Adeladius Makwega-MSAMVU-MOROGORO
Novemba 25, 2024 Mwanakwetu alipigiwa simu na ndugu mmoja akimjulisha kuwa mizigo yake imefika TRL Dodoma hivyo afunge safari hadi huku akaichukue, huku mpiga simu akimuomba afike mapema Novemba 26, 2024 ofisini mwao. Kweli Mwanakwetu alifika Dodoma na Novemba 26, 2024 alianza safari kudamkia TRL ambapo alipanda daladala moja makini huku Askari wa Usalama Barabarani wakisimamisha basi hilo na kuelewana vizuri na dereva wao. Mwanakwetu akiwa basini alikumbuka TRL enzi za Afisa Habari wao marehemu Midlady Maez ambaye amefariki mwaka huu.
Kwa hakika ndani ya basi hili kulikuwa kumejaa mno huku Mwanakwetu alikutana na jamaa mmoja aliyevalia fulani yenye maneno haya,
“Stone Lusinde Mbunge wa jimbo la Mvumi, Kazi ie ndelee.”
Mwanakwetu alipouliza basini juu ya Mbunge Stone Lusinde alijibiwa kuwa,
“Huyu ndiye muhaha Livingstone Lusinde ambaye awali alikuwa mbunge wa Mtera ambaye amezaliwa Machi 4, 1972.”
Majira ya saa tatu unusu ya asubuhi Mwanakwetu alifika TRL huku akikumbuka mchango mhe Lusinde juu ya machinga na na Benki ya Kilimo Bungeni.Kumbuka sasa Mwanakwetu yu TRL na hapa akabidhiwa mizigo yake vizuri lakini alibaini kuwa sanduku lake moja la chuma halikushushwa lilipitiliza hadi Dar es Salaam na Mungu bahati wahudumu wa TRL walipofuatilia walijibu kuwa ni kweli na lipo katika behewa na linaloelekea Dar es Salaam, sanduku hilo la chuma litarejeshwa Alhamisi.
Mwanakwetu akiwa TRL Dodoma alijifunza hili,
“Usafiri wa garimoshi ni wa uwakika sana unaposafirisha mizigo gharama zake ni nafuu na usalama wa mizigo ni mkubwa, huku watumishi wa TRL ni waaminifu wawe wenye ajira, wawe vibarua na hata wale wanaoshinda hapo. Wapo watumishi ambao ni vibarua lakini alipofika mwekezaji mhindi kufanya kazi la Shirika letu baadhi watumishi hao waliondolewa kama vile wabeba mizigo na wale wanaokagua njia. Kitendo cha kuwaondoa hawa watumishi dhana yake ilikuwa ni kupunguza gharama za uendeshaji lakini inaonekana zoezi hilo hata baada ya Serikali kurudi tena haikuwarejesha kazini watumishi waliyowekwa benchi.Kitendo hichi
kinaongeza gharama kubwa kwa wateja wa TRL akiwamo Mwanakwetu. Mathalanimzigo wa Mwanakwetu kutoka Marampaka hadi Dodoma amelipa karibu 395,000/= kwa stakabadhi yenye namba, wakati kupakia mzigo huo kwa Marampaka amelipa 70,000= na kushusha mzigo huo kituo cha Dodoma amelipa 60,000/= ambapo jumla yake ni 130,000/= ambapo hiyo ni pesa ya vibarua tu siyo ya serikali, kwa hakika hapa serikali inakosa mapato na hii ni kwa mteja mmoja tu. Fikiria kwa siku TRL Dodoma inashush kwa mfano mizigo ya wateja 25 zidisha kwa 150,000/= ya shusha pakia na zidisha mara siku 31 jumla ni 116,250,000/= Tena hapa nakuomba ondoa ushushaji na upakiaji wa mizigo ya kila mara mathalani Saruji kutoka viwandani.
Kumbuka pia hiyo 116,250,000 mara miezi 12 sawa na shilingi 1,395,000,000/= hii ni 1.4 Bilioni hapa tunapata vituo vya afya vitatu. Kwa hakika kazi hiyo inafanywa na kikosi cha watu wasiozidi watano na mshahara wa vibarua ni kati ya shilingi 270,000-350,000/=mara wafanyakzai watano na tena mara 12 ambayo ni shilingi 21,000,000/=”
Kumbuka msomaji wangu wakati huo Mwanakwetu mizigo yake inatolewa stoo na kupakiwa katika Lori, hapo hapo alifahamu jambo lingine,
“Hii kazi ya kushusha na kupakia mizigo inaweza kutumia wafanyakazi wachache kama tekinolojia ikiwa bora, kwa hiyo hata ajira ya watu watano ni kubwa, unaweza kuwa na wafanyakazi kati ya 3-4.”
Mwanakwetu alibeba mizigo yake na kuondoka zake kurudi Kijijini Chamwino Ikulu. Safari ilikwenda vizuri na alipofika kando ya Kituo cha Polisi Chamwino Ikulu aliona vijana wengi wa Jeshi la Polisi Tanzania wakiwa na sare zao.
Jamaa aliyekuwa kando na Mwanakwetu akasema maneno haya vijana wa Polisi wanajiandaa na shuguli za uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Mwanakwetu akasema hili ni zoezi la Kitaifa , jamaa kando akasema vijana wa watu wakafanye kazi kwa amani, naye Mwanakwetu akasema eee, ni vijana wadogo, wapo kazini wanatafuta maisha yao kama mimi na wewe tu, majumbani kwao wameacha wazazi na familia zao, nawatakia kazi njema. Mwanakwetu akafika kwake akashusha mizigo yake vizuri na baadaye kutoka kwake kwenda kutoa nakala ya nyaraka zake kadhaa.
