Adeladius Makwega-Serengeti MARA
Kiranja wa Propaganda Fide ya Kanisa Katoliki Inayojihusisha na Uinjilishaji wa Watu Ulimwenguni, Kadinali Luis Antonie Tagle amesema kuwa sikukuu ya ubatizo wa Bwana ni Epifani nyingine na tukio la kuangaza, maana nafsi tatu za utatu Mtakatifu zinajidhihirisha.
Haya yameswemwa na Kadinali Tagle Januari 12, 2025 katika Kipindi chake cha Words Expose kinachotoa masomo na mahubiri ya kila Jumapili /dominika.
“Tunasherehekea Sikukuu ya Ubatizo wa Bwana. na katika injili ya leo tunasikia kwa mara nyingine habari ya ubatizo wa Yesu katika mto Yordani.
Katika masimulizi ya Mtakatifu Luka, Yohana Mbatizaji anafafanua kwa wasikilizaji na wafuasi wake kwamba yeye si Kristo, kwamba wakati akiwabatiza kwa maji, atakuja mwenye nguvu zaidi kuliko yeye, ambaye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
Yesu ni miongoni mwa watu wanaopokea ubatizo wa maji wa Yohana na kulingana na Mtakatifu Luka, wakati Yesu anaomba baada ya ubatizo wake, mbingu zilifunguka na Roho Mtakatifu akashuka juu yake katika sura ya njiwa.
Kisha sauti ikasikika ikisema,
‘Wewe ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa nawe.’
Ndugu zangu, tukio hili ni EPIFANIA nyingine ya Mungu na ni tukio la kuangaza! Kwa sababu nafsi tatu za Utatu Mtakatifu zipo. Baba anaongea. Mwana ni Yesu. Roho Mtakatifu ndani ya njiwa aliyeshuka. Baadaye, Yesu anawaagiza mitume wake kufanya wanafunzi kutoka kwa mataifa yote na kuwabatiza katika Jina takatifu la Mungu wa Utatu. Huu ndio ubatizo tuliopokea ndugu na dada zangu; sisi pia tumefanywa kuwa watoto wa Mungu mwenyewe.”
Kwa upande wao Shirika la Utangazaji la EWTN katika kuipamba siku hii waliuza swali,
“Kwa nini tunasherehekea Ubatizo wa Bwana?”
Huku wakitoa majibu ya swali hilo katika ukurasa wao huo.
“Siku hii inaadhimisha Ubatizo wa Yesu katika Mto Yordani na Mtakatifu Yohana Mbatizaji. Katika tukio hili, Yesu aliingia katika huduma Yake na kupata wanafunzi wake wa kwanza; Mtakatifu Yohane alimtangaza Kristo Mwana-Kondoo wa Mungu, ambaye njia yake alikuwa ameitayarisha; na hali ya Utatu ya Uungu ikadhihirishwa. Kanisa kwa ujumla huadhimisha Ubatizo wa Bwana Jumapili baada ya Januari 6. Mnamo 2025, Ubatizo wa Bwana unaadhimishwa leo Jumapili, Januari 12.”
Masomo ya jumapili hii ni kama Ifuatavyo;
“Somo la 1: Isa 42:1-4, 6-7 Nabii Isaya anatabiri juu ya unabii wa ujio wa mtumishi wa Bwana ambaye Roho wa Bwana yuu ndani yake. Huyu ni Mteule wa Mungu na anapendwa sana na Mungu. Kwa ujio wa Yesu maneno haya yalisikika Baba akiyasema kuhusu Mwanae. Wimbo wa katikati: Zab. 29:1-4, 9-10 (K) 11, Mungu anahidi kuwabariki watu wake kwa Amani. Kwa ujio wa Kristo Amani imeingia ulimwenguni. Somo la 2: Mdo. 10:34-38 Petro anashuhudia kwamba kwakweli Mungu hana upendeleo wowote. Yesu amekuja ulimwenguni kwa ajili ya watu wote sio kwa ajili ya watu wachache tu. Wale wote wanaokubali kuwa wake kwa ubatizo anawafanya wana wa Mungu. Injili: Mk. 1:7-11 Tunasikia kuhusu hali ya Marko kuhusu ubatizo wa Yesu anaye batizwa na Yohane Mbatizaji na kujidhihirisha kwa Utatu Mtakatifu.”
Mwandishi wa ripoti hii akiwa Wilayani Serengeti, hali ya hewa ni nzuri huku mvua ikinyesha na kuyafanya mazingira kando ya Mbuga ya Serengeti kuwa ya chanikiwiti na bila shaka wanyama katika mbuga yetu hii kubwa nchini Tanzania sasa wanajipatia maji ya kunywa na aina mbalimbali za majani yanayoota na kuchipua mbugani.
makwadeladius @gmail.com
0717649257

Post a Comment