Adeladius Makwega-Musoma MARA
Wakristo wameambiwa kuwa Jumapili ya Pili ya Majilio, kuelekea Sikukuu ya Noeli ni wakati sahihi wa wao kujitafakari na kujiandaa kwa namna ya pekee kumpokea Kristo katika mioyo yao na waache kuishi kimazoea bali wabadilishe mienendo yao. Haya yamesemwa na Padri Augustine Mapambano katika Kanisa la Mtakatifu Yohane Paulo wa II Parokia ya Nyabange Bweri Jimbo Katoliki la Musoma, Jumapili ya Disemba 8, 2024.
Akihubiri katika misa hiyo, Padri Mapambano alisema kuwa wana wa Israel katika maisha yao walikata tamaa kabisa huku wakisema sasa tutavaaje vizuri na sasa tutafanyaje sherehe huku tukiwa katika maisha haya magumu na yenye dhiki tele?
Majibu yao waliyopata ni kuwa hata kama upo katika dhiki ya namna gani, kuwa na matumaini kwa Mungu ni jambo la msingi , hakuna lisilo na mwisho, kwa kuwa dhiki hiyo itafikia tamati yake na huo ndiyo ukombozi wa Yesu Kristo.
“Watazameni mama wajawazito wanavyoteseka na kuhangaika huku na kule, mwisho wa siku anajifungua salama, pia hata uwe katika maisha gani hivi tusikate tama maana sasa tunaye mkombozi wa ulimwengu ambaye ndiye Yesu Kristo.”
Akimalizia mahubiri ya misa hiii iliyoanza saa 12,30 Asubuhi, Padri mapambano alisema kuwa waamini wa Parokia hiyo waendelee kutoa michango yao kuboresha kanisa lao ambalo bado halijatabarukiwa,akisema zoezi hilo litafanyika mapema mwaka 2025.
Kwa hakika Kanisa la Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili Parokia ya Nyabange Bweri ni kubwa, la kisasa na nzuri huku bado halijakamlisha samani kadhaa kama vile mabenchi na nyumba ya Paroko ikiwa hatua za mwisho.
Mwandishi wa ripoti hii katikati ya misa hii wakati wa sadaka alishuhudia Padri Mapambano akimuagiza mlei mmoja ahesabu waamini ambao wamejiandaa kupokea, huku waamini hao hapo hapo wakanyoosha mikono juu naye Bwana Hesabu akazunguka pande zote tatu za kanisa hili kisha kujumlisha idadi na kumpa Padri Mapambano jumla kuu altareni.
Kitendo hiki kilimkumbusha mwandishi wa ripoti hii kuwa,
“Kati ya mwaka 1988-1991 akiwa na wenzake; Antony Masele na Robert Sinna walikuwa wakiambatana na Padr Wolfram kuelekea vigango vya Parokia ya Mbagala Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam huko Kigangoni Vikindu, Mkuranga, Kiparang’anda, Kise, Kisele , Magoza Kiziko na hata Dundani kutumikia misa ambapo wakati wa wimbo wa sadaka kazi hii ilifanywa nao na kumpa jumla hiyo Padri Wolfram, nazo misa hizo zilikuwa zinafanyika kila Jumapili ya tatu ya mwezi tu.”
Kwa hakika hali ya hewa ya mkoani Mara ni ya kushangaza kidogo maana ukiwa hapa Musoma Mjini mvua ndiyo zinanyesha watu wakipanda mahindi lakini huko Tarime tayari mahindi sasa wakulima wanayachoma na kuyachemsha vizuri tu, hili mwandishi wa ripoti hii akiona ni jema kwani kw ahali ya tahadhari Wilaya moja ikiwa na mavuno ya kutosha inaweza kuisaidia wilaya nyingine yenye dhiki.
0717649257
Post a Comment