WASIRA KAMA RABIA BIN MALIK



Adeladius Makwega Musoma MARA.

“Habari za asubuhi Kaka, Msiba wanazika saa nane mchana, hapo Makaburi ya Mwisenge, hawasafirishi tena.”

Jumatatu Februari 10, 2025 Mwanakwetu akiwa Mjini Musoma, siku hii ilianza kwa kupokea ujumbe huo. Mwanakwetu aliujibu ujumbe huo lakini baadaye alibaini kuwa ujumbe huo haukwenda kwani simu ya Mwanakwetu haikuwa na pesa.

 Mwanakwetu alitoka pahala anapoishi na kuelekea kazini huku anapoishi kukiwa na msiba, ambapo miongoni mwa majirani yake mmoja, mwenyezi Mungu kamchukua. Mwanakwetu alifanya kazi vizuri, kisha huku akilini mwake akisema kuwa leo haitafika saa saba nitawahi kurudi nyumbani ili niweze kushiriki maziko ya huyu jirani. Majira ya saa sita kamili Mwanakwetu anatoka kuelekea kwake, njiani akakutana na mama mmoja ana mtoto mdogo anaumwa, mikononi mama huyu ana barua kutoka kwa Katibu Tawala ya Wilaya Musoma anatafuta shilingi 500,000/- ili mtoto wake akafanyiwe upasuaji. Huyu Mama aliponiomba pesa nikampa nilichonacho huku Mwanakwetu akiwa ni mchangiaji wa saba wanane

“Mwanakwetu akamuomba kadi ya nida huyu mama, namba ya Mtendaji na Mwenyekiti wa Mtaa na Diwani na jina la Mbunge, kwa bahati mbaya mama huyu alikuwa hafahamu vyote. Mwanakwetu akamwambia huyu mama, njoo nazo hizo taarifa hasa hasa namba ya mwenyekiti wa Kijiji, hivi zingine nitazipata maana Mbunge wa jimbo lako ni Jumanne Sajini nitampigia simu nna hakika katika shilingi 500,000/- yeye atachangia kiasi fulani, Njoo kesho na Mwanakwetu kumkabidhi mama huyu kwa walinzi ili akija kesho Februari 11, 2025 asipate tabu.”

NIkiwa nataka kutoka getini nikapigiwa simu na  Bi Hadija Kisubi huyu ni Afisa Utamadani Mwandamizi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, hapo nikaongea pia na Bi Amne Kassian ambaye nayeye Afisa Utamaduni Mwandamizi wa  wizara hiyo hiyo. Hawa ni dada wa Mwanakwetu. Baada ya simu hiyo kukata Mwanakwetu katika bodaboda hadi nyumba kwake kushiriki maziko ya jirani yake. Alipofika hapo alikaa kama saa moja unusu hivi maiti ikafika katika Hiace na kushushwa ikiwa katika jeneza, likabebwa jeneza hilo na kuelekea ndani ya nyumbani kwa marehemu ile kufika mlangoni dada mmoja mtani wa marehemu kutoka Kabila la Washeta akawa akawa mkali mno akasema hapa maiti haingii ndani, mama huyu kuhakikisha maiti haiingii ndani akaenda kando ya nyumba akachukua mchanga na majani akashika jeneza, hiki kikiwa kitendo kama cha ulozi hivi na kweli alipofanya hivyo jamaa waliobeba jeneza wakiwa jamaa wenye nguvu wakarudi nyuma na kuwa kama wamepigwa ganzi kusubiri maamuzi yafanyike. Kweli wakafika wazee wakaongea na mtani huyu na baadaye mtani akapewa chake akafunga katika pindo la khanga huku akipiga vigegele vya shangwe , kisha jeneza kuingizwa ndani ya nyumba. Kweli maiti haikuka sana baadaye maiti ikatolewa katika jeneza za kuzibwa kote na kuingizwa katika jeneza la kubebea mwili kwa Waisilamu tayari kwa Salat Maiti. Kabla ya Salat Maiti ilionekan aliyefariki alikuwa mtu mzima.


