NAOMBA NA MIMI MNIOMBEE HERI

 



Adeladius Makwega-Musoma MARA.

 

Septemba 25, 2015 Baba Mtakatifu Fransisko alizungumza kwa Kiingereza kwa mara ya kwanza akiwa na watumishi wa Umoja wa Mataifahuku New York alipokuwa ziarani nchini Marekani huku akiongozwa na Mwenyeji wake Ba Ki-Moon ambaye wakati huo alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (2007-2016.)

Baba Mtakatifu Fransisko akiwa nchni Marekani kulikuwa na matukio kadhaa ya kuvutia mojawapo nikwenda gerezani na kuwatembelea wafungwa wa kike na wakiume na kuwabariki huku akipiga nao picha.

 

Siku ya leo Mwanakwetu anagusia namna Baba Mtakatifu Fransisko alivyozungumza Kwa Kiingereza na Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa.

“Wapendwa habari za asubuhi, katika hafla ya ziara yangu katika Umoja wa Mataifa, ninayofuraha kuwasalimu mabibi na mabwana ambao kwa sehemu kubwa nyinyi ni mhimili wa shirika hili, nawashukuru kwa makaribisho yenu na ninashukuru kwa yote mliyonifanyia na kuandaa kufanyika kwa ajili yangu, Ninawaomba pia muwape salaam  zangu za dhati kwa wanafamilia  wenu wote ambao hawakuwezakuwa nasi leo kwa sababu kazi nyingi za Umoja Mataifa zinafanyika nje ya hapa na nyuma ya pazia, juhudi zenu za kila siku zimefanikiwa maana kidiplomasia, kiutamaduni kiuchumi na kisiasa katika mipango ya Umoja wa Mataifa ambayo ni muhimu sana kwa ajili ya kukidhi matumaini na matarajio ya watu ambao wanaweza kusaidaia binadamu.

 

Ninyi ni wataalam mambo mbalimbali na mna uzoefu wa nyanja makatibu watafsiri, wafanya usagi wapishi Wafanyakazi wa usalama asante kwa yote unayofanya mkizunguka huku nakule mkijitoleakuchangia katika uboreshaji wa Umoja wa Mataifa pia kuna umuhimu mkubwa kwanu binafsi kwa jinsi mnavyozunguka kufanyakazi kunaonyesha utu wetu kwa  watu wengi, mmekuja katika jiji hili kutoka nchi mbalimbali, duniani kote kama vile wewe ni mjumbe wa ulimwengu wa watu ambao shirika hili linawakilisha na linatafuta kutumikia kama watu wengine wengi ulimwenguni kote,Pia nyinyi binafsi mnajali Maslahi ya Watoto wenu na elimu  yao natambua mna wasiwasi juu ya wakati ujao wa sayari hii.

 

Je itakuwa ya namna gani?lakini leo na kila siku ningewaomba kila mmoja wenu kujali uwezo wenu wote wa kuthamini watu wengine , kila mmoja awe karibu mwingine kuheshimiana na hivyo mjumuishe miongoni mwenu dhamira ya shirika hili la familia ya Umoja wa Kibinadamu inayoishi kwa upatano na kufanya kazi si kwa ajili ya amani tu bali kwa amani, amani itendayo kazi si kwa ajili ya haki tu bali katika roho ya Haki, Wapendwa nawabariki nawabariki kila mmoja wenu kutoka moyoni mwangu nitawaombea dua na familia zenu na ninawaomba kila mmoja wenu tafadhali akumbuke kuniombea na kama yeyote kati yenu siyo muumini namuomba anitakie mema , Bwana Mungu awabariki wote asanteni.”

 

Awali Baba Mtakatifu Fransisko alizungumza Kiingereza hadharani kwa mara ya kwanza alipokuwa akituma ujumbe wa video Oktoba 18, 2013 kwa washiriki wa mkutano nchini Ufilipino kuhusu uinjilishaji mpya.Msichoke kuwa na huruma kama ya Baba kwa maskini, wagonjwa, walioachwa, vijana na familia,anasema. Ili Yesu na ajulikane katika ulimwengu wa siasa, biashara, sanaa, sayansi, teknolojia na mitandao ya kijamii.Roho Mtakatifu afanye upya uumbaji na kuleta haki na amani katika Ufilipini na katika bara kuu la Asia lililo karibu na moyo wangu. ."Baba Mtakatifu Fransisko ni mzaliwa wa Ajentina, anajulikana kwa ufasaha wa kuongea Kihispania na Kiitaliano anajulikana pia anaweza kuzungumza angalau Kilatini, Kifaransa, Kijerumani, na Kireno, jumla kuu zikiwa lugha sabaa za Kimataifa. 


 

Si kwamba Baba Mtakatifu huwa haongei Kiingereza la hasha bali ni nadra mno kuongea Kiingereza mwanzo mwisho wakati anatoa ujumbe wake, mara nyingi huzungumza kiingereza huku na lugha zingine zikichanganywa kwa faida ya umma wa Wakristo Ulimwenguni.

 

Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?

Katika maelezo yake Baba Mtakatifu akizungumza na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa alisema maneno haya.

“…Wapendwa nawabariki nawabariki kila mmoja wenu kutoka moyoni mwangu, ninawaombea dua njema na familia zenu na ninawaomba kila mmoja wenu tafadhali akumbuke kuniombea na mimi lakini kama yeyote kati yenu siyo muumini namuomba basi anitakie mema, Bwana Mungu awabariki nyoote, asanteni.”

Kwa maelezo haya ya Baba Mtakatifu Francis yanaonesha mwanadamu yoyote hata kama siyo muumini basi lazima anahitaji wema kutendewa na mwenziwe, hivyo hivyo kwa waamini na wasio waamini, hata kiongozi mkubwa wa Kanisa ktemblea gereza kuwakumbuka wanadamu wenzetu na kama hili lingalizingatiwa kwa hakika dunia ingekuwa sehemu salama.


 

Mwanakwetu Upo?

Kumbuka,

“Hata Kama Siyo Muumini Basi Naomba Uniombee Heri.”

Nakutakia siku njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257.











 

 

 
 

0/Post a Comment/Comments