Adeladius Makwega-MWANZA
Wakristo wameambiwa kuwa utoaji wa taarifa kwa umma unahitaji umakini, ukiwa na takwimu halisi na bayana zenye uhalisi katika vijiji na mitaa ilipo jamii husika ili kuepuka kutoa taarifa zenye taharuki na hilo kusababisha jamii kushindwa kuendelea na shughuli zake za kila siku.
Haya yamesema na Padri Abel Nyalugeto ambaye ni Mlezi wa Shule ya Sekondari Archbishop Mayala katika mahubiri ya dominika ya 26 ya Mwaka Bee wa liturujia ya Kanisa Septemba 29, 2024 katika Kanisa la Bikira Maria –Malkia wa Wamisionari, Parokia ya Malya - Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza.
“Nyinyi Parokia ya Malya mna bahati hapa ndipo Ukristo wetu ulianzia, endeleeni kuishi katika umoja, msizuie zile karama njema lakini makarama mabaya kama vile ; UVIVU, hii siyo karama, UWONGO nayo siyo karama. Mwongo ni mshirika wa shetani, UCHOYO siyo karama ila UPENDO, UPOLE, UAMINIFU, FURAHA , AMANI na USAFI ndizo za kuendeleza Ili na KIPINDUPINDU KIONDOKE.
”
Padri Nyalugeto akifafanua juu ya USAFI alinyambua hilo kwa kina,
“Japokuwa tunaambia Kipindupidi kipo, je kipo wapi? Sasa si utoe TAKWIMU tujue vizuri? Maana yake mnatuchanganya, toeni takwimu ili tujikinge vizuri, sasa mnajenga hofu, watu wanashindwa hata kuja kusali,watu wafikiria wataambukizwa Kipindupindu, maisha ya hofu siyo mazuri, tuwe wakweli tuelezane ukweli, jamani sasa hivi kuna Kipindupindu watu kadhaa wa kadhaa wameambukizwa, jamani jiepushenijamani. Unaweza ukashangaa mtu anaibuka na kitu mathalani kule kwetu MALIGISU tunaambiwa kuna Kipindupindu Kigangoni tunaulizana hawa wenzetu wamekizulia wapi?”
Padri Abel Nyalugeto ambaye anaonekana ni msomi, akihubiri kwa maswali yanayohibua hoja zenye kuhitaji majibu, hoja zenye maantiki zinazohitaji kila mmoja kutimiza wajibu wake alipigilia msumari wa KIPINDUPIDU kuwa,
“Saa zingine tuwe na akili ya kuhoji kwa wataalamu wetu ili watueleze vizuri na sisi viongozi wa dini tunajikuta humo humo na kufikisha ujumbe ili watueleze vizuri. Mimi nikikaa kimya waumini wangu wanaweza kuwekewa kiovu lakini na nyie waumini siyo kwamba hatuwashauri munywe maji safi na salama lakini je hayo maji safi na salama mnayapata wapi? Wawezeshaji hayo maji safi na salama tutayapata wapi maji hayo? Vyoo vya kisasa tumeweka mara tunaambiwa vinaleta UTI lazima tukae kama jamii , tukae kama jumuiya kuyaweka mambo sawa na tukifanya hivyo tutamiza haja ya Mwenyeenzi Mungu ya kupendana.”
Katika ibada hii ya misa alikuwepo pia Paroko wa Parokia ya Malya Padr Samson Masanja aliyesoma Injili huku alitaniwa na Padri Nyalugeto kuwa waamini wa Malya wanalo jukumu lingine na kuhakikisa Padri wao anakula vinono ili anenepa siyo na siyo kila siku amekonda, baada ya misa hii kulifanyika pia harambee kubwa ya kukamilisha ujenzi wa vibanda vya Parokia hii huku Padri Nyalugeto alisema mradii huu ukikamilika utasadia kupunguza michango kwa waamini.
Katika ibada hii ya misa hali ya hewa angani inaonesha kuwa kana kwamba mvua zimekaribia huku ibadani kati ya saa 3 30 hadi saa 5 30 ya asubuhi umeme ulikatika mara mbili saa 4 03 na saa 5 09 hali hii ilisababisha Katekista wa zamu kutoka nje mara kadhaa kwenda kuwasha jenereta.
makwadeladius@gmail com
0717649257
Post a Comment