ya shule yake kwa hiyo zikiingia anajua kuwa 200,000-250,000/= ni fedha yake nayeye Mratibu Elimu Kata/Mkaguzi Elimu Kata huwa pesa yake inawekwa katika shule moja za kata husika.‘Bosi njoo uchukue posho yetu imeingia anasem al-hamndulai wa Bilalamina anakwenda kuichukua.’ Mambo yanakuwa hivyo.”

Mwanakwetu sisemi haya kwa kuwa ninamfahamu Mwalimu Pindi la hasha bali nasema ili ule ukweli mambo ili kutoa elimu kwa umma. Awali makala haya nilipiga chapuo juu ya maneno ya watu wa Mbagala baada ya Madaam Pindi kuondolewa Uratibu Elimu Kata ya Mbagala.

“Kwa hakika tukio hilo lilileta maneno mno, kwa watu wa Mbagala kuwa inakuwaje rais anawateua viongozi wenye roho namna hii ambao wanafanya maamuzi tu bila ya kujiuliza mara mbili mbili?”

Mwanakwetu anajaribu kusafiri nawe msomaji wake huko kote kikubwa ni hasa ni tabia za viongozi wetu wajaribu kuwa na utu kwa jamii maana jamii na tekinolojia inarekodi haya matukio katika maktaba ya kumbukumbu. Mathalani hili suala la watu kutekwa , kupotea na kuuwawa wakati maeneo mbalimbali huku maeneo haya yana wenyeviti wa Kamati za Ulinzi na Usalama hadi ngazi ya Mkoa.


 

Kumekuwa na dhana ya wanajamii ya Tanzania kuutishwa mzigo huu kwa Jeshi la Polisi Tanzania, hilo kwa picha ya nje linaweza kuonekana lawama hizo ni za haki kwa Jeshi la Polisi lakini lakini lakini Mwanakwetu anaamini kuwa lawama hizo kwa Polisi Tanzania siyo sahihi.

Muhusika wa kwanza wa kuuliza ni Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi la Usalama kwa ngazi ya Mkoa Jeshi la Polisi. baadaye. Haya Mwanakwetu anayasema hasa kwa Mkoa wa Mbeya kwa ndugu yetu Juma Zuberi Homera maana Agost 2024 wakati anapotea Shadrak, ndugu yetu Juma Zuberi Homera ni Mkuu wa MKoa na amepokea mshahra wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa huo. Kibaya zaidi hata baada ya tukio la kutekwa kwa Mdude Nyagali ndugu Jumaa Zuberi Homera ametoka hadharani na kutoa ahadi ya kitita kwa Milioni tano kwa atakayefanikisha Mdude Nyagali kupatikana , mhilo lina maana kubwa kuwa yeye anawajibu mkubwa katika hilo.

“Kweli ndugu Homera anasimama na kutoa ahadi ya milioni tano kwa mtu atakaye mpata Ndude Nyagali , swali ilikuwaje kijana huyo anapotea ikiwa wewe ni msimamizi wa vyombo vya ulinzi na usalama?

Matukio haya mawili ya Shadrak Chaula na Mdude Nyagali ni deni analodaiwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ndugu yetu Juma Zuberi Homera kwa cheo chake.”

Haya Mwanakwetu aliyakumbuka tu na kuamua kuyaweka katika makala haya siku ya leo na iwe tafakari na uchambuzi juu ya maisha ya viongozi wetu hasa kwa ngazi ya MKUU WA MKOA.


 

Mwanakwetu anasema ni siku ya leo?

Kwa hakika usalama wa taifa letu ni jukumu la kila Mtanzania kuhakikisha binadamu mwenzake anakuwa salama ,Lakini kutokana na uwepo kwa tekinolojia za kisasa jambo hilo wanakabidhia vyombo vya ulinzi na usalama wenye mafunzo ili wao wawe vinara kwa kuwa wana mafunzo ya kutosha katika hilo, hawa ndugu wanakuwa chini ya viongozi wetu na wa mkoa wa Mbeya vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama Mwenyekiti wake ni Juma Zuberi Homera. Kunapotokea matukio ya kupotea watu na bila kujua kilichotokea na hakuna anayepatikana kufanya uhalifu huo kunavunja heshima ya mamlaka zilizokabidhiwa ikiwamo jukumu hilo huku wakiwa na mafunzo chini ya usimamizi wa Mkuu wa Mkoa Husika.

Mwanakwetu anashauri mamlaka ya Uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambayo ndiyo mamlaka inayopaswa kuunda Tume ya Uchunguzi, ikae na iunde Tume Maalumu kuangalia haya matukuio ya utekaji kuna nini nyuma yake , nani amefanya hivyo na kw amanufaa ya nani na kipi kifanyike?

Wahusika nambali moja wa kuhojiwa katika Tume hii ambayo Mwanakwetu anapendekeza iongozwe na Jaji wa Mahakama ya Rufaa wawe wajumbe wote wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya, waseme wanafahamu nini katika hilo? Wasema kipi kilichotokea katika kila matukio hayo? Kwanini kimetokea na wao wametimiza wajibu kiasi gani? Kisha rais afanyie kazi mapendekezo yote yatakayotolewa na TUME HIYO. Maana isije ikawa mambo kama yale yale ya Waraka wa Utumishi wa Umma Namba 3 wa Mwaka 2014 pengine Mkuu wa Mkoa Wetu hajausoma Waraka Huu? Na Maafisa wake Mkutanoni hawakuweza kukumbuka kilichomo katika Waraka huo, Maana Posho zingine ni kwa Ajili ya Haiba ya Mtumishi wa Umma kama alivyosema Mwlaimu Pindi lakini wapo wanaofahamu kwa kina Waraka huo akiwamo Mwalimu bora Mwanakwetu. Kwako Rais Samia malalamiko ni kwamba Mama Yetu ni Mzito wa Kuunda Tume za Uchunguzi nap engine wapo wanaofhamu juu ya haya mambo waje kuiambieaTume pengine hii michezo itakoma.


 

Mwanakwetu Upo? Kumbuka

“Rais Samia Aunde Tume ya Uchunguzi.”

Nakutakia Siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257







 

 

 

 

0/Post a Comment/Comments