MWANA KIDONDA MJUKUU KOVU
Adeladius Makwega-Buigiri
Jioni ya Januari 30, 2023 mwanakwetu akiwa nyumbani kwake alipigiwa simu na nduguye mmoja ambaye alimsalimu huku akimwambia kuwa shule ya kwao Kingu Sekondari Morogoro Mjini haijapata sufuri hata moja wanajipongeza sana na imekuwa shule ya pili kwa mkoa wa Morogoro ikitanguliwa na Kilakala.
Mwanakwetu akashangaa mno na hizo takwimu za kuwa shule hii ni ya pili na hii ni ya kwanza mbona Baraza la Mitihani Tanzania wamekuwa na kigugumizi kutangaza hilo !
Mwanakwetu akajisemea moyoni Baraza la Mitihani linatakiwa kuzitangaza takwimu hizo mara moja ili kulinda na kuzuia kusambaa taarifa za uwongo juu ya shule ipi ya kwanza na ipi ya mwisho maana jamii ina kiu, kumbuka mwenye kiu anaweza kunywa hata maji ya mrejini.
Mwanakwetu akasema orodha ya kumi bora na kumi dhaifu bado haijatoka. Ndugu huyu akasema hilo liachwe kando alafu alimuuliza mwanakawetu umeona binti wa Franki Kidani amepiga daraja la kwanza kali ?
Mwanakwetu akauliza Frank Kidani ? Alafu akaelewa akacheka sana, alafu akasema hajayona matokeo hayo, jamaa akasema taarifa zipo mtandaoni, mwanakwetu akasema aah kumbe ! Frank Kidani ana binti mkubwa ? Jamaa akajibu ndiyo.
“Anaweza kuwa baba mkwe wako kabisa kabisa ” Mwanakwetu akacheka sana akasema mie biashara ya kuongeza majiko siiwezi na dini yangu inakataza labda wewe ?
Jamaa akajibu alafu binti mwenyewe mwanafunzi labda uwe na uvumilivu wa mitume miaka miwili ndiyo amalize kidato cha sita.
(MATOKEO YA KIDATOCHA NNE 2121)
Mwanakwetu akamwambia na baba yake mpanga sare anataka mtoto wake awe mpanga sera unaweza kupeleka posa ukafukuzwa na jamvia.Jamaa akasema
“lakini mwanakwetu unasema kweli ! Lakini mbona yeye kaoa watoto wa watu atakubali tu.” Jamaa alijipa moyo.
Mwanakawetu akamkumbusha jamaa huyu kuwa sheria zetu za Tanzania ni kali wewe tukikutambua kuwa unataka kutuharibia mwanafunzi wetu hatukuachi salama tutakushughuliki huko huko ulipo hata kama upo ughaibuni utarudishwa kujibu tuhuma. Ndugu huyu akasema yeye atakuwa msamilivu hadi binti huyu atakopomaliza shule.
Jamaa akasema mwanakwetu umesema wafanya maamuzi /watengeneza sera wengi ndoto zao ni kwa watoto wao kuwa wasomi wakubwa na hata kufuata nyayo zao, hilo linasaidia mno hata mipango mingi inayopangwa nayo inawalenga mno wasomi lakini linawapa kisogo walio wengi wnaofany avibaya kimasomo ambalo ni kundi kubwa.
“Sasa hivi hakuna mtu yoyote anayezungumza juu ya kuwasaidia kundi la waliopata daraja la nne na sufuri. vikao vyote vya sasa ni juu ya kuwapokea kidato cha tano kidogo na wale wa vyuo vya kati waliopata daraja la II na la III.” Jamaa akasema hilo ni kweli.
“Kwa mfano itangazwe sasa hivi wale waliopata sufuri na daraja IV wote wiki ijayo wakaripoti VETA za kanda wakasome bure stadi mbalimbali za maisha nchi nzima kw kwa mpango maalumu ungeona vurugu yake na asiye ripoti huko serikali imchukulia hatua mhusika, wazazi / mlezi wake. Huo uwe mpango maalumu wa mafunzo ya miezi minane ya dharura kuokoa kundi hilo nchi nzima. Hawa wangehitimu wangeweza kurudi mtaani na kujiajiri na wangejiongeza kipato cha mtu mmoja mmoja ”
Jamaa akawa anasikiliza.
Ndugu huyu akasema kweli watungaji wengi wa sera na wafanya maamuzi mawazo yao mengi wanadhani hata watoto wao watakuwa miongoni wafanya maamuzi hapo baadaye kosa moja kubwa sana na mipango mingi inawekezwa kwa wanafunzi waliofanya vizuri na kuacha kundi kubwa waliofanya vibaya kama ilivyoelezwa hapo awali bila ya wao kufahamu jamii inategemeana kwa mambo mengi mathalani kuoleana na kuzaana.Mazungumzo haya ya simu yaliendelea.
(KIDATO CHA NNE 2018/2019)“Kwa mpanga sera ana mtoto wake wa kiume/kike aliyepata daraja la kwanza na pointi saba, kumbuka huyu anaweza kuoa/kuolewa au kuzaa kwa bahati mbaya kama inavyosemwa au kwa bahati nzuri na kijana/binti ambaye katika haya matokeo ya Baraza la Mitihani amepata sufuri, huyu mpanga sera wa sasa atapata mjukuu. Baba/mama kasoma vizuri baba/mama msingi wake wa elimu haueleweki mjukuu wa mpanga sera anaweza kuharibikiwa kutokana na msingi wa mzazi mmojawapo kuwa mbovu.”
Jamaa hapo akadakia hapo kosa ni la mpanga sera Frank Kidani na madhara yanakwenda kwa mjukuu. Daa wafanya maamuzi / wapanga sera wa sasa lazima wawe makini mno kwa kuwatilia makundi yote ya ngazi za elimu kwa manufaa ya kesho ya vizazi vijavyo
“Mwana Kidonda, Mjukuuu Kovu.” Mwanakwetu alisema.
Simu hiyo mara ilikatika na mwanakwetu hakuwa na muda wa maongezi wa kumpigia muungwana huyo.
0717649257
Post a Comment