NILIVUTIWA NA HUYU BINTI

Adeladius Makwega-Korogwe Tanga.

Mwanakwetu yu wilayani Korogwe Mkoani Tanga katika mafunzo ya Shule Bora, mada kadhaa zinaendelea katika mafunzo haya ya siku tano, hii ikiwa siku ya tatu mafunzoni.Siku hii ilianza kwa ndugu David Harns, huyu Mwingereza alikuja na swali kwa wana mafunzo akiwemo, akiwemo akiwemo Mwanakwetu.

Swali ubaoni lilitaka kila mwanamafunzo kumchagua mtu mmoja ambaye hajazungumza naye tangu kuanza mafunzo haya siku ya Julai 7, 2025. Kwa hakika swali hili lilikuwa gumu mno kwa Mwanakwetu maana katika kundi lote la wanamafunzo hakuwepo hata mtu mmoja ambaye hakuweza kuzungumza naye.

Mwanakwetu akiwa njiapanda kujibu swali la mtoa mada aliamua kumchagua dada mmoja ambaye kwa hakika alikuwa hamfahamu jina lake lakini baadaye alipomshika mkono alibaini kuwa anaitwa Jesca Silaa.

“Nilimvutiwa kando binti huyu na kumuuliza yeye ni nani ana anafanya kazi gani?”

Jesca alijibu kuwa yeye ni mwanasheria, Mwanakwetu akiwa na binti huyu kazi ilikuwa ngumu kuweza kupata cha kujibu kutoka katika swali la muwezeshaji, huku Jesca akisema kuwa lazima uwe na jibu la kujibu kwa mwezashaji vinginevyo utafeli mafunzo.


 

Kweli Mwanakwetu siku hii kweli anakosa cha kujibu mafunzoni? Muda wa zoezi hili ambalo lilitolewa na mwezeshaji David Hans ulikwisha hivyo kila mwanamafnzo alipata nafasi ya kueleza kile alichojifunza kwa mtu mmoja ambaye alikuwa hajaongea naye tangu afike mafunzoni.

Lo salalee! Akilini mwa Jesca Slaa anajua kuwa Mwanakwetu ameshafeli mafunzo. Wanamafunzo walipewa nafasi na kila mmoja kueleza yake na pia ikafika zamu ya Mwanakwetu anaeleza nini mbele ya mkufunzi huyu kutoka Uingereza.

Mwanakwetu alichukua ulingo na kueleza haya,

“Mimi nilimchagua Jesca Slaa, yeye ni mwanasheria. Hivi sasa anaishi huko Dodoma, yeye ni miongoni mwa watoa mada mafunzoni, kwa hakika nimejifunza mengi kwa binti huyu wa Kitanzania, nikiwa naye wakati wa zoezi hili leo nilijiuliza maswali kadhaa akilini mwangu ambayo nlikuwa najijibu huku nikiongea naye kwa dakika tano za zoezi.

Miongoni mwao ni hili je Jesca akihamishiwa mkoa wa Mara je ataweza kuishi? Nilijipa majibu kuwa hilo kwake litakuwa ngumu.

Nilijiuliza suala linguine, je Jesca akija nyumbani kwetu Mbagala ataweza kukamua maziwa wa ng’ombe wa akina Mwanakwetu? Mazungumzoni nilibaini kuwa Jibu lake Jesaca japokuwa pengine anatokea jamii ya wafugaji yeye ni msomi kuamka kila asubuhi kukamua maziwa ya ng’ombe wa Mwanakwetu itakuwa ngumu. Swali langu la mwisho lilikuwa je Jesca kama akiwa katika mji wake, yeye kama mwanasheria je kama kutatokea kutokuelewana suluhu yake itakuwa ni mahakama? Mwanakwetu nilipata jibu jibu la ndiyo maana Jesca ni Mwanasheria.”

Mwanakwetu alimaliza kuwasilisha alichojifunza kwa binti Jesca Slaa na kueleza hili mafunzoni na baadaye Mwanakwetu kuamua kuyaweka haya yote aliyoyasema mafunzono katika makala haya siku ya leo.


 

Mwanakwetu anasema nini?

Kikubwa msomaji wangu ninajaribu tu kueleza namna nilivyoshiriki mafunzo haya ya Shule Bora na namna alvyojifunza kutoka kwa Jesca Slaa ambaye Mwanakwetu alimchagua siku ya leo.


 

Mwanakwetu ana hakika Jesca Slaa yeye ni miongoni mwa wakufunzi na wanaotoa mada katika mafunzo haya, makala haya ni sehemu ya mafunzo ya siku leo hapa Korogwe na  inawezekana Jesca Slaa akaweza kuisi mkoani Mara, inawezekana Jesca Slaa akaweza kukamua maziwa ya ng’ombe wa Mwanakwetu na inawezekana Jesca Slaa akawa mama mzuri hata akawa mama mwenye suluhu kumbwa katika mji wake, inawezekana Jesca Slaa akaweza kufanya kazi vizuri Mkoani Mara kama alivyo Mwanakwetu , inawezekana Jesca Slaa akaweza kukamua maziwa ya ng’ombe nyumbani kila siki inayokwenda kwa Mungu.

Mwanakwetu upo?

Kumbuka,

“Nilivutiwa na Huyu Binti.”

Nakutakia siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257




 

 

 

 

 

 



0/Post a Comment/Comments