Aprili 29, 2023 Mwanakwetu alikwenda kusali jumuiya,
alipotoka huko alirudi nyumbani kwake, akiwa hapo alifanya usafi kidogo wa nguo
zake na alipomaliza, akaichukua simu yake iliyokuwa katika chaji, alipoifungua
simu hiyo alikutana na ujumbe na picha mbalimbali katika makundi kadhaa
yaliyomo katika simu hiyo.
Picha mojawapo aliyoiona iiimuonesha mwanahabari Yotham
Ndembeka, rafiki wa Mwanakwetu, Kada wa CCM wa miaka mingi wakiwa na tabasamu
moja zuri na mzee wetu Bernad Membe.
Mwanakwetu aliitazama picha hiyo kwa umakini mkubwa,
alitafakari na aliliona wazi wazi tabasamu la mzee Membe (Mzee wa Londo-Mzee wa
nimtoe nisimtoe?) Mwanakwetu huku akiikodolea picha hiyo aliyakumbuka mambo makubwa
mawili: kwanza ni simulizi ya mtumishi wa benki huko mikoa ya kusini mwa
Tanzania na simulizi ya pili ni ya mafundisho yake ya Komuniyo ya Kwanza mwka
1988.
Kwa kuanza msomaji wake anaomba asiwe mchoyo aanze na
simulizi ya mtumishi wa benki huko mikoa ya kusini mwa Tanzania,
“KIjana mmoja Mkwere alikuwa akifanya kazi mikoa ya kusini
mwa Tanzania, nyumbani kwa mheshimiwa Bernad Membe. Kijana huyu alifuata na mtu
aliyekuwa na shida ya kuuza eneo lake, kijana wa benki hakuwa na fedha, hivyo
aliiomba benki yake anapofanya kazi mkopo na kuchukua fedhai hizo na kulinunua
eneo hilo. Kijana huyu alikuwa bado kijana sana, hakuwa na majukumu ya mke na
watoto. Hivyo alipata eneo hilo zuri sana ambalo lilikuwa kando na Bahari ya
Hindi. Eneo hilo kijana huyu alinunua kwa ngekewa tu maana muuzaji alikuwa na
shida hivyo mtumshi wa benki alibahatisha kulipata eneo hilo na kulipa pesa zote
taslimu. Kutokana naeneo hilo kuwa nzuri mheshimiwa Bernad Membe alivutiwa na eneo
hilo, hivyo mheshimwa wetu alimtuma mtu wake wa karibu kuulizia eneo hilo ni la
nani? Majibu yalipatikana kuwa ni la kijana anayefanya kazi benki ndiye
mmmiliki halali wa eneo hili makini. Mheshimiwa Bernad Membe alimtuma mtu wake
wa karibu kumfuata kijana huyu kuwa Mzee Londo amelihusudu eneo hilo hivyo
anataka kulinunua kwa bei atakayotaja kijana huyo wa Benki. Kijana wa Benki
alipofuatwa alimpokea mjumbe akamsikiliza akamjibu mjumbe kuwa yeye hauzi eneo
hilo. Mheshimwa Membe alijaribu kumbembeleza kijana huyo lakini kijana huyu
alikata kuliuza. Alifuatwa mtu mwingine kumshawishi kijana huyo lakini,
mheshimiwa wetu aligonga mwamba kulinunua eneo hilo hadi kesho na yule kijana wa
benki hadi hii eneo lake na amejenga makazi yake ambayo amepangisha .”
Mwanakwetu alipouliza je mheshimiwa
Membe hakutumia uaskari kanzu wake na Uwaziri wake kukutisha ? Kijana alijibu
kuwa hakufanya hivyo, japokuwa kijana wa benki uwoga ulimuingia lakini
mheshimwa Bernad Membe hakufisidi.
Mwanakwetu akamuuliza kama angefanya hivyo ungefanyaje?
“Nilipanga kumfuata mheshimiwa Jakaya Kikwete nyumbani kwake,
kama wangenisumbua.”
Mwanakwetu alipoitazama picha hiyo pia aliyakumbuka mafundisho
ya Komuniyo ya Kwanza akiwa kijana mdogo akifundishwa na Watawa wa Shirika la
Dada Wadogo Kanisa la Mtakatifu Antony wa Padua, Parokia Mbagala Jimbo Kuu Katoliki
la Dar es Salaam enzi hizo .Mtawa aliyefundisha mafundisho hayo aliitwa Sista
Getruda aliwambiwa maafunzo haya.
