HUU NDIYO MWALIKO KWETU

Adeladius Makwega-Lushoto TANGA

Siku hii ya Julai 13, 2025 ilianza huku masikio ya Mwanakwetu yakisikia kwa mbali mbali kengele za Kanisa zikilia ambapo Kengele hizo zilitoka katika Kanisa Kuu la Usharika wa Lushoto la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ambalo lililikuwa umbali mchache na makazi ya Mwanakwetu.

Kwa mbali zilisikika sauti za bodaboda na magari moja moja , huku kukiwa na milio ya wadudu ambao wameweka makazi katika uoto wa asili wa Mji huu Mkongwe.

Hali ya hewa ilikuwa ni ya baridi kali ya sentigredi 17 huku upepo ukivuma kwa kasi ya KM 6 kwa saa, nayo baridi kali yote hilo haikuwa na hata tone la manyunyu wala mvua yenyewe.

Mwanakwetu alipoamka tu akiwa katika blangeti lake zito aliamua kusikiliza mahubiri ya Kadinali Luis Antonie Tagle ambaye ni Mkuu wa Proapaganda Fide ya Kanisa Katoliki Ulimwenguni inayojihusisha na Uinjilishaji wa Watu  kwanza Kadinali huyu aliyepo Vatikani alipuuliza mbiu yake ya mgambo kwa maneno haya; Leo ni Jumapili ya 15 ya Mwaka C wa Kanisa. Katika injili ya leo, Yesu anajaribiwa na msomi wa sheria. Akisema Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele? Yesu anajibu kwa kumuuliza, ‘Imeandikwa nini katika torati na kwa jinsi gani?’ Mara ,Msomi wa sheria anatoa muhtasari wa yote yaliyoandikwa Toratini akisema. Kisha anasema nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa nafsi yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote, na jirani yako kama nafsi yako. Yesu hapa akamthibitisha ufahamu wake wa sheria na kumwambia, ‘Fanya hivyo hivyo, nawe utaishi?’ Hata hivyo msomi huyo wa sheria akaibuka na swali jengine. ‘Na jirani yangu ni nani?’ Yesu anamjibu kwa mfano, si kwa ufafanuzi. Akisema Wakiwa njiani kuelekea Yeriko, mwanamume mmoja alishambuliwa na watu wasiojulika, aliibiwa, akapigwa, na kuachwa mahututi akidhania kuwa amekufa. Kasisi mmoja alipita kando akaenda upande mwingine. Mlawi akaja na kufanya vivyo hivyo kama Kasisi. Kisha Msamaria Mwema akapita akafika, akionyesha huruma. Alimwendea mhasiriwa huyu aliyevamiwa na wasiojulikana, akamuhudumia, akamfunga majeraha yake, na kumpeleka kwa matibabu na kisha kwenye nyumba ya wageni, na kumwagiza mlinzi amtunze vizuri.Kwa swali la Bwana Yesu, mwanachuoni aliyepotea anaashiria yule aliyemtendea mwenzake kwa rehema kama jirani wa kweli. Bwana akamwambia afanye vivyo hivyo. Huu ndio mwaliko kwetu. Tenda kama mafundisho ya neno la Mungu.”Haya yalikuwa na maelezo ya muhtasari ya dominika hii kama alivyodokeza Kadinal Tagle. Swali ni je mimi na wewe katika mfano huu wa Injili ya leo ni nani? Je Msamaria?Kasisi au Mlawi?Kwa hakika kila mmoja wetu analo jibu lake moyoni na tunafahamua tunapaswa kuwa kama nani.Mwanakwetu alipomaliza kusikiliza mahubri haya yua Kadinali Tagle alfungasha vifurushi vyake na kuianza safari ndefu ya kutoka Tanga kuelekea Musoma Mkoani Mara ambapo ni umbali wa KM karibu 850.

 
Mwanakwetu Upo? Kumbuka
“Huu ndiyo Mwaliko Kwetu.”
Nakutakia Jumapili Njema.
 
makwadeladius@gmail.com
0717649257
 

 








0/Post a Comment/Comments