Adeladius Makwega-Musoma MARA
Sikukuu ya Epifania inawaalika watu wa mataifa yote kusafiri pamoja na Wanafunzi wa Yesu ili kutoa ushahidi kwa udugu wa ulimwengu mzima kwa kufuata nyota ya Mungu, na tuifanye ili kuwa kweli.
Haya yamesemwa na kadinali Luis Antonie Tagle, Mkuu wa Propanga Fide ya Kanisa Katoliki inayoshugulikia Uinjilishaji wa watu ya Kanisa katoliki Ulimwengu katika mahubiri yake ya kila dominika katika kipindi cha Word Expose cha Jumapili ya Sherehe ya Epifania Januari 5, 2025.
“Leo ni Sherehe ya Epifania ya Bwana. Tunasherehekea udhihirisho wa Mungu katika Mtoto Yesu kwa Mamajusi kutoka Mashariki. Hili ni tukio muhimu, ndugu na dada zangu, kwa sababu Mungu Mwenyewe alimfunua Mwanawe, Mfalme mpya wa Wayahudi, kwa Mataifa, au watu wasio Wayahudi.
Mungu mwenyewe aliwaongoza watu hawa kwa kuwaonnesha nyota, ambayo ilitumika kama dira yao. Kwa maneno mengine, kupitia tukio hili, Mungu aliwasilisha mpango wake wa kuokoa ulimwengu wote.
Baada ya kumpata mtoto Yesu, Mamajusi walifurahi sana. Wakamsujudia na kumpa zawadi zao za dhahabu, ubani na manemane.
Hawakumrudia tena Herode baada ya kuonywa.”
Kwa upande wa Kanisa la Mtakatifu Augustino Parokia ya Mwisenge, Jimbo Katoliki la Musoma ambapo mwandishi ripoti hii alisali Padri Julius Ogolla aliyeongoza Misa hii alitlia mkazo kwa mahitaji ya zawadi tatu zilizotolewa na Mamajusi kwa Mtoto Yesu hata leo kanisa la Yesu Kristo linazihitaji kufanikisha shughuli za kiroho..
“Manenamne siyo pesa bali na mafuta ambayo yalitumika kuwapa wafalme, viongozi na makasisi. Mfahamu kuwa hata mapadri wanapakwa mafuta hivyo mahitaji ya ubani, dhahabu na manemane kwa kanisa ni muhimu hata ukitoa kipande cha dhahabu kinawekewa utaratibu na kutumika kwa shughuli za kiroho.
Mahubiri ya Padri Ogolla yalitanguliwa na maelezo ya kina juu ya kuwaaga watawa wawili na kuwakaribisha watawa wengine watatu katika shughuli za kiroho Parokiaya Mwisenge hususani kufundisha Chekechea na Ukatekista, huku Padri Ogolla akisema kazi kubwa ya katekista siyo tu kufundisha Wakatukumeni bali hata watu wazima wenye umri mkubwa, kuhakiksha wanabaki katika imani.
Misa hii iliambatana na nia na maombi kadhaa , mojawapo ya maombi hayo lilikuwa hili,
“Ututie moyo wa kumtafuta na kumshuhudia Kristo Mwanao kwa ajili ya kuwahudumia wenzetu wenye shida kama vile; wagonjwa, yatima, wajane na wasiojiweza. Eee Bwana Twakuoma Utusikie.”
Hadi Ibada hii ya misa inamalizika majira ya saa mbili unusu ya Asubuhi hali ya hewa ya Mji wa Musoma ni jua la kadili nyakati za mchana huku mvua ikinyesha wa kudonoadonoa nyakati za usiku.
0717649257
Post a Comment