Adeladius Makwega-MWANZA
Wakristo wameambiwa kuwa wanapobatizwa wanakubali kuungama
kifo na ufufuko wa Kristo, wataishi katika alama zake na huyo wanaemuamini na
huyo wanaemsadiki ndiye huyo huyo anayejitambulisha kwao leo kuwa yeye ni
mchungaji mwema. Hayo yamesemwa katika mahubiri ya Jumapili ya nne baada ya
Pasaka ya Mwaka A wa Liturjia ya Kanisa, Aprili 30, 2023 katika Kanisa la
Bikira Maria Mama wa Wamisionari, Parokia ya Malya , Jimbo Kuu Katoliki ya
Mwanza na Paroko wa Parokia hiyo, Padri Samwel Masanja.
“Mchungaji mwema ni yule aliyetayari kuyatoa maisha yake,
akiwalinda na kuwatetea kondoo wake. Katika mazingira yetu mfano huu ni mwepesi
sana kueleweka kwa sababu mazingira yetu ni ya wakulima na wafugaji, tunapozungumza
habari ya mchungaji kila mmoja anaelewa ni mtu mwenye kazi gani, ni mtu mwenye
jukumu gani. Mchungaji mwema ana jukumu la kuwafahamu na kuwatambua hao
anawachunga, hao anaowapeleka malishoni, hao ambao amekabidhiwa. Ndugu zangu mchungaji
mwema ni yule anayewangoza kondoo wake wapite katika njia iliyo sahihi.”
Awali akisoma somo la injili ya
Dominika hiyo Padri Masanja alisema,
“Yesu aliwaambia Wayahudi, amini amini nawaambieni yeye
asiyeingia mlangoni katika zizi la kondoo na ukwea kwenye zizi yeye ni mwizi na
mnyang’anyi, aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo, bawabu umfungulia huyo
na kondoo huisikia sauti yake, naye huwaita kondoo wake kwa majina yao na
kuwapeleka nje, naye awatoapo nje kondoo wake wote huwatangulia na wale kondoo
humfuta maana huijua sauti yake.”
Misa hiyo ya pili iliyoanza saa mbili
kamili ya asubuhi ikitanguliwa na misa ya kwanza iliyoanza saa kumi na mbili ya
asubuhi ilisindikizwa na nyimbo zilizoimbwa na kwaya ya Chuo cha Maendeleo ya
Wananchi Malya (FDC) ikiambatana na maombi kadhaa mojawapo lilikuwa hili,
“Eee Bwana Yesu, Kama mchungaji mwema, unatufungulia mlango
wa kumfahamu Mungu, kabla ya kufika kwake, utusaidie kuongozwa naye katika
maisha yetu, Ee Bwana.”
Kwaya hii ya Chuo cha Maendeleo ya
Wananchi Malya ilikuwa na mwanakwaya mmoja aliyekuwa akiimba sauti ya kwanza
akiwa nambali moja kwa waimbaji hao ambaye alionekana mgonjwa wakati misa hiyo
ikianza huku nyimbo kadhaa za awali alishindwa kusimama na kuimba lakini baada
ya muda alioneka hali yake ilitengemaa, alijisikia vizuri na kuendelea kuimba
hadi misa hiyo ilipomaliza.
Mpaka misa hiyo ya pili inamalizika hali ya hewa ya eneo hili la Malya Kwimba Mwanza lilikuwa na, mawingu , manyunyu, mvua na jua kidogo kwa juma zima huku baadhi ya wakulima wakilima mahindi na mbogamboga ambazo mwandishi wa ripoti hii ameshuhudia mazao hayo yapo katika hali nzuri.
Post a Comment