Adeladius Makwega-MBAGALA
Kumbuka msomaji wangu Mwanakwetu alikudokeza kuwa anakita kambI Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kidhahania, hapa Mtumba Jijini Dodoma na alishaipiga hodi ofisini kwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Bi Alice Mtulo.
Kumbuka msomaji wangu pia Mwanakwetu alibisha hodi kwa dada yake huyu mpendwa , akiwa kidhahania katika Ofisi hii ya umma inaonesha wanaofanyakazi ni Watanzania hawa hawa kutoka kariba mbalimbali , hawa ni ndugu zetu wanaozaliwa katika misitu tunayotoka mimi na wewe.Misitu yenye Simba, Chui ,Mamba Kima na Fisi tele. Msiti iliyojawa na wadudu na miba ya kila aina ukitaka kuitembelea misitu hii Vaa Kata Mbuga.
“Kinachofanyika ni mgawanyo wa majukumu tu, wengine wakulima, wengine wavuvi, wangine walimu, wengine wauguzi na wengine ni mawakili.Huu ni mgawanyo wa majukumu tu na ndiyo maana Mwanakwetu ni Mwanahabari.”
Mwanakwetu akiwa kidhahania Ofisi Hii ya Wakili Mkuu wa Serikali alibaini kuwa inatoa huduma tatu; Usuluhishi, Madai na Udhibiti Ubora. Huku wakiwa na Ofisi 17 za mikoa nchi nzima,
“Arusha, Dodoma, Iringa, Kagera, Kilimanjaro, Mara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Ruvuma, Shinyanga, Tabora , Tanga na Kigoma.”
Nakuomba msomaji wangu nikutajie mawakili wafawidhi watatu wa kwetu Morogoro anaitwa Xavier Ndahwa, wa Mkoa wa Mara anaitwa Kitia Turoke na Mwanza anaitwa Subira Mwandambo.
Hawa jamaa wanalo jukumu moja zuri sana,
“Kufanya vikao mbalimbali na wadau juu ya mashauri yasiyo na tija kwa Serikali na kuangalia ni kwa jinsi gani yanaweza kuyamaliza nje ya Mahakama na hivyo kuipunguzia Serikali gharama.”
Hawa ndugu katika vikao hivyo wanaweza kuipunguzia gharama kubwa serikali, Mwanakwetu BI Alice Mtulo akinifungulia Mlango nitamuuliza je kwa mwaka wa 2023/2024 Je mliweza kuipunguzia gharama kiasi gani serikali?
Pia hawa jamaa wanayo kazi nyingine ambayo nimeipenda mno nayo ni hiii,
“Kutambua mashauri mbalimbali ya Madai yasiyo na tija na ambayo yanayoweza kuongeza hasara kwa Serikali na kuyatatua kwa njia za majadiliano na maridhiano nje ya Mahakama.”
Pia na hapa litakuja swali lingine kwa mwaka wa fedha 2022/2023 je hasara ya kiasi GANI iliweza kukwepwa?
Kwa hakika hizi kazi na majukumu ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali nimezipenda mno lakini sijawahi kushuhudia kikao cha Wadau cha Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali siku wakiitisha nitafahamu na kikao hicho nitakujulisha msomaji wangu.
Kumbuka Mwanakwetu anabisha hodi Ofisini kwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali siku ya leo na akimtangulizia maswali mawili Bi Alice Mtulo na jibu yeye mwenyewe Bi Alice Mtulo, Mwanakwetu naweka wazi staki mtu mwingine anijibu maswali hayo.
Mwanakwetu bado yupo katika ofisi hii.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Kwa hakika msomaji wa Mwanakwetu umejifunza majukumu mawili ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali iliyopo hapo Mtumba Jijini Dodoma na hakika umezifahamu ofisi zao 16 na pia umewafahamu mawakili watatu mkumbuke sana huyu wa Mkoa wa Mara Wakili Mfawidhi Kitia Turoke, wengine wanabaki kibindoni.
Unajua ukiwa wakili ukiwa mwanahbari na ukiwa mwalimu lazima uwe hodari wa Kuvaa Kata Mbuga. Hivi Bi Alice Mtulo anaweza kuvaa Kata Mbuga?
Mwanakwetu Upo?
Je makala haya niyaitaje? Bi Alice Mtulo Anaweza Kuvaa Kata Mbuga? Hodi Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali? Au Vaa Kata Mbuga? Mwanakwetu anachagua VAA KATA MBUGA
Nakutakia siku Njema.
0717649257
Post a Comment