CCM INAHITAJI INTELIJENSIA KUBWA YA KICHAMA ILI KIBAKI SALAMA-KADA WA CCM

 


 


Adeladius Makwega-Rorya & Tarime MARA

 

Aprili 25, 2025 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amefanya mikutano mikumbwa miwili Wilayani Tarime na Wilayani Rorya Mkoani Mara, huku mikutano hiyo ikihudhuliwa na Waziri Mdogo wa Katiba na Sheria mhe. wa Jumanne Sagini (Mbunge wa Butiama) maarufu kama Mbunge wa Katikati huku huku Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Alfred Mtambi akimuongoza mgeni wake hatua kwa hatua sambasamba na Viongozi wa CCM Mkoa wa Mara.

Kwa tathimini ya Mwanakwetu mikutano hii miwili imetia fola ya mikutano yote ya ndani ya CCM aliyofanya Katibu Mkuu huyu wa CCM ambaye sasa ndiye Mgombea Mwenza wa nafasi ya Urais kupitia chama hiki akikokotana Dkt . Samia Suluhu Hassan.


 

Katika Mkutano hii miwili Balozi Dkt. Nchimbi amefanya mambo makubwa mawili kwanza kupiga marufuku michezo ya siasa chafu na wana CCM kuacha matumizi ya maneno makali dhidi ya upinzani huku la pili ameongea moja kwa moja na waziri anayeshugulika Barabara wa Tanzania mh. Abdallah ulega kujibu hoja za wananchi wa Rorya.

Wakati haya yakifanyika, kwake Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Mtambi alitoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Mara kushiriki zoezi la maboresho ya daftari la wapiga kura , zoezi hili linatarajiwa kuanza mkoani Mara mapema Mei 1 na kuhimishwa Mei 7, 2025.

Kwa tathimini ya Mwanakwetu mikutano hii miwili ndani ya siku moja imeonesha ukomavu mkubwa wa kisiasa wa Dkt Emmanuel Nchimbi majukwaani.

Mwanakwetu alibaini kuwa siasa za Rorya na Tarime ni ngumu na katika kujifunza hili Mwanakwetu alikutana na kuzungumza na wana CCM kadhaa na Mwana CCM mmoja alitoa maelezo haya,

“Shida ya hili eneo letu halihitaji Viongozi Timamu, linahitaji viongozi waliyo kama vichaa. Changamoto kubwa ya Rorya na Tarime na hata Serengeti unadhania ni CHADEMA? Unadhani ni upinzani? Shida ni rasilimali zetu zilizolala ardhini , Ziwani na Mbugani, jambo hili likikaa sawa hauwezi kuiona CHADENA kabisa wala upinzani.

Kwa haya ya rasilimali wananchi wanaamua kumpa Uongozi hata kama mtu anaonekana na wengine ni mwendawazimu.”

Jamaa huyu alitoa mfano huu,

“Hapa tuna mpaka wa Sirari, kuna upande wetu na upande wa taifa lingine, shida ni bei ya bidhaa upande wetu bei za bidhaa zipo juu.’Mfano mfuko wa saruji hapa nyumba 20,000/=kule bei 13,000/= hivi nani atakubali kununua upande wa kwetu? Hii linaleta ugomvi mkubwa na hata taasisi zinazosimamia mambo haya, haya mambo yarekebishwe.”

Mwanakwetu upo? Kwa leo inatosha sana.

 


Kumbuka,

“CCM INAHITAJI INTELIJENSIA KUBWA YA KICHAMA ILI KIBAKI SALAMA.”

Nakutakia siku njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257

NB Kuyaelewa makala haya zaidi sikiliza sauti inayoambatana na makala haya au Tembelea MwAnAkWeTu Tube akaunti

































 

0/Post a Comment/Comments