 

Shekhe Omari  Amani Bini Kapama ambaye aliyekuwa anaongoza ibada hiyo akasema.

“Sasa ni nafasi kwa wale wanaomdai marehemu au wale wanaodaiwa wajitokeze maana kama marehemu kafa kisha anadaiwa hili ni jambo baya roho yake inakuwa inaning’inia tu huku haipo na kule haipo, kudaiwa kubaya hata kwetu sisi ambao tupo hai, hivyo kwa usalama wetu kama wewe ulikuwa unakaa katika nyumba ya marehemu unadaiwa kodi nakuomba uione familia ipo kupkea na kulipa madeni hayo.”

Hakukuwa na mtu aliyejitokeza kudai wa kudaiwa , mwili ulisaliwa na kubebwa kuelekea makaburini. Wakati tunakwenda makaburini jeneza mbele likiwa limebebwa na dazeni moja ya watu mkono wa shoto nusu dazeni na mkono kulia nusu dazeni.

“La ilaha illallah Muhammadur Rasulullah, La ilaha illallah, La ilaha illallah Muhammadur Rasulullah.”

Mwanakwetu akitambua kuwa maana ya sentensi  La ilaha illallah Muhammadur Rasulullah ni Hakuna mungu bali Allah na Mohhamed ni Mjumbe wake Tulipofika Makaburni watu watano walitajwa majina yao, kisha wakaingia kaburini, mwili ukaingizwa kaburini huku shuka imefunikwa na watu tiliyo makaburini hatuoni kinachoendelea, kisha ukaingizwa ubao alafu majani, huku shuka juu ya kaburi iliyoziba ikipepea pepea kuingiza hewa waliomo kaburini. Hapo hapo Ustadh Kapama akaingia ulingoni na kuongoza utenzi wa maziko huku Ustadh Kapama akiupa uhai mkubwa huu utenzi kwa kuimba beti nne ambapo mara nyingi katika misiba utenzi huu huwa unaimbwa kiitikio bila beti.

 “La ilaha illallah, La ilaha illallah, La ilaha illallah Muhammadur Rasulullah, La ilaha illallah, La ilaha illallah, La ilaha illallah Muhammadur Rasulullah, La ilaha illallah, La ilaha illallah, La ilaha illallah Muhammadur Rasulullah, La ilaha illallah, La ilaha illallah, La ilaha illallah Muhammadur Rasulullah. La ilaha illallah, La ilaha illallah, La ilaha illallah Muhammadur Rasulullah.‘Tuliletwa duniani, hapa sipa masikani , kitu duni, duniani thamani kitolewa.’

La ilaha illallah, La ilaha illallah, La ilaha illallah Muhammadur Rasulullah, La ilaha illallah, La ilaha illallah, La ilaha illallah Muhammadur Rasulullah, La ilaha illallah, La ilaha illallah, La ilaha illallah Muhammadur Rasulullah, La ilaha illallah, La ilaha illallah, La ilaha illallah Muhammadur Rasulullah.‘Dunia hii mapito, hata kama ina vito, hakuna njia mkato ,mauti tutapitia.’

La ilaha illallah, La ilaha illallah, La ilaha illallah Muhammadur Rasulullah, La ilaha illallah, La ilaha illallah, La ilaha illallah Muhammadur Rasulullah, La ilaha illallah, La ilaha illallah, La ilaha illallah Muhammadur Rasulullah, La ilaha illallah, La ilaha illallah, La ilaha illallah Muhammadur Rasulullah, La ilaha illallah, La ilaha illallah Muhammadur Rasulullah.‘Wangapi walikuwapo na leo hawapo kwa mola wamerejea mola wetu subahana.’

La ilaha illallah, La ilaha illallah, La ilaha illallah Muhammadur Rasulullah, La ilaha illallah, La ilaha illallah, La ilaha illallah Muhammadur Rasulullah, La ilaha illallah, La ilaha illallah, La ilaha illallah Muhammadur Rasulullah, La ilaha illallah, La ilaha illallah, La ilaha illallah Muhammadur Rasulullah, La ilaha illallah, La ilaha illallah Muhammadur Rasulullah.‘Wako wapi Matajiri, waliokuwa na kiburi ,nyumba zao makaburim kwa mola wamerejea.’

