Adeladius Makwega-Musoma MARA
Sekretarieti ya Maadili ya
Viongozi wa Umma imesema kwamba Uadilifu wa Viongozi wa Umma ni jambo la msingi
kwa kila kiongozi ili kujenga imani kwa wananchi na hata kujiuzuLu ni kiashiria
cha uadilifu huku wakimkumbuka Aggrey Mwanri.
Haya yamesemwa Disemba 17, 2024 na Katibu Msaidizi wa Sekretarieti hii anajihusisha na Ukuzaji wa Maadili, ndugu Fabiani Pokelea hapa mkoani Mara akiongoza mada juu ya Uadlifu wa Viongozi wa Umma.
Akitoa mada hiyo hatua kwa hatua, ndugu Pokela alisema kuwa suala la uadilifu ni pana na hata kama wewe kama kiongozi unaona kuwa jambo ulilopanga kulingana na utaratibu uliowekwa kama halitekelezeki kujiuzuLu ni moja ya viashiria vya uadilifu.
“Je hapa Tanzania tunayo hiii tabia? Wenzetu wamejijengea tabia hii, kujiuzulu ni tabia njema na inaweza kufanikisha baadhi ya mambo yafanyike.”
Akitoa mada hii huku ukumbi huu ukiwa tulivu, zaidi ya kusikika kwa mbali mvumo wa mawimbi ya Ziwa Victoria, ndugu Fabian alisisitiza,
“Serikali ni watu na hakuna kitu kinachoweza kubebeka na kushikika kuwa hiki ni Serikali, Serikali inaonekana kwa namna viongozi wanavyofanya kazi zao, mambo yao, namna wanavyoendesha maisha yao ya kila siku.”
Mada hii iliendelea kutolewa kuwa ni vizuri kila kiongozi pahala alipo, akumbuke kuacha alama, akitolea mfano kuwa kwa desturi Tabora Mjini ilikuwa haina miti, kwa hakika aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora wakati huo Mh Aggrey Mwanri wananchi wa Tabora Mjini wanasema kuwa kiongozi huyu alipokuwapo hapo aliifanya kazi kubwa ya kusimamia upandaji wa miti, sasa Tabora Mjini ina Miti ya kupandwa tele.
“Kila kiongozi akumbuke kuacha alama katika maisha yake ya utumishi wa umma popote alipo, huo pia ni uadilifu .”
Akihitimisha mada hii ya Uadilifu wa Maadili kwa Viongozii wa Umma ndugu Pokela alitoa nafasi ya kuulizwa maswali ambapo maswali kadhaa yaliulizwa na kujibiwa.
0717649257
Post a Comment