Alipita kando ya Ofisi ya CCM Kijijini Chamwino Ikulu majira ya saa 6.30 mchana, hapa akakuta ofisi hii hakuna watu na mlango wa mbele umefungwa, Mwanakwetu akajiuliza, hawa CCM wapo wapi? Hawa jamaa kama hawan a uchaguzi?Au wameshamaliza kazi? Hawafanyi hata vikao vya ndani? Akilini Mwanakwetu akakumbuka mbona RPC Dodoma vijana wake wanajianda na uchaguzi? Inakuwaje chama tawala watu hawana wasiwasi?Wakati polisi wanajiandaa? Mwanakwetu kumbuka anakwenda kutoa vivuli vya nyaraka zake, akafika hapo akampa binti akatoa vivuli vya nyaraka zake na kumaliza kazi hiyo na hapa hapa mama mmoja akamuomba Mwanakwetu flashi yake, akampa naye Mwanakwetu akakaa katika benchi kwa muda kidogo kungoja mama huyu amalize kazi yake.
Akiwa hapo akakumbuka hili,
“RPC Dodoma vijana wake wamejaaKituoni wanapanga mikakati ya Ulinzi wa Raia na mali zao na usimamizi bora wa uchaguzi, huku ofisi ya CCM imefungwa au wapo ndani au labda wanazunguka mitaani? Vijana wa RPC Dodoma wanapokuwa pamoja kituoni hapa wanapeana uzoefu wa namna ya kuifanya kazi hiyo vizuri na kumbuka pengine wako vijana ambao hawajawahi kushiriki zoezi hili la uchaguzi, hapo polisi wanapeana uzoefu na wanarithishana huo uzoefu kutoka Polisi mmoja kwenda Polisi mwingine, vipi CCM mbona kimya na ofisi zilikuwa zimefungwa?”
Mwanakwetu alirudi nyumbani kwake na kuwapigia simu ndugu zake wa Kata ya Mbagala ambapo alipompigia simu diwani wa Mbagala Mh Michael Makwega alikuwa katika Mkutano wa kufunga kampeni na alijibu kaka tupo tunafunga kampeni, tafadhali nitumie ujumbe. Kumbuka mh Diwani Makwega anasema maneno haya huku nyimbo CCM zinasikika.Baadaye Mwanakwetu akaongea na Bi Amina Ngwele (Mama Mchafu) ambaye ni mgombea ujumbe kutoka Mtaa wa Kizinga nyumbani kwa akina Mwanakwetu, Bi Amina Ngwele akasema maneno haya,
“Mimi nashinda kwa kura nyingi tu, tena mchana kweupeeee… maana hizo kura zenyewe za maoni CCM nimepata kura nyingi, jamaa wa Upinzani waliona mimi ni mtaji, hivyo wakawa wanatupa maneno Bi Amina njoo huku, sisi tunakupa nafasi ya Kugombea Uenyekiti wa Mtaa,Mama Mchafu njoo upande wa pili,nikacheka,nikawajibu mimi ni zaidi ya huo wenyekiti wa mtaa, sina papara na hivi vyeo niacheni hapa hapa katika ujumbe, mimi nabaki na CCM.”
Baadaye Mwanakwetu akiwa hapa Kijijini Chamwino Ikulu akasikia nyimbo za CCM na hapo akasema kumbe hata Kijijini Chamwino Ikulu ile ofisi iliyofungwa kumbe sasa mlango umefunguliwa na sasa Kampeni zinafungwa kama kwetu Mbagala.Baadaye Mwanakwetu akaamua kuyatayarisha makala haya.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Kikubwa ni uchaguzi wa Serikali za Mtaa, wengi wa wanasiasa hata wa CCM inasikitisha wana shida ya moja fikra zao wakidhani tunafanya uchaguzi na shabaha ni moja tu ushindi, hilo siyo sahihi,narudia kusema hilo siyo sahihi , kikubwa tunafanya chaguzi ili kurithisha utarataibu wa uendeshaji wa mamlaka kwa njia ya amani, jamii iweze kuendelea na maisha yake kama ilivyo kuwa desturi,ashindee yoyote yule , iwe wewe iwe mimi kama ulivyopokea haya kutoka kwa waliyokutangulia je mamlaka yanahama kwa amani? Jamii inapokuwa katika uchaguzi lazima hatua kadhaa zifanyike kikamilifu ili kuwapa uzoefu wenye umri mdogo ili kurithisha haya mamlaka kwa amani , kwa hiyo yoyote yule anashindwa kurithisha mamlaka kwa amani hawezi kuwa na chake , watu tunataka maisha yetu ya leo , maisha yetu ya kesho na hata kesho kutwa yaendelea kuwa kama yalivyokuwa awali, watu wakiishi kwa amani. Suala ushindi wa John/Juma/Amina/Rose au chama chochote cha kisiasa halina maantiki kama mfumo wa maisha watu ukaharibika, watu wakauwawa hovyo.
Shabaha ya pili ya Mwanakwetu katika makala haya ni hili, suala la mizigo kwa TRL, ni vizuri wahusika hapo TRL kulifanyia kazi hususani maboresho ya nyenzo bora za kupakia na kushusha mizigo.
Kwa hakika Mwanakwetu moyo wake unazo chembe chembe za matumaini kwa haya mambo mawili kama yasipofanyiwa kazi leo, maandishi na sauti ya maneno ya makala haya yatabaki vizazi na vizazi na yatakuja kufanyiwa kazi tu, wakisema kumbe kuna jamaa aliwahi kusema haya.
Mwanakwetu upo?
Kumbuka,
“Njoo Upande wa Pili, mimi Nabaki na CCM, Chembe chembe za Matumaini.”
Nakutakia siku Njema
0717649257
Post a Comment