La ilaha illallah, La ilaha illallah, La ilaha illallah Muhammadur Rasulullah, La ilaha illallah, La ilaha illallah, La ilaha illallah Muhammadur Rasulullah, La ilaha illallah, La ilaha illallah, La ilaha illallah Muhammadur Rasulullah, La ilaha illallah, La ilaha illallah, La ilaha illallah Muhammadur Rasulullah.‘Wako wapi ndugu zetu, na pia wazazi wetu, kwa mola wamerejea, mola wale subahana.’

La ilaha illallah, La ilaha illallah, La ilaha illallah Muhammadur Rasulullah, La ilaha illallah, La ilaha illallah, La ilaha illallah Muhammadur Rasulullah, La ilaha illallah, La ilaha illallah, La ilaha illallah Muhammadur Rasulullah, La ilaha illallah, La ilaha illallah, La ilaha illallah Muhammadur Rasulullah.

La ilaha illallah, La ilaha illallah, La ilaha illallah Muhammadur Rasulullah, La ilaha illallah, La ilaha illallah, La ilaha illallah Muhammadur Rasulullah, La ilaha illallah, La ilaha illallah, La ilaha illallah Muhammadur Rasulullah, La ilaha illallah, La ilaha illallah, La ilaha illallah Muhammadur Rasulullah.”

Alafu waombolezaji kuufukia mwili kaburini. Zoezi hili lilifanyika vizuri kabisa na Ustadhi Kapama akielekeza umma huu kuwa mlipo hapa mnajua maana ya kuzika?

“Kuzika kuna mambo mawili, kwanza mwili tunaufukia kaburini vizuri ili usiharibiwe na wanyama huku nje na pia sie tusipatwe na harufu na madhara wakati mwili unaharibika.”

Kisha likasomwa dua na ustadh mmoja ambaye alikuwa amechuchumaa kando ya kaburi hili alafu Ustadh Kapama akarudi tena na mawaidha ya mwisho kaburini,

“Nitasema maneno machache tu, ingekuwa dunia watu waliopendwa hawafariki basi Mtume Mohammed asingalikufa, wengine hapo hawamjui Mtume Mohammed basi kama ingekuwa watu waliopendwa, wenye kutumiliki sisi na dola kama Mwalimu Nyerere wasingalikufa vivyo hivyo kwa Rais Mkapa na Rais Magufuli, lakini leo wapo wapo, wapo wapi?

Nimetumia mfano wa Nyerere, Mkapa na Magufuli maana hawa ni watu wetu, tunawafahamu, leo hawapo. Huyu mzee tuliyemzika alikuwa mpole sana , hakuwa mtu korofi korofi, basi mwenyeezi Mungu angembakiza lakini hilo haliwezekani. Hakuna atakayebaki, tusidanganyane sote tutakufa haku janjajanja na ndiyo maana huyu mshairi, anasema  ‘Tumeletwa duniani, hapa si masikani, kitu kikiitwa duni, thamani kimetolewa’ Duniani kitu duni thamani imeondolewa  mshairi huyu anaongeza pia .‘Wangapi walikuwepo, na leo hii hawapo, hakuna njia mkato mauti tutaingia.’

Ndugu zangu leo ninasema maneno machache tu sasa Nije katika shukurani ya familia, wana familia wameniuma sikio kuwa, ‘Mtu asiyemshukuru mwanadamu mwezake hawezi kumshukuru Mungu maana Mungu haonekani.’ Familia hii haina cha kulipa kwenu nyoote mliokuja kuzika hata wale ambao hawakuweza kufika. Ninaposema Mungu atalipa, wengine wanachukia ohh kila mtu anakufa na chake, malipo hapa hapa duniani. Hata kama utalipwa 200 utapewa utatumia kesho 200 imeisha malipo bora kwa Mungu. Familia inawaomba turudi nyumbani, wameandaa sadaka, mkiiacha sadaka hiyo nani atakula? Tukale na kila anayekula asibakize punje hata moja katika sahani. Chakula ni cha marehemu lakini kula tunakula sisi, tumalize chakula kuonesha mapenzi kwa huyu marehemu wetu.

