Adeladius Makwega-MBAGALA
Mwanakwetu alifika eneo hilo akiwa amechelewa kidogo maana makubaliano alitakiwa kufika hapo saa 11.00 ili waende safari fulani alipokuwa anakwenda Mgeni Rasmi Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete ,Rais Mstaafu wa Wa Awamu ya Nne kando yake milio ya mabundi na paka waliokuwa wakikimbizana ilisikika. Mwanakwetu alipotazama yake ilionesha saa 11.47 ya asubuhi, Mwanakwetu ndiyo anafika, chamno alichelewa, kilichomchelewesha ni ukabwela wake tu, alikuwa anapika chai na kiporo ale ili ainze safari yake vizuri, huku mfukoni hakuwa na pesa ya kula huko huko ugenini aendapo, hivyo basi kunywa chai na kiporo cha wali, maharage na dagaa nyumbani kwake ilikuwa ni hekima na muhimu sana mkongwe Mwanakwetu, alifanya hivyo akikumbuka wajomba zake wagogo wanapokwenda machungaji asubuhi ula ugali na maziwa maana Machungani Hakuna Jiko .
Mwanakwetu alipofika hapo alipokea rundo la lawama mbona kaka umetuamsha mapema na wewe umechelewa, si unajua huu ugeni ni mkubwa unadhani tutaweza kuwahi? Mwanakwetu akawaomba msamaha hawa ndugu kisha kuendelea kuyaweka vizuri mabegi yake. Nje ya eneo hilo walipokaa hawa jamaa kukawa na mjadala mrefu wa vijana fulani ambapo wakati Mwanakwetu anawavuka hawa vijana mjadala ulikatishwa kwa salaam za SHIKAMOO, SHIKAMOO na SHIKAMOO. Mwanakwetu akasema kumbe Nshakuwa Mzee. Mwanakwetu yu ndani ya chumba akipokea lawama kwa kuchelewa, hao vijana nje waliyotoa zile Shikamoo Tatu, SHIKAMOO TELE wakawa wanaongea kwa ukali mkubwa.
“CCM wameshabugi, hata kama watabadilisha jina la mgombea wao wa URAIS hawezi kuvuna kitu. Kubadilisha jina la Mgombea kwa Chama Cha Mapinduzi kwa sasa itakuwa sawa na Mwanamke anayepaka mkorogo usoni, mikononi na miguuni, je ataweza kuupaka huo mkorogo katika makalio(Ashakumu si matusi )?Je ataweza kuupaka mkorogo katika mikunjo ya miguu, je ataweza kuupaka mkorogo katika mikonjo ya mikononi na maeneo mengine yasiyofikika? Watu ni wale wale. Kifo cha Magufuli kilikuwa funzo kubwa kwa CCM na kilitakiwa kuishi kama Mwanamke Mtawa (Baada ya Kifo cha Magufuli CCM Ingeishi Kama Mwanamke Mtawa.) Kwanini Rais Wetu Afariki Madarakani? Je Mungu Anatuambia Nini? Unajua haya mambo CCM hawayaoni, hata wanaolalamika dhidi yao, CCM inaona kama wanawaonea vile ! Kumbe ndiyo ukweli, kuyaona haya inahitaji uwezo wa Mungu.Haya malalamiko CCM ingeyatumia kama fursa lakini wapi? Kama mmesoma Biblia Vizuri Baada ya Kifo cha Abeli,Je Nduguye Hakuchaguliwa Kuwa Mwana Mrithi?”
Mjadala huo unaendelea kwa nje naye Mwanakwetu na jamaa zake walikuwa ndani ya chumba kuogopa baridi kali ya asubuhi, Mwanakwetu anayasikiliza vizuri maneno haya, mara Mwanakwetu na wale jamaa ndani ya chumba wakaingia katika gari kuelekea eneo ambalo Mgeni Rasmi alikuwa huyu huyu Jakaya Mrisho Kikwete kwenda kuifanya kazi hiyo, wale vijana wakabaki nje wakawa wanaendelea na mjadala wao na kilichoendelea hapo Mwanakwetu hakujua.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Kwa wale wanaosoma makala za Mwanakwetu wanatambua kuwa msimamo wa Mwanakwetu ni kuwa nafuu ya CCM ilikuwa ni kuja na jina lingine la mgombea wao wa nafasi ya urais, kidogo hii ilikuwa na nafuu. Lakini lakini lakini hawa vijana waliotoa shikamoo tele walimchanganya mno Mwanakwetu kwa sentensi hii,
