Adeladius Makwega-Korogwe TANGA
Hii ilikuwa ni majira ya jioni hivi, makundi ya watu yalikuwa matatu; kundi la kwanza waliingia katika magari yao na kuondoka, kundi la pili walipanda bajaji na boda boda za kukodi na kuondoka na kundi la mwisho lilikuwa la waliotembea kwa miguu kutoka eneo yalipokuwapo makundi yote matatu.
Katika makundi haya matatu Mwanakwetu alikuwepo kundi la tatu waliokuwa wakitembea kwa miguu.
Kwa hakika Mwanakwetu alikuwa na fursa ya kuwaomba kundi la wenye magari akapanda na kuondoka nao au angeweza kupanda bodaboda au bajaji nayeye kuondoka zake, lakini hili halikufanywa na Mwanakwetu, sababu ilikuwa moja tu kundi la watembea kwa miguu, wazee wa TZ NYANYO ndilo kundi la Mwanakwetu tangu anazaliwa, huku akisema moyoni maneno haya,
“Siwezi kujitenga na kundi hili kisa ninamfahamu fulani kwakuwa yeye anagari au kisa ninaposho ya kumlipa mwenye pikipiki, nikajitenga na kundi langu la asili? Hilo , abadani, siwezi kufanya hivyo.”
Aliyekuwa mbele ya kundi la watembea kwa miguu akasema jamani huu upande tuliopo siyo salama, maana magari yatakuwa yanakuja nyuma yetu, tuhamie upande ambapo magari tunayaona, kweli hilo lilifanyika vizuri huku wale wenye magari , na wale waliokodi bajaji na bodaboda wanapita huku wakitusalimia na maneno juu yake,
“Mwanakwetuuuu… Braza Kazimbaya Makwegaaaa, mkubwaaa mbona mbona kaka mbona unatembea kwa miguuu!”
Mwanakwetu aliwapungia kwa mikono miwili huku akijibu kuwa leo, leo nimeamua kutembea tu.
Katika hekima za maisha ukiwaona watu kundi wanatembea kwa miguu, baada ya shughuli fulani tambua kuwa kila mmoja anaufahamu mfuko wake ukoje, hivyo hekima ni kuungana na wanaotembea kwa miguu na siyo busara na siyo hekima kuuliza mbona mnatembea kwa miguu?
Kumbuka msomaji tumevuka upande ambao magari yanakuja tunayaona mbele yetu yanatuvuka na siye tunaenda.
Tukiwa tunatembea ile shoto kulia shoto kulia,kulia kushoto kulia kushoto, mara ikapita gari na picha za wagombea urais wa CCM wa mwaka 2025, jamaa mmoja akasema jamani hivi mmesikia kuwa Aggrey Mwanyri ametia nia Ubunge wa Siha? Jamani mwingine, jamaa mwingine kabisa wa tatu akajibu kuwa Aggrey Mwanri yupo vizuri, CCM taifa wajitahidi jina la huyu mzee walirudishe na wajumbe wa Kilimanjaro kama jina hilo litarudi wawe makini, waache mizengwe, wampe huyu mzee.
Katika mazungumzo haya Mwanakwetu alikuwa kimya sana, hakuweka kuweka neno lolote lile japokuwa alikuwa nayo mengi juu ya jina hili la Aggrey Mwanri.
