NYATURU NYIRAMBA

 




Adeladius Makwega-Musoma MARA

Binti mrembo muuguzi anatoka zake kazini, akiwa amechoka hoi bini taabani, amebeba mkoba wake begani, anapita njia kando ya ofisini yake, anapita katika eneo lenye biashara nyingi, kama ujuavyo hali ya sasa ya Tanzania kila penye biashara nyingi hapako duka la dawa na vibanda vya wakala wa fedha.

Mandhari hiyo ya vibanda vya kubadilisha fedha kila mwanaume aliyekuwamo katika vibanda hivyo alivyogeuka kumtazama muuguzi anayepita alivutiwa mno na kila mwanamue  lijali alisema neno la mapenzi iwe moyoni au hadharani. Sarakasi za kuitafuta namba ya simu ya muuguzi huyu ni ya kila siku huku simu ya mkononi ya muuguzi wetu ikipokea fedha kutoka kwa wanaume wa kila aina bila hata ya yeye kuwaomba au kuwafahamu.

“Siku moja alikuwa Karikoo, jamaa akapiga simu, binti akajibu nipo Kariakoo nanunua vitu vyangu nipigie baadaye, jamaa akatuma laki tatu. Siku nyingine binti kapigiwa simu na jamaa huyu huyu kwa bahati mbaya mtandao haukuwa vizuri, siku hii simu ikawa haisikiki vizuri, jamaa akauliza kwanini? Binti akajibu simu yangu mbovu, hapo hapo jamaa akatumia laki sita binti akanunua simu nyingine ya laki nane akiongeza laki mbili zake.”

Kumbuka msomaji wangu binti muuguzi mrembo anarudi kwake, alipofika eneo hili la Wakala mmoja Msukuma alimuona binti huyu anapita jamaa wakala akawasha gari lake huku akimfuata kwa nyuma, huyu binti, alipomkaribia akamsalimia, kwa kuwa wanafahamiana kiasi, jamaa akamwambia karibu upande gari twende nikupeleke kwako. Binti Muuguzi mrembo kwa kuwa huyu jamaa wakala anamfahamu na ni miongoni mwa jamaa wanaotupa ndoano zao katika bahari ya mapenzi ya binti Kinyiramba na Kinyaturu na ndiyo wale wanaotuma mapesa , pesa uchawi wa mzungu binti akaingia garini vizuri.

“Wakiwa wanakwenda jamaa akabadilisha muelekeo wa gari, binti muuguzi mrembo akauliza huku wapi? Jamaa akajibu napita pahali kuna kitu nachukua kidogo, binti akasema haya, hakuna neno. Wakaenda gafla binti anashangaa gari imeingizwa katika nyumba ambayo geti limefunguliwa na gari lipo ndani.

 Jamaa akashuka kisha akarudi tena akimwambia huyu binti muuguzi shuka, binti anashanga yamekuwa hayo?

Binti akagoma. Jamaa alikuwa na mwili mkubwa, geti likafungwa. Jamaa akawa anamshika kwa nguvu kumshusha garini, zake zote kumtoa katika gari ili akampeleke chumbani kwake.”

Hii nyumba alipoingizwa binti muuguzi na huyu Wakala Msukuma ilikuwa nyumba ya kipekee hakuna watu na hata upige kelele namna gani nje haisikiki, kumbuka msomaji wangu ndani vita vimepamba moto, jamaa anataka kulazimisha penzi binti kagoma.Hapo sebuleni meza, viti , vyombo, runinga na makabati yanavunjika vunjika kelele zinapigwa lakini hakuna aliyeweza kusikia kinachoendelea.

“Jamaa japokuwa alikuwa na nguvu baadaye akachoka na binti akachoropoka na kukimbia kutoka nje ya nyumba hii, akauliza jina la eneo hilo na kupanda bodaboda hadi kwake, alipofika nyumbani kwake Wakala akapiga simu, wewe kwanini unanifanyia hivyo  utaona.”

Usumbufu ulipozidi binti huyu Mnyiramba&Mnyaturu akaamua kuibloki simu ya Wakala Msukuma, huku sasa binti muuguzi akawa anaendelea na kazi vizuri.

 


 

Siku chache zilipopita binti muuguzi akiwa kazini akatoka na mwenzake waende wakanywe chai mkahawani, wakafika kila mmoja akaagiza kinywaji chake, baada ya dakika tatu akaja jamaa yule Wakala Msukuma, akafika walipokaa hawa wauguzi wawili, jamaa bila aibu akawa anasema wewe si ulikuwa unajifanya mjanja , si ulikuwa unanikimbia na umenibloki simu zangu zote unadhani utanikimbia hadi lini?