“….wameshabugi, hata kama watabadilisha jina la mgombea wa URAIS hawawezi kuvuna kitu. Kubadilisha jina la Mgombea kwa Chama Cha Mapinduzi kwa sasa itakuwa sawa na Mwanamke Anayepaka Mkorogo…je ataweza kuupaka huo mkorogo katika makalio(Ashakumu Si Matusi)? Je ataweza kuupaka mkorogo katika mikunjo ya miguuu , je ataweza kuupaka mkorogo katika mikunjo mikononi na maeneo mengine yasiyofikika? Kifo cha Magufuli kilikuwa funzo kubwa kwa CCM na kilitakiwa kuishi kama Mwanamke mtawa (Baada ya Kifo cha Magufuli CCM Ingeishi Kama Mwanamke Mtawa.) Kwanini Rais Wetu Afariki Madarakani? Je Mungu Anatuambia Nini? Unajua haya mambo CCM hawayaoni, hata wanaolalamika CCM inaona kama wanawaonea vile, kumbe ndiyo ukweli wenyewe, kuyaona haya inahitaji uwezo wa Mungu. Kama umesoma Biblia Vizuri Baada ya Kifo cha Abeli Nduguye Aliyeishi nae Hakuchaguliwa Kuwa Mwana Mrithi…”
Maneno haya yalikuwa sindano ya Kristapeni kwa Mwanakwetu, huku alikuwa akiyatafakari tangu siku hiyo hadi leo hii, alipoyakumbuka na kuyaweka katika makala haya. Mwanakwetu anatoa ushauri mmoja tu kwa CCM Taifa na hasa Kamati Kuu. Kwanza kwanza kwanza kwa msomaji wa Mwanakwetu ambaye hafahamu Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ni ni nini? Hii ni sawa na zile Kamati za Siasa tangu ngazi ya Chini ya CCM hadi Mikoa kwa hiyo hii Kamati ya Siasa ya CCM taifa inaitwa Kamati Kuu. Ukitazama muundo wa Wajumbe na wanavyopatikana kwa Ujumla wake wajumbe karibu wote ni wale wale waliopewa majukumu na CCM katika kazi mbalimbali, hawa wajumbe wanaweza kufanya chochote tofauti na kilichofanywa na serikali? Ni vigumu maana watu ni wale wale. Kwa hiyo hata Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na pia Mkutanoa Mkuu wa CCM Taifa ni vigumu na hawawezi kupata nafasi ya kulijadili jambo tofauti na kile kinachotakiwa na Kamati ya Siasa ya CCM Taifa yaani Kamati Kuu.
Mwanakwetu anaamini hawawezi kujishauri wenyewe vinginevyo na hawawezi kuyaona makosa yao wenyewe lakini msomaji wnagu unaona vijana wadogo sana hata elimu hawana lakini wanajenga hoja vizuri sana. Kwa ujumla wake msomaji wangu ni vigumu Kamati Kuu ya CCM Taifa ikajisonda kidole yenyewe, CCM ilitakuwa kubalisha muundo wa upatikanaji wa Wajumbe wa Kamati Kuu ili vikao vya chama viwe vya moto na nje ya CCM itakuwa salama,maana moto wa ndani una nafuu lakini moto wan je unakuwa mkubwa vinginevyo ni kujichimbia kaburi yenyewe.
Katika haya yote ndipo Mwanakwetu anaamini hata hili fupa la watu wasiojulikna na Mgogoro na Askofu Dkt Josephart Gwajima unaibuka, kama Kamati Kuu ingekuwa na watu tafauti na siyo wenye majukumu katika nafasi za dola Kama akina Dkt Tulia hawawezi kushuari tofauti maana jamii inaona wao ndiyo tatizo. Haya yasingekuwepo Chama hiki kilikuwa na uwezo wa kuiagiza Serikali na lingefanyiwa kazi mara moja na Suala la Watu Wasiojulikana na wangekoma harakati zao. Mashaka ya wananchi ni sahihi je Tanzania itaendelea kuwa na Watu Wasiojulikana miaka mitano ijayo?
Maana uhai wa binadamu ni zaidi ya miradi yoyote ile maana mradi unaweza kubomolewa na kujengwa lakini aliyeuwawa anaweza kurudishwa? Na ni haki ya Wananchi kuhoji hilo na haki ya Wana CCM kuhoji hilo kw aviongozi wao. Je CCM inajibu nini katika Mikutano ya hadhara kama CCM itataja Miradi Mikubwa iliyofanya huku wananchi watanyanyua juu picha hadharani picha za Watu walipotea, kuumizwa kudhalilishwa au kuuwawa na watu wasiojulikana tangu mwaka wa 2015 hadi 2025? Kwa hakika Wagogo wanasema Huu ni Mlimo, Kwa hakika hii ni Kazi Nzito siyo katika kushinda uchaguzi tu bali hata kuliongoza taifa hili kwa miaka mitano ijayo.
Mwanakwetu upo?
Je makala haya niyaitaje? Kumbe Nishakuwa Mzee? Baada ya Kifo Cha Magufuli CCM Ilipaswa Kuishi Kama Mtawa?Baada ya Kifo Cha Abeli Nduguye Hakuirithi Nchi?Huu ni Mlimo? Shikamoo Tatu? Sawa na Mwanamke Mpaka Mkorogo? Mwanakwetu anakupa nafasi msomaji wake uchague mwenyewe kichwa kimoja kati ya hivyo lakini wale vijana walisema Sawa na Mwanamke Mpaka Mkorogo
Nakutakia siku Njema.
0717649257
Post a Comment