Adeladius Makwega-MBAGALA.
MwAnAkWeTu! Inawezekana hii dhana ya mgombea mwenza haieleweki vizuri kwa viongozi wetu, ngoja leo hii msomaji wangu nitoe Darasa la Mgombea MWENZA; mwenza ni mtu jirani yako na anapopata shida lazima ulie naye na anapopata raha ule naye. Huyu ni Mwenzi WAKO, ndiyo maana katika dini ya Kiisilamu mara baada ya Mwanakmke kufiwa na mwenza wake ameweka dhana moja inayoitwa EDA.
Msomaji wangu tambua kuwa MwAnAkWeTU ni Mkristo Mkatoliki huku akikulia katika jamii inayofuata misingi ya dini ya Kiisilamu.Swali mezani je EDA ni nini?
“Hiki ni kipindi anachokaa Mwanamke mara baada ya kufiwa na mwenza wake au mara baada ya kupewa talaka.”
Kulingana na tovuti ya Alhidaaya wanakwenda mbali zaidi katika makala iliyoandikwa na Abd Adillaah wanasema;
“Neno Eda linatokana na neno la Kiarabu IDDAH ikimaanisha mkusanyiko wa idadi ya miezi na hekima yake kubwa huyu anakwenda eda pengine anao ujauzito wa yule mwenza wake wa awali, hivyo basi eda ni kipindi cha uangalizi na baada ya hapo mwanamke husika huwa na ruhusa ya kuolewa na mtu mwingine. ”
Haya ni maelezo ya tovuti ya Alhidaaya , kikubwa msomaji wangu mwanamke hukaa EDA kama kipindi cha mpito akijitafakari kuanza maisha mapya baada ya tukio la talaka au msiba. Kwa hiyo kwa mujibu wa makala haya ya Alhidaaya mwanamke hawezi kuolewa mara baada ya msiba/talaka na/wa namwenza wake, lazima apitie kipindi cha EDA hiki ni kipindi mpito baada ya talaka/msiba.
“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wao wanafanya kazi kwa pamoja na yako matunda yanayoweza kupatikana katika kufanya kazi pamoja, hawa ni wenza, hawa ndugu hapa hakuna mahusiano yale ya kindoa lakini matunda ya kazi yapo.”
Kwa mawazo ya MwAnAkWeTu anatambua kuwa Jamhuri ya Muungano ni Taifa lisilo la dini, lakini dhana hizo muda zinasaidia kutoa muelekeo sahihi wa taifa letu, dhana ya EDA baada ya kifo cha John Pombe Magufuli ilikuwa haikwepeki lakini, lakini lakini ibara ya 37 (5) ua Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inapingana na dhana hiyo.
“… endapo Rais atafariki akiwa madarakani, nafasi hiyo itakuwa wazi, naye Makamu wa Rais ataapishwa kushika nafasi hii, naye Rais husika atamchagua mtu mmoja kushika nafasi ya Makamu wa Rais baada ya mashauriano na chama chake cha siasa anachotokea, kisha jina husika kupigiwa kura na Bungeni kuthibitishwa na asilimia hamsini ya kura zote Bungeni.”
Msomaji wangu Katiba ya Jamhuri ya Muungano haitoa nafasi ya Makamu wa Rais mara baada ya kifo cha Rais kulia msiba wa mwenza wake, haitoi nafasi kama ile ya kukaa EDA baada ya msiba wa Rais, bali Katiba yetu inatoa nafasi ya Makamu wa Rais ambaye awali alikuwa Mgombea Mwenza kukalia kiti. Japokuwa maelezo ya Katiba yanatoa mwongozo huu wapo baadhi ya watu wanaamini kuwa haiwezekani mara tu baada ya msiba wewe uwe na heka heka tele, wewe umefiwa, wewe umefiwa na mwenza wako lazima uwe makini na kila hatua unayopiga maana umma unatambua kuwa unalia msiba na ndiyo maana hekima ya EDA inabaki kusimama.
“Jamani eee mwezangu John Pombe Magufuli amefariki, sasa mie ndiye Rais wenu kama Mwenyenzi Mungu alivyopenda, kwa uhakika kwa mila zetu haiko hivyo Magufuli nimefanya naye kazi kwa karibu kuliko mtu yoyote yule. Sisi kama taifa hatuwezi kulia msiba milele Serikali lazima iendelee na majukumu yake na ndiyo maana nimekula kiapo sasa ndiye Rais wenu.
Miaka hii minne Mungu kanipa inakuwa mithili ya EDA yangu nimalizie vizuri, nawashukuru Watanzania kwa kunipa ushirikiano, mnatakiwa kujipanga upya, CCM tafuteni wenzetu wengine ili waendeleze gurudumu letu.”
Wapo wanaokubaliana na Rais Samia Suluhu Hassan kuendelea kuukalia Urais kama Katiba ilivyo baada ya kifo cha Rais Magufuli lakini siyo tena kugombea mara baada ya 2025 na hii inaipa nguvu dhana ile ya Mungu kapenda na mapenzi yake hayapingiki na Dkt. Samia Suluhu alitakuwa kuwaongoza wana CCM kumuombea kura mgombea Urais wa CCM mwaka wa 2025 kwa sababu mitano tena sawa lakini hadi ikifika 2030, Watanzania Mioyo Yao Itakuwa Imefubaa na Kuchujuka.
“Sasa CCM kinakuwa Chama Cha Mabwenyenye, chama cha wenye nafasi, wanaojipendelea wenyewe na koo zao,wenye rasilimali zao, CCM Hakikuwa Chama cha Kinasaba.”
