WANAFUNZI WALE CHAKULA CHA MCHANA SHULENI-KANALI MTAMBI

 


Adeladius Makwega-Musoma MARA

“Miradi mingi inatolewa,

Yote inatekelezwa,

Tena kwa Kiwango bora

Veda’ Tunakupongeza.”

Ni majira ya jioni, hapa Mjini Musoma ndani ya Viwanja vya Mkendo, umati mkubwa wa watu umejaa mithili ya mashindano ya Ndondo Cup. Mwanakwetu anafika hapo na begi lake mgongoni na kushangaa kinachoendelea, huku masikio yake yakikaribishwa na mashairi ya kugani yenye maneno hayo.

Akiwa hapo mara akamuona kijana mmoja mrefu aliyevalia shati la kijani na suruali nyeusi, ndiye aliyekuwa akifurahisha hadhira hiyo huku shangwe za wananchi na meza kuu zikiendelea kupamba eneo hili.

Mara anamuona Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Alfred Mtambi yu meza kuu na hata alipouliza mwanahabari kandoni alijibu,

 ‘Mkoa wa Mara unaendelea kulitandaza jamvi lake la maboresho ya Elimu ya Msingi na Sekondari kwa kusisitiza utoaji wa chakula cha mchana shuleni kwa kila shule na kila mwanafunzi, huku wananchi wa mkoa huu wakiambiwa wahakikishe hilo.'

 Haya yanafanyika maana mlo wa chakula cha mchana shuleni unasaidia kupunguza utoro na kuongeza ufaulu mashuleni.”

Kweli Kanali Mtambi aliponyanyuka kitini alisisitiza kwa herufi kubwa katika hili,

“Nawakumbukusha suala la chakula cha mchana mashuleni, angalau mlo mmoja, hili suala halikwepeki, hili ni lazima kwa wana Mara wote, nawaombeni tuhakikishe chakula cha mchana kinachangiwa na kila mzazi/ mlezi mwenye mtoto shuleni kwetu.

Ninaomba nisisikie ubadhilifu wa chakula hicho, ninasema wazi sitomvumilia mtu yoyote atakayefanya ubadhilifu wa chakula cha wanafunzi shuleni.”

Akizungumza katika Mji huu wa Musoma Aprili 30, 2025 Kanali mtambi huku kandoni kukiwa na harakati za kuandaa uwanja huu kwa sherehe za Mei Mosi, 2025 Kimkoa.


 

Kanali Mtambi alisisitiza Wilaya zote za Mkoa wa Mara kuhakikisha zinakamilisha kutengenezwa madawati yote yaliyo pungufu na wanafunzi mkoa wa Mara ni mwiko kukaa chini.

“Tangu jana nilikuwa na vikao na viongozi wezangu juu suala hili hakuna mtu atakayevumiliwa kwa uzembe huu na ndiyo maana leo nimekuja kukabidhi madawati haya yaliyotengenezwa na wadau mbalimbali .”

Mwanakwetu alidokezwa kuwa awali kuwa akisoma taarifa ya Manispaa ya Musoma Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Mwalimu Bakari Sagini alisema kuwa Manispaa yake ina shule 65 ambapo 44 za msingi na 21 za Sekondari, shule hizo zina wanafunzi 55,764 shule za msingi zikiwa na wnafunzi 38,212 na Sekondari wanafunzi 17,552 wakiwa na upungufu wa madawati 4406 ambapo zoezi hili kukabidi madawati hayo linalofanyika ni kupambana kuyatengeneza madawati pungufu na zoezi linafanikiwa.

“Tunamshukuru Mbunge wa Musoma Mjini Vedasto Mathayo na wadau wengine kwa kufanikisha zoezi hili .”

Kwa hakika Mwanakwetu alishuhudia jukwaa kuu likiwa limepambwa na viongozi kadhaa akiwamo Mkuu wa Wilaya ya Musoma mhe.Jumaa Chikoka na viongozi wengine.

makwadeladius@gmail.com

0717649257


 









 

0/Post a Comment/Comments