Adeladius Makwega-MWANZA
Katibu Mkuu mmoja wa Wizara mojawapo nchini
alimuita mtumishi wake wa umma ili kuongea naye, kwa bahati nzuri kando ya
kikao hicho alishiriki kiongozi anayesimamia masuala ya kiutumishi.
“Ndugu yetu nimekuita bila shaka unafahamu nafasi
yangu na huyu kando ndiye anayesimamia masuala ya kiutumishi. Wewe ni mwandishi
mzuri lakini namna unavyoandika kana kwamba kama siyo mtumishi wa umma.
Jambo hilo linatukwaza na ndiyo maana tumekuita
na taratibu za kiutumsihi zinakataza hilo, kwa hiyo tunakuandikia barua kwa
kukiuka hilo ujieleze.”
Katibu Mkuu akatoa
nafasi ya Mkuu wa Utawala na Rasilimaliwatu nayeye akasema jambo katika hilo
hilo huku akinukuu vipengele vya kanuni za utumishi wa umma.
KIongozi huyu
alinukuu kanuni ya utumishi wa umma C.15(1) ya 2009,
“No correspondence which has passed between
Ministries, Independent Departments, Regions, Local Government Authorities or
between the public and Ministries/ Independent Departments/ Executive Agencies/
Regions/Local Government Authorities may be communicated to the Press or any
member of the public without the approval of the Chief Executive Officer
concerned.”
Hivyo ndivyo
ilivyonukuliwa na kiongozi wa rasilimali watu ana kuungwa mkono na Katibu Mkuu.Kikao hicho kilimalizika kidugu nayeye mtumishi
kukubaliana na aliyoambiwa na maisha yakaendelea kama kawaida. Baada ya kikao
hicho mtumishi husika alirejea kanuni iliyotajwa na alibaini kuwa kanuni hiyo
ya utumshi wa umma ilinukuliwa kwa kifupi na kipengele muhimu kuachwa ambapo
ilitakiwa kusomwa hivi,
“No correspondence
which has passed between Ministries, Independent Departments, Regions, Local
Government Authorities or between the public and Ministries/ Independent
Departments/ Executive Agencies/ Regions/Local Government Authorities may be communicated
to the Press or any member of the public without the approval of the Chief
Executive Officer concerned;
but information of
general nature which may be material assistance in discussing local questions
need not be withheld, provided that such information is not of confidential
nature or likely to infringe the privacy of others.”
Ndiyo kusema kwa kifupi siyo taarifa zote
zinatakiwa kuombwa kibali kwa wakubwa kwa mtumishi wa umma anapozitumia katika mijadala
kwa umma. Ndugu huyu alikwenda mbali zaidi na kufahamu kuwa hata katika Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 Sura ya 2 Marejeo ya 2008, nanukuu;
“18 (1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na
maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake na kutafuta, kupokea na kutoa habari na
dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana
uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati.”
Kwa
hakika maelezo ya ibara hiyo yako wazi na hayana mjadala .
Kwa
vigezo vya kanuni ya utumishi wa umma C 15 (1) ya 2009 na Ibara ya 18 ya Katiba
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hapo mtumishi huyu alisema hakuna
kigugumizi, haki yako ukiifahamu itumie ipasavyo, usipoitumia shauri ni lako
wewe mwenyewe na itapendeza kama haki hiyo utaitumia kwa maslahi ya wengi.
Kwan
ini siku ya leo Mwanakwetu anayandika makala haya?
Kubwa
ni kutokana na msiba wa Thadei Ole Mushi aliyefariki Dunia ambapo kwa mujibu wa
taarifa zilizotolewa mazishi yake ni Jumatano Februari 7, 2024 huko Kilimanjaro
akiwa ni miongoni mwa vijana wadogo wachache wa Kitanzania walioweza kutumia
kalamu zao kwa manufaa ya jamii ya wanyonge wa Tanzania.
Mara
baada ya msiba wa Thadei Ole Mushi, hakuna shaka mitaani nchini Tanzania yanazungumzwa
mengi na mojawapo ni kuwa Thadei Ole Mushi alikuwa mwalimu wa kawaida akiijenga
Tanzania katika kada hiyo.
Mwanakwetu
anachoweza kusema kwa leo ni kuwa Thadei Ole Mushi alikuwa Mtanzania aliyeitumia
vizuri ibara ya 18 ya katiba ya Jamhuri wa Tanzania katika kutoa maoni yake yenye
shabaha ya kumkomboa Mtanzania mnyonge.
“Swali la kujiuliza kwa kila mmoja wetu, wakati mwili wa Mtanzania huyu
kutoka mkoa Kilimnajaro unaporudishwa mavumbini, Je kila mmoja wetu popote
alipo anaitumia ipasavyo haki hiyo ya ibara ya 18?
