NYIMBO NYINGI KUMUIMBA SALIMA.

 


Adeladius Makwega-MWANZA

Siku hii ilianza kwa kwa bahati mbaya ambapo Kompyuta Mpakato ya Mwanakwetu iliharibika, hivyo alitoka kwake hadi kwa fundi ili kukiweka sawa kifaa hicho. Alipofika kwa fundi ambaye alikuwa kijana alisema maneno haya,

“Mwanakwetu nimekusoma katika makala yako ya Fomu Moja tangu Mashinani hadi Nchani, sasa tunasubiri tu chama chetu kituambie.”

Kijana huyu ambaye kaka yake ni miongoni mwa Makatibu Kata wa CCM waliyopokea Pikipiki kutoka kwa Mwenyekti wa CCM Taifa mwaka huu wa 2024 akisema,

“Matamko ya viongozi yanatolewa lakini ajenda halali za chama zinatakiwa zianzie Mashinani hadi Taifa, siyo ajenda za overlap hadi nchani tu.”

Mwanakwetu akakabidhi kifaa chake vizuri na huyu kijana fundi kuanza matengenezo. Mwanakwetu akasema moyoni,

“Hawa ndiyo wenye chama chao, akina Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi na wenginepo kwenye CCM wao ni vibarua ambao wamepewa ngwe tu na ndiyo maana wanalipwa posho na stahiki zingine katika chama hiki.”

Mwanakwetu akiwa hapo mara akaingia binti mmoja mdogo mwenye umri kati ya miaka 18-24. Binti huyu akasalimia wote waliokuwapo hapo naye Mkongwe Mwanakwetu akapewa SHIKAMOO. Hapo hapo Mwanakwetu hakuvunga salaam hiyo akajibu MARAHABA. Fundi akaongea manemo mawili matatu na binti huyu na kuonesha wanafahamiana sana. Kisha fundi akamwambia Mwanakwetu,

“Huyu binti anasoma chuo hicho kando, anaitwa SALIMA, jina lake nalipenda sana maana jina SALIMA limeimbwa na wanamuziki wengi, inavyoonekana akina SALIMA ni mabingwa wa kuchanganya madawa, wanawalaza watu macho wazi hadi wanamuziki wanakesha kuwatungia nyimbo, hawa hawa akina SALIMA wana mambo?”

Mwanakwetu akilini mwake akasema kweli maana zipo nymbo nyingi zenye jina la SALIMA.

 

“Linex, Franco Luambo, Marijani Rajabu, Papi Kocha, Lovy Longomba na wengine wengi. Msomaji wangu , je hao wote wameshalogwa na uchawi wa mapenzi wa akina SALIMA?”

Kijana Fundi akasema ,

“Mwanakwetu kuna kaka mmoja miongoni mwa mteja wangu wa kompyuta mara nyingine namtengenezea, kuna siku nashangaa meseji zake zinapotea njia na kuja kwangu zimekimlalamikia mke wake.Nikafunga safari hadi kwake , nikamkuta kachanganyikiwa kabisa, anaandika meseji ndefu anamtumia mpenzi wake aliyepo Mwanza, zile meseji zingine akawa anakosea zinatumwa kwangu na wat wengine, nilipofika kwake namuuliza kaka una shida gani? Akanijibu

’Nilijenga nyumba katika kiwanja cha shemeji yako, juzi nimekwenda Mwanza nimekuta kuna jamaa ndani, hilo limeniuzi sana, nisamehe kwa ujumbe huo kufika kwako.’

Mimi nikamwamba achana naye wewe endelea na maisha yako, pesa inatafutwa, duniani tumekuja kutafuta siyo kutafutana. Nilipota kwake nikapigiwa simu kuwa jamaa kapanda juu ya mti anataka kujinyonga. Wananchi waliposikia hilo wakasema huyu ni mtu mzima wale asitusumbue, yeye abaki huko juu ya mti aendelee kujinyoga sisi tunachofanya sasa hivi tunaanza kuukata huu mti ili tusipate tabu ya kumshusha baada ya kujinyonga-yeye aendelee na kusudio lake. Jamaa juu yamti alijiuliza maswali mengi mwisho wa siku hakujinyonga.”