Wakati tunazika nilisika jamaa wanasema huu udongo usiache ni wake, ni kweli udongo ni wake kama huu wali tunaokwenda kula na ndiyo maana tusibakize punje hata moja. Duniani kuna udongo wa aina mbili wenye wenyewe kwanza udongo wa kaburi na pili Udongo wa Madini. Udongo wa madini haubaki na udongo wa kaburi haubaki na mimi naongeza twendeni tukale na wali marehemu haubaki.

Rabia Bin Maliki alikwenda kwa Mtume Mohhamed , huyu Rabia alikuwa Swahaba wa Mtume alikuwa kapatwa na msiba-Ninaposema Swahaba na mtu aliyeishi jirani na kumuona mtu fulani. Mathalani Steven Wasira aliishi jirani na Julius Nyerere Wasira ni Swahaba wa Nyerere, aliishi naye jicho kwa jicho. Rabia Bini Maliki kafiwa akamueleza Mtume nimefiwa sasa napaswa kufanya nini?

Mtume akasema ukifiwa fanya mambo matano; muombee dua marehemu wako, muombee msamaha marehemu wako, usivunje udugu alioacha marehemu wako…”

Ustadhi Kapama hakumaliza mambo mawili yaliyosalia. kisha waombolezaji wote kurudi nyumbani kwa marehemu. Tulipofika nyumba kwa marehemu tulinawishwa mikono na kila mmoja kupewa wali tele, maharage na nyama mnofu mkubwa.Mwanakwetu alianza kula kidogo kidogo, akajitahidi kukamilisha nia ya Ustadh Kapama hakuna kuacha punje, Mwanakwetu chakula hiki hakukimaliza hivyo alibeba ili akile jioni nyumbani kwake na kufanya hivyo ilikuwa ni kukamilisha agizo la kiongozi huyu wa dini. Mwanakwetu akafika kwake na kuyatayarisha makala haya huku akiwa na kiu ya kujua Rabia Bin Maliki kama aliambiwa mambo matano je mambo mengine mawili ni yepi?


Mtani baada ya kupewa pesa msibani.

 

Mwankwetu anasema nini siku ya leo?

Mwanakwetu baada ya msiba huo akiwa nyumbani kwake akawa anatafakari mahusiano baina ya Mtume Mohhamed SAW na Rabia Bini Malik yanafanana mia kwa mia na mahusiano baina Julius Nyerere na Steven Wassira?

Mwanakwetu alibaini haya,

Rabi'ah bin Malik alikuwa swahaba wa Mtume Muhammad, Akamwomba Mtume awe swahaba wake peponi, na Mtume akamwambia asali zaidi. Hadithi zinanadi kuwa Rabi'ah alikuwa na shauku ya kumtumikia Mtume na alikuwa akilala karibu na mlango wa mbele wa nyumba yake ili aweze kujibu haraka atakapoitwa. Mtume alipomwita Rabi'ah, Rabi'ah alijibu, ‘Labaik Ya Rasuol Allah wa Sa'daik’. Mtume alimuuliza Rabi'ah anachotaka, na Rabi'ah akaomba kuwa swahaba wa Mtume Peponi. Mtume alimwambia Rabi'ah asali zaidi akiomuombea.Mtume alimpangia Rabi'ah kuoa katika familia nzuri na akampa ardhi.”

Mtu ambaye anaomba awe swahaba wako peponi analla mbele ya mlango wa nyumba yako ni mtu wa karibu mno na walikuwa jirani sana sasa haya ta Julius Nyerere na Steve Wasira Mwanakwetu anayaweka kiporo kwa kuwa makala haya ni ya dini.

 

Makala haya yametayarishwa na Mwanakwetu kwa heshima ya jirani yake aliyefariki na kuzikwa hapa Musoma mkoani Mara.

Kumbuka,

“ Ati Steven Wasira Kama Rabia Bin Malik .”

Nakutakia siku njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257















 

 

 

0/Post a Comment/Comments