Kwa sasa wapo wanaoamini kuwa hata ile CCM ya kujivua gamba ya mwaka 2007/2008 ina nafuu maana CCM ya kujivua Gamba ililitambua tatizo na ikalifanyia kazi na hiyo ndiyo pona pona ya Jakaya Kikwete na hadi John Pombe Magufuli anaingia madarakani.
“Ebu tujiulize hata huu mchakato wa kuchuja wagombea ubunge waliotia nia katika majimbo mbalimbali kupitia CCM, Kamati ya Maadili ya CCM inaweza kuwaeleza wana CCM je ilipata wapi taarifa za wagombea wote nchini nzima kuwa mgombea A apite na mgombea B asipite? Je Ilitumia mbinu gani kupata taarifa hizo? Kwa hakika ninavyoona taarifa hizo kuna dalili zote CCM ilitumia taarifa kutoka vyombo vya umma ambavyo vipo chini ya Serikali, vipo chini ya Mawaziri, Vipo chini ya Rais ambaye ndiye mgombea wa nafasi ya Urais.
Je ipo taasisi ambayo inaweza kutoa taarifa vinginevyo dhidi ya Mtia Nia wa Ubunge, hata huyo Mgombea Urais wa CCM Taifa ambaye ni Rais Je ipo taasisi yenye uwezo wa kutoa taarifa vinginevyo dhidi ya rafiki, ndugu, Waziri Anayependwa na Mgombea Urais wa CCM kwa mwaka wa 2025? Taasisi Hiyo Haipo.”
Mwanakwetu anafakari sana na hata anafikia katika kuwatazama wajumbe wawili wa Kamati Kuu ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anaowafahamu ambao ni Salim Abri na Rajabu Abdallah. Kwa uhakika hawa jamaa wawili ni wana CCM wazuri sana ambao Salim Abri ni Mkulima Mfugaji, huku Rajabu Abdallah yeye ni Mkulima. Swali ni moja aina ya wajumbe wa Kamati Kuu na hulka zao wanapokuwa vikaoni zikoje? Wajumbe wote 24 wanafahamika na wengi wao wanaingia kwa vyeo vyao ambao hawawezi kupinga chochote kilichokuwa katika ajenda kwa dalili kinabaki kama kilivyo.
Katika Wajumbe hao wa Kamati Kuu yupo ambaye anaweza kusimamia msimamo wake kwa niaba ya Watanzania maskini? Wana CCM maskini?
“Hoja siyo kuingia vikaoni, kupokea kilichotayarishwa na kujadli kidogo na kuyaacha mambo yaende kama yalivyo.”
Mwanakwetu nimejiuliza swali hili mathalani Mhe. Rajabu Abadallah ambaye ni miongoni mwa wajumbe Kamati Kuu akiwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga, Je tangu tukio la kuuawa kwa marehemu Ali Mohhamed Kibao.

Nije kwa ndugu yangu na rafiki yangu Salim Abri ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Kuu ya Siasa Taifa na amechaguliwa nafasi hiyo kipindi hiki cha Uenyekiti wa Dkt . Samia Suluhu Hassan, je nayeye tujiulize amewahi hata mara moja kwenda kutoa neno la faraja kwa familia za Mdude Nyagali na Shedrack Chaula na kueleza Chama cha Mapinduzi hakiungi mkono haya yaliyofanyika?
Msomaji wangu tambua Salim Abri yeye anatokea Iringa kwa maana yeye ni Mnyalukolo wa Iringa Mjini, huu Mkoa wa Iringa na Mkoa wa Mbeya ni mikoa ndugu. Kisiasa kama tunafanya hivi kasha haya mambo yanafanyiwa kazi inaondoa malalamiko.
MwAnAkWeTu ninaamini kuwa hili halijafanyika na wala halifikiliwi kufanyika, swali ni je wajumbe hawa kwenye vikao vya Kamati Kuu wanajadili nini, je upo ushahidi wa mihutasari na michango yao katika ajenda kama hii?
“Mathalani inatokea shida, alafu wajumbe wote 24 wa Kamati Kuu kila mmoja akaulizwa hilo ajitetea na iwe kwa ushahidi wa maandishi vikaoni, kuna ushahidi? Hata ushahidi mbele ya Mungu.”
Swali ni moja tu wajumbe wote wa Kamati Kuu ya CCM wanawajibu wa kuiombea kura CCM maana nyinyi ni sehemu ya maamuzi ya CCM mpaka sasa, yawe mazuri yawe mabaya.
“Mathalani mnafika Tanga Mjini mnajieleza wee, wananchi wanasema tumewasikia lakini tunatka tumjue alimuwa Ali Mohammed Kibao.Tunajibu nini? Mnajibu nini? Au mnaenda Mbeya Mjini mnaongea wee utekelezaji wa Ilani, kisha wanannchi wanataka wajue alipo Shadrack Chaula na Mdude Nyagali Mnajibu nini/ Mnajibu nini?”
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
MwAnAkWeTu siku ya leo asiseme mengi maneno, lakini lakini CCM lazima ije na mgombea mpya wa nafasi ya Urais.
Mwanakwetu upo?
Je makala haya niyaitaje? Mioyo Iliyofubaa na Kuchujuka? Jamani Tunaombaje Kura? Naongea na Wajumbe Kamati Kuu. Mwanakwetu siku ya leo anachagua Jamani Tunaombaje Kura?
Nakutakia Siku Njema.
0717649257
Post a Comment