KATUNI KITINDA MIMBA

 



Adeladius Makwega-MWANZA

Msikilizaji wangu nakualika tena katika makala ya katuni siku ya leo, haya ni makala ya  uchambuzi wa katuni mbalimbali kama zilivyokusanywa na Mwanakwetu zikiwa na maudhui mbalimbali kutoka vyanzo kadhaa bini kadha.

Nikianza kulipiga kasia ya makala haya siku leo nakutana na katuni iliyochorwa na ndugu Saidi Bini Mikaeli ambapo katuni hii pia imetumiwa na Shirika la Utangazaji la Ujerumani DW KISWAHILi . Katuni hii inaonesha watu watano wakiwa wamesimamishwa mstari hadharani, mstari ulinyooka wa kwanza amevaa shati zuri na amechomekea huku kapachika tai maridadi, kwapani ana faili limeandikwa MKOA , wa pili kuna jama amevaa mavazi ya kiaskofu , wa tatu kuna ustadhi akiwa katundika tasibihi na wanne kama jamaa aliyevalia sare za kipolisi naye kwapani ana faili limeandikwa DOLA.

Cha kusikitishwa jamaa hawa wanaulizwa kifkra na mtu watano juu ya Paulo Makonda yu wapi? Hawa jamaa wote wamepigwa zipu kutoka wa kwanza hadi wanne.Cha kustajabisha jamaa wa tano muuliza swali anauliza swali upande zipo ilipoanzia kufungwa

Huyu jamaa wa tano amepewa kibandiko wananchi na hao ndiyo wanauliza alipo mhe. Paulo Makonda. Katuni hii Mwanakwetu anakubaliana na swali hilo kuulizwa na pia lipewe majibu Maana Paulo Makonda ni ndugu yetu hata kama yako ambayo Mwanakwetu amekosoa sana juu ya utendaji wa kazi wa Makonda lakini Mtanzania mwenzetu, ni ndugu yetu na mwana CCM mwenzangu.Wenye majibu wajibu vizuri swali hilo huku kukiwa na majibu ya likizo iliyoombwaTAMISEMI.


 

Mwanakwetu anaiweka kando katuni hiyo ya Saidi wa Mikaeli ambayo Shirika la Utangazaji la Ujerumani imepanguvu zaidi na sasa anachukua katuni ya pili kutoka kwa alwatani Masod Kipanya na yeye hapa ana  katuni inayooneesha mandhari ya makaburini ambapo kuna makaburi tele yenye misalaba na kaburi moja anaonekana jamaa amefufuka kutoka wafu na jamaa huyu kibandiko chake kina neno TLS TANGANYIKA LAWS Hiki ni chama cha Mawakili wa Tanganyika ambacho kimefanya uchaguzi wake hivi punde na kumchagua wakili msomi Mwambukusi kushika nafasi ya Urais wa chama hicho.

Mwanakwetu anaitaza katuni hii ambapo imebeba matumaini makubwa kwa Wakili msomi Mwambukusi ambaye ni mwanasiasa machachari wa Tanzania siyo mwanasiasa dhaifu. Alwatan Masod Kipanya mchoraji wa katuni hii anayo matumani makubwa ya Rais Mpya wa TLS. Hilo Mwanakwetu anakubaliana nalo lakini anamkumbusha mchoraji wa katuni hii kwamba kuwa na matumaini na mtu n hatua ya kwanza na matumani kukamilika ni hatua ya pili, hivyo Wakili Msomi Mwambukusi nakutakia kazi njema hapo TLS na unawajibu wa kuyalinda matumaini ya wanachama waliyokupigia kura, wanufahika wa TLS ambao ni Watanzania  wote hata sie wanahabari Masod Kipanya na Mwanakwetu.


 

Nakubeba mzega mzega msomaji wangu hadi katika katuni ya tatu ambayo inaonesha kitanda kizuri kimetandikwa maridadi huku kikiwa kimelaliwa na joka cha kustajabisha joka hilo lina mkia mkubwa. Chumba hiki kinaonekana kizuri chenye kiyoyozi , kimezimwa taa, huu ni usiku wa manane. Mchoraji wa katuni hii ameibuka na dhana ya kulipa joka tabia za kibinadamu kutembea sakafuni, kupanda kitanda na kujifunika kitandani. Je Joka hilo limewezaje kuyafanya matendo haya?

Mchoraji wa katuni analipiga kasia lake kwa kasi tele za sifa hizo za joka na kuibua wazo kuwa wako binadamu wanaweza kuwa na sifa la joka kubwa ambalo linaweza kutumeza bila kutarajia na pengine sifa hizo zinaoneka tu pale zikizimwa, hivyo umakini unahitajika kikubwa tutayambua hilo joka kwa matendo tu na si vinginevyo.

Msomaji wangu naivuta kwa mikogo katuni ya King Kinya ambapo kuna vifaa saba vinavyotoa sauti  ya MAMA MAMA MAMA…Vifaa hivyo ; Redio, runinga  ,gitaa, mpira wa soka, kipaza sauti, simu na marufaa ya kuongele mikutanoni.

Mwanakwetu anajiuliza inakuwaje vifaa hivyo vyote vinatoa sauti moja?Sauti yenyewe ya mama mama mama wakati mama huwa na  baba mara zote ?Mwanakwetu inamjia tafakari kuwa Kinga Kinya anaibua hoja ya Tanzania kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025 Rais Samia Suluhu Hassan kila kona anatajwa yeye.

Swali ambalo linabaki kwa Mwanakwetu je vyombo vinafanya hivyo kweli au propaganda ya KING KINYA? Mwanakwetu anasema tusiandikie mate na maneno na 2025 si mbali kubwa tuombe uhai .

Basi kwa katuni hizo nne siku ya leo ile ya jamaa waliyofungwa zipu, ile ya kufufuka kwa TLS , ile ya Joka kitandani na hii Katuni Kitinda Mimba ya mama mama na vyombo saba ndiyo namalizia makala haya ya katuni siku ya leo.

Mwanakwetu Upo?

Kumbuka

“Vifaaa Sabaa Vinavomtajaa Mamaa–Katuni Kitinda Mimba.”

Ndiyo na mimi nashusha nanga bahari katika makala haya ya Uchambuzi wa Katuni siku ya leo.

Nakutakia Siku Njema.

makwadeladius@gmail.cm

0717649257


 

0/Post a Comment/Comments