Adeladius Makwega-MWANZA
Msomaji wangu hii ni siku nyengine ambapo nakualika tena katika makala mengine ya katuni. Huu ni mkusanyiko wa katuni nne zenye maudhui mbalimbali, zikipachikwa, zikielezewa na kuchambuliwa kwa jicho la Mwanakwetu moja baada ya nyengine karibu.
Kwa kuyaanza makala haya, mikononi mwangu nina katuni inayoonesha mama mmoja amevaa suti yake ya kijivu na juu kapachika hijabu, akiwa kando ya ubao, haya ni mandhari ya darasani,ukiutazama ubao huo una michoro kadhaa na mahesabu, bila ya shaka huyu ni mwalimu wa mahesabu, mkono wa kushoto wa mwalimu huyu mwanamke kunaonesha grafu ambayo ilipanda alafu imeshuka.
Kwa hakika kulinganisha mavazi na wajihi wa mhusika huyu mwalimu pengine ni yule yule mwenye Jamhuri yake. Katuni hii ni ya kisiasa na siasa za Tanzania.
Mwanakwetu anavyoitazama katun hii na hasa huu mchoro wa grafu, mchoraji anaamini huyu mwenye jamhur yake amefanya kazi hadi grafu kupanda lakini imeshuka .Mwanakwetu anatambua na kuyaheshimu maoni haya ya mchoraji wa katuni na ndiyo maana yamepewa nafasi katika makala haya leo hii lakini hata kama grafu imeshuka Mwanakwetu anaamini bado huyu mama , mwalimu wetu wa mahesabu bado yupo darasani , kazi inaendelea na grafu itapanda, bado kuna mwaka na miezi 5.Mwanakwetu anaona mchoraji wa katuni hii tumpe nafasi ya miezi 15 ijayo aje achore katuni nyingine tuone atakuwa na maoni gani? Kwa sasa TumuacheAchape Kazi.
Sasa naisogeza katuni ya pili ambapo kunaonekana kibanda cha mchuuzi wa mazao ya chakula. Hapa kunaonekana kapu la nyanya zimeiva nyekunduuu , mapapai , ndizi mbivu na mbichi lakini pia kuna viazi na kando kuna chombo cha kutupa takataka na kunaonekana haya mazao chakula yaliyooza yametupwa hapo, huku inzi wakiruka huku na kule kwa shangwe tele. Huyu mchuuzi amevalia misurupwete na kibaya amejishika kichwa, kama amechanganyikiwe pengine kwa kukosa wateja. Kando kuna jamaa ambaye anamevaa suti maridadi, huku akinywa juisi kwa mrija, huyu jamaa koti lake limepewa kibandiko afisa wa serikali na afisa huyu akilini mwake anasema Kilimo ni Uti wa Mgongo wa Taifa .
Mwanakwetu anapoizama picha hii inasadifu kabisa mazingira ya wachuuzi wa mazao na matunda na mbogamboga wa Tanzania , ukisafari safar ndefu hawa ndugu wanaoneka huku wakikimbilia magari na mabasi kutafuta wateja. Mazao yao, mengi yanaharibika shida ni wateja. Jambo hili lazima lifanyiwe kazi na ndiyo maana katuni hii inapewa nafas leo hii katika makala haya.Kulingana na totuti ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania www.tanzania.go.tz kama ilivyotembelewa na Mwanakwetu Septemba Mosi, 2024 saa 10.58 jioni inaeleza haya;
“Nchini Tanzania, Sekta ya Kilimo ni muhimili wa maendeleo ya uchumi. Sekta hii inachangia kiasi cha nusu ya pato la Taifa, robo tatu ya bidhaa zinazouzwa nje ya nchi na chanzo cha chakula pamoja na utoaji wa fursa za ajira zaidi ya 75% ya Watanzania. Kilimo kina uhusiano na sekta zisizo kuwa za kilimo kupitia uhusiano wa usafishaji kwenda kwenye usindikaji wa mazao ya kilimo, matumizi na uuzaji nchi za nje;Inatoa malighafi kwa viwanda na soko kwa bidhaa zilizotengenezwa. Tanzania inazalisha takribani 97% ya mahitaji yake ya chakula. Uzalishaji wa mazao ya chakula unatofautiana mwaka hadi mwaka kutegemea kiasi cha mvua kilichopatikana.Maendeleo ya kilimo yamekuwa chini ya Serikali/fedha za umma kwa kipindi kirefu. Hata hivyo marekebisho ya uchumi kwa jumla yamekuwa na yanaendelea kuwa na matokeo ya muhimu kwenye sekta ya kilimo. Marekebisho ya kiuchumi yamesababisha kufunguka sekta hiyo kwa uwekezaji binafsi katika uzalishaji na usindikaji, uagizaji pembejeo za kutoka nchi za nje na usambazaji na masoko ya kilimo.”
Kwa hakika hii katuni inakumbusha serikalia wajibu wake kulitatua hili lililochorwa ili kuongeza tija maradufu kwa wakulima, wachuuzi na Watanzania wote.
Sasa ninaikamata katuni nyengine ambapo kunaonekana daladala ipo kando na kandakta anadai nauli kwa abiria wawili wa kike, kondakta huyu hao abiria wanawake wakiwa ndani ya dalaala alifanya kosa kwa kumuita mmoja mchumba, wakati wa kushuka mchumba hakulipa nauli, jamaa kando wamebaini kilichotokea wanasema mjini mwanamke hataniwi, hawa mabinti mmoja anasema umefanya kama kawaida yako, mwenzake anajibu si kaniita mwenyewe mchumba. Msomaji wangu haya ndiyo mambo ya mjini yalivyo Mwanakwetu hana cha kuongeza.
Sasa ninaikamata katuni ya nne ambapo kunaonekana ugomvi baina ya mhadhiri chuo kikuu na mwanafunzi wake wakiume wakimgombea binti.Mhadhiri anasema ukimgusa nakukamata katika mtihani, mwanafunzi anajibu mapigo ukimgusa namwambia mkeo. Kando binti mrembo anapita. Kwa chonjo kuna maneno haya. Ugonjwa Huu Mpaka Lini?.
Mwanakwetu upo?
Basi msomaji, kwa katuni ile ya mwalimu na grafu yake ubaoni, ya pili ni ile ya mchuuzi wa mazao ni kilimo uti wa mngongo, ya tatu ni hii kaniita mchumba wangu simlipi nauli na katuni ya mwisho ni ya ugomvi mapenzi vyuoni ,ndiyo na mimi nalifunga zulia hili la Uchambuzi Katika Makala ya Katuni siku ya leo.
Kumbuka,
“Tumuache Achape Kazi.”
Nakutakia Siku Njema.
0717649257
Post a Comment