Frank Kashonde –MJINI FM
Julai 18, 2025 Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetoa taarifa yake kwa umma kuwa kimeharisha vikao vyake vya ngazi ya juu vilivyotakiwa kufanyika Julai 18 na 19 2025 kutoka na barua hii Redio ya Mjini FM ya Dar es Saam iliwasiliana na Adeladius Makwega ambaye ni mwalimu, mwanahabri na mchambuzi kutaka kujua je hairisho hilo lina madhara gani kwa wana CCM na jamii ya Watanzania?
Akilijibu swali hili kwa njia ya simu akiwa Musoma , mkoani Mara nchini Tanzania ndugu Makwega ambaye ni mwa CCM kwa muda mrefu amesema,
“Jambo hili lina madhara na faida yake; kwanza faida yake kubwa kwa sasa wana CCM wanatamani kuona michakato wa kuwapata wagombea wao tangu udiwnai , ubunge na urais inafuata taratibu za chama hiki na pili madhara yake ni kuwa kwa watumishi wa umma wana CCM waliochukua fomu za udiwani na ubunge waliotaraijia kujua hatima yao leo katika tatu bora wataendelea kuwa likizo ndefu hadi CCM itakapo fanya maamuzi yake na haijulikani ni lini.”
Ndugu Makwega alisema kuwa kwa muda mrefu CCM imeendelea kunufahika sana na watumishi wa umma wanaogombea nafasi mbalimbali hata ukingazia mawaziri wakuu wa Tanzania wengi wao wasifu waoa walikuwa watumishi wa umma huku akikumbusha kuwa CCM ni chama cha wakulima na wafanyakazi.
Post a Comment