HABARI ZENU WAZEE

 

Adeladius Makwega-MBAGALA.

Ilikuwa ni majira ya asubuhi, baada ya misa ya asubuhi ya Disemba mwaka 1988, Mwanakwetu na rafiki yake anayefahamika kama Prosper tukamfuata Padri Wolfram.

“Father sisi hatuna fedha, tupe kazi, tupate pesa, Father Wolfarm akacheka akasema nyie watoto wa Darisalaam pesa ya nini? Nikajibu tunataka tukanunue jinzi za Sikukuu ya Noeli Tandika, Father akacheka tena .”

Tukiwa katika mazungumzo haya akapita Buruda mmoja Mchaga akiwa na BURUDA mwenzake anaitwa Buruda Linuma, huyu BURUDA Mchaga akatusalimia kwa matamshi ya KICHAGA

“Habari Zenu Wazee?”

Tukajibu nzuri huku tunacheka. Father Wolfram akauliza mbona mnacheka?

Mimi nikajibu kwa sauti ya chini,

“Huyu BURUDA MCHAGA KUKAAA KOOOTE DARESALAMA KISWAHILI HAJUI !”

Padri Wolfram akasema huyu anajua KISWAHILI ila matamshi yake ndiyo USWIZI USWIZI kama yangu, kisha Padri akawaambia hawa MABURUDA hawa vijana wanataka kazi ili wapate pesa wakanunue jinsi Tandika. Ati BURUDA LINUMA  kumbe Tandika zinauzwa sana Kafa Ulaya Mazishi Afrika ? Buruda MCHAGA akajibu ndiyo.

Father Wolfram akasema hawa vijana wangu siku hizi wamekuwa Watu wa Mshahara yule BURUDA MCHAGA ambaye alikuwa anapenda kutusalimia kwa toni ya Kichaga Habari Zenu Wazeee akaondoka zake na kutuachi akina Mwanakwetu na Prosper na baadaye alikuja jamaa mmoja alikuwa anaitwa Deus mpiga kinanda maarufu sana tukawa tunapatana kazi ya kulima eneo ambalo lilikuwa na mananasi mengi japokuwa sasa eneo hilo ambalo lipo Kituo cha Kiroho Mbagala sasa limejengwa na makazi wa Mapadri.

Makubaliano ya kazi hiyo kulima ngwe hiyo malipo yalikuwa shilingi 3000 /=kwa watu wawili kila mmoja apate shilingi 1500/= mabpo jinsi moja iliuzwa kati ya 700-900 Tandika Sokoni. Tukaifanya kazi hiyo vizuri na wakati kazi hiyo ikiwa inaendelea akapita Mzungu Mmoja Muitaliano anaitwa NANDO RIVOLTA akapiga picha hiyo, hapo hapo akaomba sanduku la barua kwa PROSPER hakuwa nalo, Mwanakwetu akampa huyu mzungu kupita Sanduku la Posta la Shule ya Msingi BUNGE Dar es Salaam Tanzania na Mzungu akaondika katika shajala yake vizuri na kuondoka.

 


Tukaifanya kazi hiyo vizuri na kisha tukachoma majani Mpishi wa Padri Mzee Makota akatupatia chakula cha mchana tukala na kumalizia kuyachoma majani tulipomaliza Padri Wolfram akatulipa Elfu tatu yetu kisha akafungua Koontena moja kubwa na kutupatia jinsi mbili mbli kila mmoja na fulana mbili mbili rangi nyeupe zilizokuwa na maneno SHULE YA SEKONDARI YA MTAKATIFU ANTONY WA PADUA MBAGALA.

Neno lile kuwa sisi ni watu mshahara lilinikera, wakati Padri anafunga Koontena nikauliza kwanini Padri sisi umetuita watu wa mshahara? Kwani wewe Padri siyo mtu wa mshahara?

Padri Wolfram akasema Adeladius bado unakumbuka?Nikajibu ndiyo, Kwani Padri wewe siyo mtu wa mshahara? Padri akacheka huku anakooa ,akawa anajibu;

“Mimi siyo mtu wa mshahara, mimi ni mtu wa posho tu ili niweze kuishi nisife kwa njaa ningekuwa mtu wa mdhahara ningebaki kwetu USWIZI.”

Hapo hapo Mwanakwetu Prosper n Deus tukanawa vizuri na Kisha kurudi zetu nyumbani na safari ya Tandika kununua suruali za jinsi kafa Ulaya Mazishi Afrika ikafa.

Yule mzungu alipokwenda Ulaya alikaa kama Mwaka Mmoja na miezi kadhaa kisha baadaye akatuma picha hiyo na cheki ya Dola Kumi za Kimarekani kupitia anuani ile niliyompa.


 

Mwanakwetu siku ya leo anasema nini?

Katika simulizi hii majina mengi yaliyotajwa mathalani  Padri Wolfram Nando Rivolta , Deusi na hta huyu Prosper sifahamu alipo kwa sasa Prosper maana alikuwa Askari wa Jeshi la Polisi Tanzania. Kwa hakika Padri Wolfram, Deusi na Nando Rovolta ni Marehemu kwa sasa, jamani kikubwa hapa Duniani tunapita, tukae na watu vizuri, ukiwa mtu wa posho au hata mshahara kaa na watu vizuri. Hatari kubwa ipo kwa sisi watu wa mishahara haya ni mapito tu , watu wa mishahara sasa wengine wanakuwa watu wasiojulikana wakitaka vyeo na pesa teletele, haya mapito tu, kesho siyo mbali utamsimulia Mwanakwetu nayeye alikuwepo, kama ninavyowasimulia hawa ndugu zangu waliofariki. Watu wa mishahara hadi mnatoa roho za watu!? Ndugu yangu hapa unakaa kipindi kifupi mno, achana na hiyo michezo haina maana yoyote.


 

Siku ya leo msomaji wangu niliona nikusimulia hilo pengine unaweza kuuokota busara katika haya

Mwanakwetu upo ?

Je makala haya niyahitaje? Mtu wa Posho, Mtu wa Mshahara au Habari Zenu Wazee? Mwanakwetu anachagua Habari Zenu Wazee na hili liwafikie watu wasiojulikana.

Nakutakia Siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257









 

0/Post a Comment/Comments