Swala la pili je mimi na wewe tunazitumia vipi taaluma zetu tulizosomea
kwa manufaa ya wengi?”
Kwa
hakika kila mmoja anayo majibu yake, nakuomba msomaji wangu hayo majibu kaa
nayo moyoni alafu ujitathimini, kama tutapiwa kwa alama kati ya 1-100 % kila
mmoja atapata maksi zake , Mwanakwetu anaamini kuwa Thadei Ole Mushi alipata daraja
A katika hilo.
Wako
wanaodai kuwa Thadei Ole Mushi alikuwa Mwana CCM, hilo ni kweli swali ni Je
viongozi wa CCM wote walikuwa wanaridhika na mwenendo huo wa mwanachama wao?
Majibu
yanaweza kuwa pengine ni sawa na yaleyale ya mtumishi yule aliyeitwa na Katibu
Mkuu wake ofisini hadi kufikia kunukuliwa kwa kanuni ya utumishi wa umma C.15(1) ya
2009, kwa kifupi na mtumishi yule alikwenda mbali zaidi hadi kufikia ibara ya
18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mwanakwetu
anaamini kuwa Thadei Ole Mushi alitimiza vizuri katika ahadi ya nane ya Mwama CCM.
“Nitasema kweli daima, Fitina kwangu mwiko; Nitasema kweli daima fitina
kwangu mwiko.”
Katika
hilo ipo mifano mingi ya mambo yaliyosemwa na Thadei Ole Mushi na kufanyiwa
kazi baadaye, kilichokuwa kinapishana ni muda tu baada ya jambo hilo kuandikwa
na muda wa kulitekeleza, kama ikiwa
siku, juma, mwezi au mwaka.
Mwanakwetu
anaamini kuwa Thadei Ole Mushi yeye kama Mkristo alitimiza kikamilifu amri kuu
ya MAPENDO.
Mwanakwetu
kwa siku ya leo ananukuu kutoka Bibili Takafifu, kitabu cha Waebrania 12, 14 ,
“Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote na utakatifu, ambao bila
ya kuwa nao hakuna mtu atakayamwona Bwana.”
Mwanakwetu
anaamini kuwa yako mambo mengi ya kujifunza katika msiba wa Thadei Ole Mushi;
Kwanza
walioguswa na kifo chake,
Ni
Watanzania kutoka vyama mbalimbali vya siasa, iwe upinzani na hata CCM na viongozi
mbalimbali katika serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Kaka, rafiki na
ndugu yangu Thadei Ole Mushi, Mungu Baba yetu , akupe pumziko la milele
mbinguni. Kizazi chetu kimempoteza mwalimu, mchambuzi na mwanajamii kijana
aliyetumia maarifa na kalamu yake kutoa maoni na hisia zake katika nyanja
nyingi.”.
Hayo
ni ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe mhe . Mtaka Antony.
“Poleni sana sana.
Nimesikitishwa sana
na msiba huu. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
Tumempoteza kijana
mahiri katika kuwasilisha jumbe mbalimbali kwa jamii kupitia makala zake pendwa.
Lala Salama Ole
Thadei Mushi.”
Hayo
juu ni ya Balozi Hoyce Temu, Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika
Umoja wa Mataifa .
Jambo
la pili la kujifunza kutokana na msiba huo,
“Kwa wanahabari wote tunatakiwa kutumia vizuri kalamu zao. Thadei Ole
Mushi alifanya kazi nzuri ya kihabari, japokuwa hakuwa mwanahabari, hivyo wanahabari
tusipotimiza wajibu wetu ndani ya jamii wanaweza kuibuka akina Thadei Ole Mushi
wengi na wakasaidia jamii kuliko hata vyombo vya habari. Huku wanahabari hao wakiwa
miongoni mwa wafuatiliaji wa taarifa zake.
Wanahabari wa Tanzania tusifungwe na ajira, tusifungwe na itikadi,
tusifungwe na maslahi binafsi, tujali maslahi ya walio wengi ambao hawana sauti.
Hapa duniani tunakaa kipindi kifupi sana, ndugu yetu Thadei Ole Mushi
ameecha mke, ameacha watoto, ameecha kila kitu huku akirudi alipotoka na hiyo ni ya sisi sote, hiyo ni safari yetu. Kila mmoja atapimwa kile alichokisomea na
namna alivyoitumikia jamii yake”
Mwanakwetu
anaiweka chini kalamu yake katika makala haya ya buriani akitoa pole kwa
familia ya Thadei Ole Mushi tangu mkewe , watoto wake, wazazi, ndugu jamaa na
marafiki.
“Raha ya milele
uumpe ee Bwana na Mwanga wa Milele umuangazie apumzike kwa amani amina.”
Mwanakwetu
upo
Buriani
Thadei Ole Mushi.
0717649257
Post a Comment