WALIOPEWA JUKUMU LA KUKUSANYA USHAHIDI WAKISHINDWA KUFANYA HIVYO TUPIGE KELELE.

Adeladius Makwega-MBAGALA

Mwanakwetu bado na leo yupo katika kuta za Mahakama Kuu ya Tanzania, huku akiendelea kumtazama kwa miwani ya mbao Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungani waTanzania,mzee wake Profesa Ibrahimu Hamis Juma . Huyu ni Jaji Msomi.

Mwanakwetu siku ya leo anarudi nyuma kabisa miaka tisa iliyopita na kuipekua maktaba ya Habari ya Mahakama Kuu ya Tanzania juu ya baadhi ya kauli zilizowahi kutolewa na Jaji Mkuu wa Tanzania.

Hapa Mwanakwetu alikutana na hili la Septemba 21, 2017 Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahimu Hamis Juma alizungumza na vyombo vya habari juu ya tukio la kushambuliwa kwa aliyekuwa Mbunge wa Singida wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Tundu Lissu Jijini Dodoma.

Jaji Mkuu Profesa Jumaa aliyasema haya,

“Chama Cha Mawakili wa Uingereza wamezungumzia tukio lililotokea…Kwanza lile tukio ni la kiharifu, tukio la uharifu mkubwa na siyo uhalifu mdogo, jaribio la kuuwa, kitu cha kwanza ni kukusanya ushahidi na huo ushahidi utakusanywa hapa hapa Tanzania, asikudangnaye mtu kwamba mtu kutoka nje ndiyo atakuwa na uwezo wa kukusanya ushahidi.

Ushahidi unakusanywa hapa hapa.

Sasa sisi mahakamani haturuhusiwi kutoa maoni, ama kuongelea jambo ambalo tunaona moja kwa moja litakuja mahakamani. Kanuni zetu zipo wazi na ndiyo maana mnatuona kimya, kwenye mitandao mnajaribu kutuvuta tutoe maoni, hatutasema.

Ukweli ni kwamba kuna hakimu mmoja ameshambuliwa hadi amefariki, lakini hamjasikia tunalalamika, tunalaani, tunataka nyinyi mlaani.

Kwa hiyo tunataka sheria zifanye kazi zake.

Pale tutakapoona wale waliopewa jukumu la kukusanya ushahidi wanashindwa kufanya hivyo NI TUPIGE KELELE, ni hayo tu ninaweza kusema…

 Hili ni funzo, ni nafasi ya sisi kujiangalia je tumejipanga vizuri kupambana na uharifu unaokuja kutokea? Ukienda Nairobi kila pahala zipo CCTV Kamera…”

Mara baada ya ukanda huo wa video kutoka yalitolewa maoni mbalimbali ya Watanzania kutokana na maelezo haya ya Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahimu Hamisi Jumaa.


 

Wadau mbalimbali walitoa maoni na wa kwanza anayechaguliwa na Mwanakwetu siku ya leo ni FAINALI KIGULU anasema,

“Tenda Haki Hapa Duniani Hujiwekee Hazina Mbinguni na Umuogope Mungu Katika Maisha Yako Yote.”

Mdau mwingine akayasema haya,

“Mtakavyofanya sawa, kwani kuna atakayeishi miaka 100 !”

Maoni mengine yalikuwa haya,

“…Mimi kwa maoni yangu binafsi , pale aliposhambuliwa Tundu lissu ni sehemu inayolindwa na askari na kama ni hivyo mbona rahisi maana kuna utaratibu wa orodha ya wale waliokuwa zamu ya ulinzi siku ile eneo husika, jeshini wanaita Details, hao askari ndio watusaidie wahojiwe .”

Kwa hakika maoni yalikuwa mengi na wengine wakisema hata maeneo mengine CCTV zilikuwepo lakini mambo hayafanyiwi kazi na kwa hakika katika hili hata makazi ya Tundu Lissu CCTV Kamera zilikuwepo lakini…sasa ni miaka inayokaribia 10 kama ni mtoto yupo darasa la nne.


 

Kumbuka tu msomaji wnagu Mwanakwetu leo yupo katika kuta  za mahakama na akiikagua ile maktaba ya habari ya taasisi ambayo ni muhimili wa kutoa haki nchini Tanzania.

Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?

Kwa hakika Mwanakwetu ni Mtanzania ambaye msimamo wangu dhidi ya Jaji Mkuu wa Sasa kuongezwa muda anapinga na msimamo huo unabaki pale pale, ili kutoa fursa kwa Watanzania wengine na wenye nguvu mpya ya utendaji wa kazi katika muhimili huu nchini Tanzania.

Kwa ukweli wa Mungu kauli hii ya Jaji Mkuu Profesa Ibrahimu Hamisi Juma ni muhimu na inayopaswa kuheshimiwa japokuwa yapo baadhi ya mambo aliyoyasema  yanapaswa kupingwa  kwa hili Jaji Mkuu Profesa Ibrahimu Hamisi Juma kutambua haki ya KUPIGA KELELE nakupa SHIKAMOO.

Kikubwa suala hili la shambulio la Tundu Lissu lipo deni kwa taasisi zinazofanya uchunguzi zinadaiwa, unaweza kudhani zinadaiwa hilo na Tundu Lissu mwenyewe la hasha zinadaiwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hili linatia dosari chochote kinachofanywa dhidi ya Tundu Lissu, papo pahala panaonekana kuna sukurubu imelegea lakini hata wananchi kuziamini taasisi zinazofanya uchunguzi inakuwa vigumu.


 

Jaji Mkuu alisema wazi kuwa jamii inayo haki ya kupiga kelele. Kwa hiyo kwa makala haya Mwanakwetu anatumia haki hiyo kupiga kelele.

Hata kama Tundu Lissu anamashtaka ya Uhaini na yeye ana haki yake, waliomshambuliwa washungulikiwe na shauri liende mahakamani hata kama yupo Korokoni awe anakwenda kuona shauri lake waliomshambuliwa wanavyochukuliwa hatua nayeye shauri lake ya uhaini linaendelea.Vyombo vya uchunguzi inakuwa vigumu kuaminiwa na hapo ndipo hata wachunguzi wa nje wanapewa kipao mbele.

“Jamani hapa duniani tunaishi kipindi kifupi, hakuna mwenye makazi ya kudumu tujiulize sasa hivi John Pombe Magufuli hayupo, vyombo vya uchunguzi kulifanyia kazi hili jambo Watanzania watatambua kuwa kodi zao zinazotumika na taasisi hizo kwa haki na siyo vinginevyo.”

Mwanakwetu upo?

Kumbuka,

“Pale tutakaona wale waliopewa jukumu la kukusanya ushahidi wanashindwa kufanya hivyo NI TUPIGE KELELE.”

Nakutakia Suiku Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257

NB Makala haya yametayarishwa na Mwanakwetu kwa heshima ya Binamu yake Kipenzi Msekwa Njama ambaye ni mwalimu wa sekondari Jijini Dodoma.









 

 

 

 

 



0/Post a Comment/Comments