BURIANI MOHAMMED MKUFUNZI

 Adeladius Makwega-Musoma MARA.

“Januari 27, 2012 Mwanakwetu alipanda ndege ya Swiss Air Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam kuelekea Amsterdam na baadaye Amsterdam hadi Cologne na kushuka uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Cologne Bonn nchni Ujerumani. Alipokelewa hapo na kijana mmoja wa Mjerumani na kumpakia Mwanakwetu katika gari ndogo aina ya Vokswageni hadi makao makuu ya Shirika la Utangazaji la Ujerumani Bonn ambapo awali makao makuu yalikuwa Cologne, hapa Mwanakwetu alitambulishwa mbele ya Mkuu wa Idhaa hii Bi Andrea Schmidt na Msaidizi wake Mohammed Abdul-rahaman Mkufunzi.

Mwanakwetu awali akiwa anashuka kutoka Swiss Air kuingia katika basi maalumu ili kupanda ndege ndogo alipigwa na baridi kali mno, mzee mmoja kutoka Kongo akasema kaka pole baridi ni kali mno hapa siyo Manzese. Baadaye Mwanakwetu kufika katika Jengo la DW na hali ya hewa ndani ya jengo hili baridi haikusikika maana kulikuwa na vifaa vya kuleta joto.

Mkuu wa Idhaa hii Bi Andrea alitoa koti jipya l rangi ya samawati lenye nembo za Shirika hilo ili kumsaidia Mwanakwetu kupambana na baridi hiyo kali mitaani.

Baada ya kutambulsihwa kwa wafanyakazi wa shirika hili na kutoka kurudi Hoteli ambayo alipangiwa na shirika hili hapo Jijini Bonn. Jioni yake Kijana yule wa Kizungu aliyempokea akamzungusha mjini kununua jinsi kadhaa na masweta ya baridi ambapo katika akiba yake alikuwa 250 tu na baba yake mzazi Mwalimu Francis Makwega alimtumia dola 750 kutoka Dublini Ireland kupitia Wester Union Money Transfer mara baada ya kunulia lini ya simu ya hapo Ujerumani. Kibindoni Mwanakwetu alikuwa dola 1000 za Kimarekani.

Siku iliyofuata Mwanakwetu alifika DW KISWAHILI na kuripoti ofisini na Mohammed Abdul –rahaman Mkufunzi, hapa akongea kwa kifupi na ndugu Mkufunzi kasha akamkabidhi masweta saba ya baridi na hapa hapa akambatiza Makwega jina la Inspekta Makwega, ndugu mkufunzi akisema, ‘Nilipokuwa  JKT tulikuwa na Inspekta mmoja alifahamika kama Inspekta Makwega kwa hiyo na wewe tangu leo nitakuita Inspekta Makwega.’

Kweli masweta haya yalimsaidia

mno Mwanakwetu kupambana na baridi katika kipindi hiki cha mwanzo hapa Ujerumani huku kibindoni akiwa vitu nane yaani masweta saba na jina jipya la Inspekta Makwega.”

Mwanakwetu akiwa pale alipewa majukumu ya kutayarisha makala kadhaa ikiwamo makala ya Jukwaa la Manufaa.

 

(Mwanakwetu akiwa katikati na amevalia sweta moja kati ya masweta saba aliyopewa na ddugu Mkufunzi mwaka wa 2012 Bonn Ujerumani.)

 

Makala haya yalikuwa yanaeleza maoni ya wasikilizajii yaliyotumwa kwa barua ambapo yalisomwa mara baada ya kuandikwa vizuri na kuwa Kipindi cha Jukwaa la Manufaa.

 

Siku moja Mwanakwetu akatayarisha makala haya vizuri, kabala ya kwneda kurekodiwa ilibidi mhariri ayapitie makala haya yaliyaotayarishwa na Adeladius Makwega. Katika makala haya Mwanakwetu alikuwa mkali mno wa maneno makali dhidi ya ushoga wa viongozi wanaoshabikia ushoga wa Ulaya na Marekani, mhariri akasoma makala haya vizuri kasha akamuita Inspekta Makwega huku akisema maneno haya,

“Inspekta nimesoma makala yako vizuri lakini maneno uliyoyotumia kuyajenga makala yako kupinga ushoga ni makali mno maana hapa tupo katika taifa lao, hapa Hatupo Kwetu Tanzania.”

Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?

Usiku wa kuamkia Julai 16, 2025 taarifa za kifo za mtanganzaji wa zamani wa Shirika la Utangazaji wa DW KISWAHILI Mohammed Abdul–rahaman Mkufunzi zimeenea kuwa amefariki dunia Jijini Cologne huko Ujerumani.

Mwanakwetu akiwa katika harakati ya majukumu yake siku hii ndipo alipokea taarifa hii na kuamua kuiweka kando kazi aliyekuwa akiifanya na kuamua kuandika makala haya ya buriani ya ndugu huyu ambaye ni Mjerumani aliyezaliwa Zanzibar, kukulia na kusomea Tanganyika na kulowea Ujerumani akiwa mtangazaji wa shirika hili kwa miaka  karibu 38, alianza kazi na DW KISWAHILI Oktoba 24, 1980.


 

Kwa kuwa Mwanakwetu alipata bahati ya kufanya kazi na ndugu huyu kwa kipindi fulani ameamua na wewe msomaji wake akusimulie visa hivyo viwili vya kweli kutoka kwa Mohammed Abdul-rahaman Mkufunzi akiwa Mkuu wa Idhaaa Msaidizi wa DW KISWAHILI pale Bonn Ujerumani.

(Picha hii kamera ilikuwa na itilafu kwa hiyo tarehe sahihi ilikuwa Februari 18, 2012)

Mwanakwetu Upo? Kumbuka Hatupo Kwetu Tanzania -Buriani Mohammed Abdul –rahaman Mkufunzi.

makwadeladius@gmail.com 0717649257





 



 







 

 

 

 

 

 

0/Post a Comment/Comments