Adeladius Makwega-MWANZA
Novemba 14, 2023 Mwanakwetu alipita pahala fulani
na hapo kulikuwa na mjadala wa siasa, kubwa lilikuwa ni maisha ya CCM baada ya
kifo cha Rais John Magufuli.
Mjadala huo kwa hakika ulikuwa mzuri na Mwanakwetu
alivutiwa sana na hoja za wadau hao
mmoja baada ya mwingine,
“Je
CCM inapaswa kuishi vile vile katika maisha yake ya kisiasa au chama hiki
kikongwe kinapaswa kubadilisha muelekeo wake wa namna ya kuzifanya siasa?”
Ndugu mmoja alisema wazi kuwa CCM inapaswa kubadilisha
muelekeo wa namna ya kuzifanya siasa za Tanzana na kinyume chaka kinapitwa na
wakati. Maneno hayo makali yaliibua mjadala mzito huku wengine wakipingana nayo.
“Uchaguzi
wa vyama vingi wa mwaka 1995 CCM ilimpitishaa Benjamin Mkapa, hapo jina la
ndugu huyu liliaminiwa na chama hiki na huku viongozi wake wakubwa akiwamo
Mwalimu Julius Nyerere akiliunga mkono. Nyuma ya jina hilo majina mengine ya
Cleopa David Msuya , Jakaya Mrisho Kikwete na Edward Lowassa yalilisindikiza.
Benjamin Mkapa aliposhinda Urais alitambua nafasi ya Jakaya Kikwete katika kukiendeleza
chama hiki kikongwe kubaki madarakani na kujenga umoja wa kitaifa, alimuamini ndugu
Kikwete kwa nafasi ile ile na huku jamii ya Watanzania ilimpenda mno ndugu Kikwete,
hilo lilionekana tangu mwaka 1995 hadi mwaka 2005 ambapo alikuwa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania. Jakaya Kikwete alipitishwa na chama hiki kwa mapenzi ya
wanachama na. Benjamni Mkapa alishinda mwaka 1995 kwa kuaminiwa.
Katika
utawala wa Rais Mkapa hakumnyumbisha kabisa Jakaya KIkwete, aliendelea kufanya kazi naye kwa kumtambulisha kimataifa maana ndani ya Tanzania alishaweza kukonga nyoyo zao mapema mno,
rejea kura zake ndani ya vikao vya CCM ambapo aliongoza kura za kwanza na
kushika nafasi ya pili katika kura za pili.
Mwaa
2015 CCM ilikuwa nawagombea wengi wa urais huku makamu wa Rais wa Jakaya
Kikwete ndugu Gharibu Mohammed Bilali na Waziri Wake Mkuu Mizengo Pinda walifunga
tela kugombea nafasi hiyo.
Makamu
wa Rais na Waziri Mkuu wao kama wana CCM
wana haki ya kugombea nafasi yoyote ile
swali ni Je Jakaya Kikwete kama alivyofanyiwa yeye na Benjamin Mkapa, je
alishindwa kumuandaa mtu kuchukua nafasi hiyo mapema? Hilo alishindwa kuwaambia
Bilali na Pinda mapema alafu wakakacha kuchukua fomu hiyo ya urais?
Je
viongozi wetu wanapokuwa na nafasi maofisini wanaishi kwa namna gani? Je wanakaa kidugu? Kiuwazi au wanishi kwa unafiki? Hadi
Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wachukue fomu ya Urais ndani ya CCM?
Je
John Mgufuli lilikuwa chaguo la Jakaya Kikwete?
Kura
alizopata John Magufuli wa CCM dhidi ya Edward Lowassa wa UKAWA katika uchaguzi
mkuu zilionesha fika kuwa tonge la CCM lilitaka kuponyoka .
Kura
za uchaguzi za mwaka 2015 hizo ndizo mwongozi, huyu alishinda 2015 aliyeendelea kuongoza Tanzania hadi 2020
na hadi kufariki 2021 na nafasi hiyo akachukua makamu wake.
Je
CCM iendelee kuishi kama ilivyozoea?”
Msomaji wangu mjadala huu unaendelea, huku wadau
kadhaa wakitoa maoni yao, naye Mwanakwetu akiwa karani hodari wa kuyanukuu neno
kwa neno mazungumzo hayo ya Watanzania wenzake.