Muuguzi huyu wa pili hajui kinachoendelea na wala hajui kilichotokea, muuguzi mtu mzima anashangaa huyu jamaa ni vipi ? Kichaa ? Hamnazo au Punguani ? Kwanini anasema maneno haya? Jamaa anaendelea kubwabwaja baadaye muuguzi kando akasema hawa jamaa wanafahamiana na huyu binti muuguzi? Jamaa anaongea hadi anatupa mikono kikombe cha chai kikaanguka chini. Jamaa anaongea kwa sauti ya juu lakini bahati nzuri biashara za mijini zina watu wengi watu wanajua hao watu wanaongea tu mambo ya kawaida kumbe ugomvi. Mama muuguzi mtu mzima akauliza jamani kwani vipi? Wakala Msukuma akasema

“Sista huyu dada kachukua pesa yangu na hataki kuirudisha sasa hivi ananikimbia kweli kweli na ndiyo maana nimemuona hapa alafu anataka kushangaaa.”

Binti muuguzi akasema hiyo siyo kweli, hapana kabisa huyu jamaa ananipenda amenitumia pesa kwa hiari yake, anataka penzi la nguvu na mimi simtaki. Mama muuguzi akasema swa kaka kama ni hivyo sawa lakini mlipashwa jambo hili kulimaliza kiistarabu, mnavyofanya hivyo mtadhalilishana na kuwapa watu faida. Wakala Msukuma akasema anataka pesa yake na yeye ni mshenzi hashindwi kulifanya lolote lile. Jamaa akapewa ahadi kulipwa pesa yake tarehe 16, hapo mkahawani kukawa na hali ya utulivu na hawa wauguzi kurudi kazini kwao.

Wakati wanatoka hapo mkahawani mama muuguzi mtu mzima akasema mwanangu jitahidi mlipe jamaa pesa yake mapema, kama hauna kakope , usipofanya hivyo huyu mwanaume ni hatari, kaa naye mbali ataweza kukumaliza na siku unapokwenda kumpa pesa hakikisha unakuwa na ushahidi ili jam bo hili liishe vizuri.


 

Binti muuguzi mrembo akatafuta pesa kabla ya tarehe 16 akapata mapema na kumtafuta daktari mmoja nayeye kuambatana naye hadi kwa Wakala Msukuma wakamkuta wakazungumza pesa yake karibu shilingi 1,200,000 /= na kumlipa.

“Huyu binti nafanya nae kazi anajiheshimu na sisi tunamuheshimu, wewe mwanaume mwezangu ukimpa pesa mwanamke kwa mahaba ni sawa na pesa iliyokwenda kwa mganga hairudi, pokea pesa yako sisi hatutaki maneno tena baina ya wewe na huyu binti.

Jamaa akapewa pesa yake.Wakala Msukuma akawa mpole huku akiomba msamaha sana kwa jopo hilo lililomfuata kibandani kwake.”

Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?

Kwa mujibu wa msimuliaji wa kisa hiki anasema kuwa muuguzi huyu Mnyiramba Mnyaturu ni binti mrembo sana, hata hapo kazini kwao ni binti ambaye anaonekana kwa haraka kwa urembo wake huku wanaume wengi wakirusha ndoano zao kwake, kizuri binti huyu anaye mpenzi wake anataka kufunga naye ndoa , akina mama wauguzi wamemshauri binti afunge ndoa haraka.

Pili akinamama wauguzi watu wazima wamemshauri binti huyu asipokee vizawadi kutoka kwa kila mwanaume maana binadamu wanatafautia mioyo na tabia.


 

Tatu kwa wasomaji wa Mwanakwetu watambue kuwa kitendo hiki alichofanya Wakala Msukuma ni shambulio la Aibu ambalo ukifuatilia simulizi hii kuna makosa mengi kulingana na Sheria ya Kujamiiana na 'Shambulio la Aibu kwa Mwanamke' - Sheria namba 47 ya mwaka 1954, kifungu cha 3 na Sheria namba 4 ya Mwaka 1998, na vifungu viningine vingi kikiwamo hiki,

Mtu yeyote kwa makusudi atasababisha shambulio la kijinsia la aibu kwa kutoa maneno, sauti au kuonyesha ishara itakayoonekana na mtu mwingine Adhabu ni kifungo kisichozidi miaka 5 au faini siyozidi laki tatu au vyote pamoja.”

Kwa hakika jukumu la kutazama makosa katika kisa hiki Mwanakwetu anawaaachia wanasheria ili watazame makosa hayo ni yepi kasha muumtumie Mwanakwetu katika barua pepe yake atayachapishia. na kutayarisha makala nyingine kwa shabaha ya kutoa elimu kwa umma.

Makala haya yametayarisha kwa nia ya kutoa elimu kwa umma tu juu ya shambulio la aibu

Mwanakwetu upo?

Kumbuka

“Binti Mnyaturu Mnyiramba.”

Nakutakia Siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257


 








0/Post a Comment/Comments