Kumbuka msomaji wangu Mwanakwetu yupo kwa fundi, na kwa kando ya benchi la wateja SALIMA kajaa tele anacheka mwanzo mwisho.Fundi akaongeza kuwa huyu jamaa mwenyewe anayetaka kujinyonga ni mkubwa yaani MWANAKWETU ni kijana.

 SALIMA yu jirani ya Mwanakwetu akasema maneno haya,

“Mapenzi hayana umri uwe na mvi au laa, unaweza kumuona mtu mheshimiwa, mapenzi yakimchanganya uheshimiwa unahama.”

Hapo hapo gafla akaingia kijana mmoja ambaye alionekana ni mtumishi wa umma akatamani asimuliwe visa vilivyosimuliwa hapo awali, tape rekoda-Mwanakwetu akamsimulia huyu kijana huku akicheka sana, alafu akasema maneno haya,

“Kuna jamaa ni mwalimu , shule yake ikapata walimu wapya, huyu jamaa anaye mke na watoto kadhaa, walipofika walimu wapya akapata mpenzi mwingine, walikaa vizuri sana katika mahusiano yao, hata majirani wa nyumba ya mwalimu mgeni walimfahamu huyu mwalimu na mahusiano yake . Kuna siku hawa wapenzi hawakuonekana kazini.

Baada ya siku kadhaa watu wakashituka kulikoni? Hawa jamaa wako wape au wamekwena kula fugate Mbuga za Wanyama?Walimu wenzao wakasema Mshahara wenyewe wa ualimu nani wa kwenda Serengeti?

Walimu wakakata shauri hadi nyumba ya mwalim binti, walipofika jirani na makazi ya yule mwalimu binti wakawa wanasikia harufu mbaya wakavunja mlango na kuingia ndani na kukuta mwalimu wa kike amefariki mwili umeoza huku yule mwalimu kiume hajulikani alipo.

Mwisho wa siku shule husika na Halmashauri ya Wilaya husika waliyokuwa wakifanya kazi ilipoteza walimu wawili kwa mpigo hawapo kazini tena, huyu kafariki na mwingine katoroka akidaiwa kufanya mauwaji hay o nyuma ya pazia ikidaiwa ni wivu wa mapenzi.

Haya yote ni mambo ya mapenzi, mapenzi ni hatari.”

Kompyuta ya Mwanakwetu haikupona siku siku hiyo alitoka zake hapo na kurudi nyumbani kwake kibindoni akiwa na simulizi hii.


 

Mwanakwetu siku ya leo anasema nini?

Kwanza kabisa Mwanakwetu anakuomba msomaji wake utambue kuwa jina SALIMA linaundwa na herufi sita zenye konsonati tatu Seee, Leee na Meee. Pia jina hilo lina Irabu mbili Aaaa a Iiii, huku Irabu Aaaa ikijirudia.

Jina hilo lnaweza kuwa ni SALAMA, SALIMA SALMA, SAALIMA au SELIMA nakadhalika huku jina hilo likitumiwa kama jina la kiume kama litatamkwa SALIM, SALIMU jina hilo linatokana na lugha mbili Kiebrania N  a Kiarabu na maana yake ni AMANI.

Kwa Tanzania mtu mwenye jina hilo ambaye ni maarufu sana ni Mama SALMA KIKWETE ambaye ni mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM huku akiwa ni mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya nne wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete.

Mwanakwetu alifanya jitihada za kuwatafuta wanamuziki kadhaa kutoa majibu juu ya inakuwaje nyimbo nyingi zinaimbwa na kupewa jina SALIMA? Kwa bahati mbaya majibu hayakupatikana.

Mwanakwetu bado anaendelea kuyatafuta majibu na sasa amepanga kumtafua Mzee wetu na ndugu yetu Jakaya Kikwete atupe hekima ya hilo jina na kama Jakaya Kikwete akitoa kibali ataulizwa mhe Salma Kikwete mwneyewe.

Mwanakwetu Upo?


 

Kumbuka

“Kuna Siri Gani Nyimbo Nyingi Kumuimba SALIMA?”

Nakutakia Siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257


 



0/Post a Comment/Comments