Jamaa mwingine akasema ngoja niwapeni stori, Aggrey Mwanri nilimuona mtu mwema sana kuna siku moja alikuja katika kanda yetu kama Balozi wa Pamba, kabla ya kufika alinipigia simu na nilipewa jukumu la kumtafutia nyumba ya wageni, nikatafuta nyumba moja ya shilingi 50,000/- nikaweka booking ya chumba, usiku akafika na kuingia katika nyumba hiyo, asubuhi ananipigia simu akisema mwanangu ukija mje kunichukua sehemu nyingine akiiitaja jina. Jamaa huyu akawa anaendelea kusimulia,
“Nikatoka kwangu na dereva hadi hapo tulipoambiwa kumchukua , nikijua labda alikuwa na mazungumzo na jamaa mwingine, kweli siku zote alilala hapo, lakini baadaye nilikuja kugundua kuwa nyumba ile niliyofanya booking ilikuwa na wageni wenngi vijana wengi wageni siku hiyo na hakukuwa na utulivu na milango yake ilikuwa ikitazamana, kwa hiyo vijana waliokuwemo wageni siku hiyo walipokuwa wakimpiga kelele yeye akisali kelele hizo zilimnyima amani, hivyo akaamua kuhamia nyumba nyingine ya wageni tuliyokwenda kumchukua.”
Kumbuka msomaji wangu jamaa hawa waliyo na Mwanakwetu siku hii wanatembea kwa miguu kuelekea upande wa pili wa mji huu.
Jamaa msimuliaji anaendelea, akasema Balozi wa Pamba akafanya ziara yake vizuri. Kumbe katika ziara yake na kulikuwa vijiji vitatu ambavyo hali ya usalama wake ulikuwa unatiliwa shaka, Balozi wa Pamba akafanya ziara hiyo vizuri, kumbe kuna idara moja ilipitiwa na kusahau kupeleka vijana wake ziarani kutoa ulinzi, wakati ziara imekwisha Balozi wa Pamba akawauliza jamani kwanini mmefanya hili? Au mnataka niwashitaki kwa mh Rais? Msimuliaji anasema hali ilikuwa tete, Balozi wa Pamba alitafutwa na kuombwa msamaha.
“Yaani tukiwa katika ziara ile kabla ya kuanza safari Balozi wa Pamba alianza kwa kusali, akishamaliza sala ndipo safari inaanza. Unajua sasa Tanzania inahitaji viongozi wenye hofu ya Mungu.”
Msomaji wangu jamaa hawa wanaotembea kwa miguu akiwamo Mwanakwetu wanatembea huku wakiongea safari iliendelea kisha kila mmoja kuchepuka alipokuwa anakwenda na baadaye Mwanakwetu kukutayarishia makala haya.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Kwa hakika haya ni mawazo ya Watanzania juu ya kiongozi huyu anayeyajenga makala haya siku ya leo Balozi wa Pamba Aggrey Mwanri. Maswali ni mengi, Je yepi ni mawazo ya viongozi wa CCM? Je yepi ni mawazo ya wajumbe kutoka Jimbo la Siha? Na je yepi ni mawazo ya Kamati Kuu ya CCM Taifa?
Kwa uhakika
“Iwe Viongozi wa CCM ngazi yoyote ile, iwe wajumbe wa CCM wa Jimbo la siha , iwe Kamati Kuu ya CCM Taifa, hawa wote hawa haifanyi kazi binafsi, bali bali bali wanapaswa kutambua kuwa wanafanya kazi kwa niaba ya wana CCM wote na kwa niaba ya Tanzania yetu, kwa hiyo ni vizuri kutambua kuwa jamii inahitaji Viongozi wenye hofu ya Mungu kama alivyo Aggrey Mwanri.”
Kwa hakika katika simulizi hii niliumwa sikio kuwa Aggrey Mwanri aliwasamehe jamaa hawa wawili; yule aliyemchagulia nyumba yenye milango inayotazamana na kelele tele kwa vijana usiku ule na pia alisamehewa kiongozi amabye alipitiwa kupeleka vijana wa ulinzi katika vijiji vile vitatu, huyu ni kiongozi wa msamaha.
Mwanakwetu upo?
Je makala haya Niyahitaje? Chagueni Viongozi wenye Hofu ya Mungu, Aggrey Mwanri Kiongozi mwenye msamahaa?Au Ziara ya Balozi wa Pamba? Mwanakwetu anachagua Balozi wa Pamba Kiongozi Mwenye Msamaha.
Nakutakia siku njema.
0717649257
Post a Comment