BINADAMU KUITWA MAJINA YA WANYAMA

 


Adeladius Makwega-MWANZA

Kwa muda mrefu Mwanakwetu amekuwa akikutana na watu wengi wenye asili ya makabila ya mkoa wa Ruvuma wakiwama Wamatengo, Wakisi, Wamanda , Wandendeule na Wangoni,  jambo moja zuri alilokutana nalo ni majina ya ndugu hawa kuwa yanavutia sana kuyasikia, ambayo yanalingana na majina ya wanyama, ndege na viumbe hai kadhaa.

Kwa hakika viumbe hao wanaopatikana katika mazingira ya binadamu jirani nao ndiyo majina yao yalichukuliwa na kuwabatiza binadamu kama yalivyo na mengine kuwekewa viambishi mwanzo aua mwisho .

“Komba, Makomba, Nyakomba, Nyoni, Katembo, Matembo, Nguruwe, Mkima,Kima, Sungura, Kunguru , Nyoka, Mapunda, Ngonyani, Mbawala, Kiboko na kadhalika.”

Majina haya yamekuwa yakitumika mno si kwa makabaila hayo tu bali makabila mengi ya kibantu. Mathalani jina SUNGURA linapatikana hata kwa makabila kama Wafipa .Ndiyo kusema yupo SUNGURA Mfipa na SUNGURA Mngoni na si adimu kumkuta SUNGURA wa makabila mengine ya pande zote nne za Tanzania.

Majina haya yapo ya aina mbili yale yanayotumiwa majina ya wanyama hao kwa KISWAHILI mathalani MBAWALA na yapo majina mengine yanayotumia majina ya asili ya makabila hayo .

Jina la mfano hapa linalotajwa ni NDUNGURU, yapo madai kuwa jina hilo linamaanisha SIMBILISI ambaye ni mnyama mfupi mdogo anayeishi katika mashino ardhini.



Mwanakwetu siku ya leo anasema nini?

Mwanakwetu anakuomba msomaji wake utambue mambo yafuatayo katika majina hayo.

Kwanza wanyama hao walikuwa wakipatikana katika mazingira jirani na huyo binadamu anayeitwa jina la Mnyama huyo.

Majina hayo yalitolewa kwa sababu ya baadhi ya tabia za binadamu zinazolingana na wanyama hao.

“Mathalani Tembo, Matembo, Katembo–Tabia za Nguvu za TEMBO.”

Hoja nyingine inayotolewa hapa ni baadhi ya watu kupachikwa majina hayo ilitokana na watu hao kujificha ugeni wao na kuonekana wao pia ni wenyeji wa eneo hilo.

Ndiyo kusema hata  akina KOMBA na MAPUNDA walikuwa na majina ya koo zao mengine na majina yalivuma na kuenea ni haya ya wanyama.

Kuficha huko asili yao kulisadia wao  kuonekana wenyeji na kuwa salama wao na familia zao.

Mwanakwetu Upo?

Hiyo ndiyo sababu ya binadamu kuitwa majina ya wanyama.

Nakutakia siku Njema

makwadeladius@gmail.com

0717649257





0/Post a Comment/Comments