“CCM
inapaswa kufahamu kuwa mwaka 1995 mgombea wake wa Urais wa miaka 10 yaani 2005
alikuwa anafahamika. Kwa mwaka 2025 tuamini kuwa mgombea wa urais wa CCM ndiye
rais wa sasa wa Tanzania, iwavyo na iwe , 2030 Mungu akipenda lazima Tanzania
iwe na rais mwingine .
Sasa
imebakia mwezi kufika 2024, maana yake kuna miaka mtano/sita kufika 2030, je
CCM mgombea wake wa urais ambaye yupo mioyoni mwa watu au yule anayeaminiwa ni
nani?
Ukimya
huo unatoa nafasi kubwa vyama vya upinzani kuzidi kujikita katika siasa za
Tanzania na kujikita kupimwa misimamo ya wagombea katika kutetea rasilimali
za taifa hili. Huku CCM wakiwa kimya au CCM itakuwa kama ile ya 2015 ya
wagombea lukuki huku Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wakigombea?”
Mwanakwetu mjadala wa ndugu hawa unandelea
vizuri.Sasa wadau hawa wakaja na ushauri kwa CCM
“Mosi
inatakiwa kuruhusu mijadala ya ndani yake(CCM) inayopishana kimawazo na
mijadala hiyo ipewe sauti ili Watanzania waseme jamani fulani anatufaaa baada
ya rais wa sasa kuondoka.
Kukaa
kimya CCM hakuna faida kwao bali hasara kubwa,
CCM
inatakiwa kuruhusu uchaguzi wa urais mwaka 2025 fomu ya Urais za CCM ziwe wazi
kwa wagombea wengi, hilo litakipa chama hiki heshima kubwa.
Kuruhusu
huku wana CCM kadhaa, kutatoa nafasi kubwa ya kuona majina ya wana CCM ambayo
wajumbe wa CCM vikaoni wanayakubali na kuyaunga mkono.
Kufanya
hivyo kutatoa picha kwa Watanzania wengine kuanza kuwaza moyoni mwao kumbe baada
ya mgombea wa Urais wa CCM ni fulani bini fulani kabla ya 2030.
Kwa
hakika CCM inaweza kuhofia jina la sasa kushindanishwa, hoja zikiwa mizengwe
wanaume dhidi ya wanawake.
CCM
haipaswi kuhofia mizengwe ya jinsia yoyote katika utawala wa taifa hili.2025
CCM inaweza kuwa na wagombea kadhaa hilo litasaidia kuwachuja mapema na
Watanzania watawachuja mapema na 2025
itapita salama kuliko kumuacha mgombea mmoja 2025 na kuliacha balaa hadi 2030.”
Mjadala huo ulikwisha naye Mwanakwetu
kuendelea na safari yake.
Je siku ya leo Mwanakwetu anasema nini?
Kwa sasa Katibu Itikadi na Ueneza CCM Taifa
Paulo Makonda anazunguka, basi CCM ingejipanga hata mtu mmoja mwenye ushawishi
wa kitaifa ambaye hana tuhumu za ili na lile mathalani huyu alituharibia umeme wetu au huyu anauza majenereta, mtu safi kwa Watanzania, anayezifahamu siasa za taifa hili, siyo wa kutengezwa sasa bali mtu aliyeyepo katika mfumo ya CCM tangu mdogo, ndugu aambatane na Paulo Makonda kukijenga
chama , huku nacho CCM kikimjenga ndugu huyo. wa kando. Maana sasa Paulo
Makonda anaaminika vizuri, anazungumza mambo ya watu.
CCM itazame muelekeo wa Watanzania zaidi
milioni 50 na haipaswi kumezwa na hoja za jinsia za viongozi wake. Kinyume
chake itakumbwa na shida na kila mmoja atautaka urais alafu inakuwa gombania
goli kama ilivyokuwa mwaka kwa 2015.
CCM ijifunze kwa Rais Benjamin Mkapa ,
uvumilivu wake na kulinda heshima ya CCM na kuwalinda Watanzania wengi hadi
uchaguzi wa 2005 ukapita salama. .
Mwanakwetu Upo?
Chama chochote cha siasa kisiishi kwa mazoea, na akipashwi kuhofia mizengo ya jinsia za wanachama wake. Hapo anatafutwa rais wa watu milioni zaidi 50 kuwavusha kutoka hatua moja kwenda nyingine.
Hiyo mizengwe ya wanachma haina shida bali ina tija kwa taifa na maslahi ya wengi na siyo mslahi ya mtu mmoja au jinsia yake.
Msihofie Mizengwe ya Wanaume.
Nakutakia siku Njema.
0717649257




Post a Comment