“Ni jambo la kawaida mno pale mtu anapoumizwa au kukerwa na
mtu mwingine kukasirika, maana hasira inakuja kutoka ndani yako, na hasira hizo
zinaweza kuibua mambo mengine ikiwamo kutaka kulipiza kisasi. Wakati hasira
hiyo inazidi inaweza kuwahusisha na watu wengine ambao hawakuwapo katika shida
hiyo. Hiyo ni hatari na ndiyo maana Biblia inaitaja hasira ni sumu.”
Haya yanaelezwa bayana katika kitabu
cha Waebrania 12: 15 ,
“Angalieni sana mtu ye yote asishindwe kupata neema ya Mungu,
na muwe waangalifu pasizuke chuki ambayo, kama mmea wenye sumu, inaweza kukua
ikaleta matatizo na kuwachafua wengi.”
Msomaji wangu kuwa makini, je unapenda sumu hiyo ikuumize wewe
na wale walio jirani na wewe? Mwanakwetu alilkumbuka kuwa Biblia inakwenda
mbali zaidi katika Waefeso 4.31,
“Ondoeni kabisa chuki yote, ghadhabu, hasira, ugomvi na
matusi, pamoja na kila aina ya uovu. Muwe wema na wenye mioyo ya upendo kati
yenu, na kusameheana kama Mungu alivyowasamehe kwa ajili ya Kristo, Watoto wa
Nuru.”
Msomaji wangu Mwanakwetu aliendelea kuyakumbuka haya, je
unawezaje kumsamehe huyo aliyekukosea? Mafundisho ya Mwanakwetu Komuniyo ya
Kwanza anakumbuka kuwa watawa hao walisema kuwa , KIla mmoja atambue umuhimu wa
msamaha ambopo Yesu aliutilia maanani mno wakati anawafundisha wanafunzi wake
namna ya kuongea na Mungu (kusali) rejea Matayo 6,12.
“Na utusamehe makossa yetu kama na sisi tulivyokwisha kuwasamehe
waliotukosea.”
Mafundisho ya Ukristo yanaelekeza kuwa ni lazima kila Mkirsito
amkatae shetani, rejea Waefeso 4, 26-27
“Kama mkikasirika, msikubali hasira yenu iwafanye mtende dhambi,
na wala msikae na hasira kutwa nzima. Msimpe ibilisi nafasi.”
Mwanakwetu alikumbuka kuwa Ukristo unakwenda mbali zaidi,
rejea Wakosai 3.13.
“Mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya
kumlaumu mwenzake: Kama bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.”
Mwanakwetu akachukua simu yake na kuiweka katika begi lake huku
akitabasamu kama tabasamu la mzee Membe akafunga mlango na kuondoka zake.
Je siku ya leo Mwanakwetu anasema nini?
Kama kilivyosimuliwa na kisa cha yule wa kijana wa Kikwere wa
benki juu ya Mheshimiwa Membe hakutumia cheo chake na wala uaskari kanzu
kumtisha yule kijana ambaye alikuwa hauzi eneo lake. Katika ulimwnegu wa sasa
wapo watu wanaotumia uaskari kanzu wetu na vyeo vyetu kuwatisha wengine hilo
halikubaliki. Bernad Membe ni mtu mzuri sana alikuwa anatambua kuwa Uaskari
kanzu na Uwaziri wake ni dhamana tu hiyo
ni mali ya Watanzania, hilo ni jambo zuri linapaswa kuigwa na kila mmoja
wetu ambaye atajaliwa kuisoma matini haya.
Katika kisa cha Mafundisho ya Komuniyo ya Kwanza ni kukumbushana
kumsamhe mwenzako aliyekukosea maana huo ndiyo Ukristo. Ndugu yangu tambua
msamaha wa Mungu kwako? Je unatambua na kuiheshimu sadaka aliyoitoa Bwana wetu
Yesu Kristo Msalabani? Yesu alifanya hivyo ili mimi na wewe tusamehewe dhambi zetu.
Je unaiheshimu sadaka hiyo ? Msomaji wangu usisite, samehe haraka na wala
usichelewe.
Mwanakwetu kwa heshima zote anawashukuru mno na kwa pamoja
Yotham Ndembeka na mheshimiwa Bernad Membe kwa picha hiyo nzuri iliyosaidia
kujenga tafakari hii.
0717649257
Post a Comment