HADHI SAWA KWA WOTE

 



Adeladius Makwega-Kwa Omari Kijana-MOROGORO

Mwishoni mwishoni mwa Novemba 2024 kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa nchini Tanzania, Mwanakwetu alikuwa nyumbani Kwake Kijijini Chamwino Ikulu ambapo alifika hapo kwa nia moja ya kufika Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo kufuatilia baadhi ya nyaraka zake za kiutumishi. Asubuhi  moja ya siku hizo kabla ya uchaguzi huo alimkumbuka Yasser Arafat ambaye pia anajulikana kama kama Abu Ammar kiongozi wa zamani wa kisiasa na Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Palestina yaani Munazzamat al Tahrir Filastiniyyah Kwa Kifupi ni (PLO) PEELEE OOO.

“Arafat Aliiongoza PLO tangu mwaka 1969-2004, alikuwa pia Rais wa Mamlaka ya Palestina tangu mwaka 1989-2004. Kiongozi huyu alizaliwa Cairo Misri Agosti 24, 1929 kwa wazazi wa Palestina ambapo utoto wake mwingi aliishi huko lakini baadaye alisoma Chuo Kikuu cha Mfalme Fuad 1, Arafat alikuwa ni miongoni mwa vijana wa Kipalestina waliyopinga kuanzisha kwa taifa la Israel mwaka 1948, huku alipigana vita vile vya Waarabu dhidi ya Israel mwaka 1948 akiwa mpiganaji wa wanamgambo wa Udugu wa Kiisilamu, ambapo ule muunganiko wa Mataifa ya Kiarabu ulipigwa na, baadaye alirejea Cairo Misri na akachaguliwa kuwa Kiongozi wa Umoja wa wanachuo wa Kipalestina tangu mwaka 1952-1956.”

Kumbuka msomaji wangu Mwanakwetu yu kwake hapo hapo alikumbuka matukio makubwa mawili ya kiongozi huyu wa Palestina wakati huo akiwa hai.

 Tukio la kwanza ni hili,

“Yasser Arafat mkewe alikuwa ni mama Mkristo Mkatoliki mzaliwa wa Yerusaleem Suha Arafat ambaye alizaliwa kutoka familia ya kisomi na tajiri, mama huyu ni mshairi, mwandishi na mwanasiasa wa Kipalestina, Mke huyu wa Arafat katika shughuli zake hizo alishakamatwa mara kadhaa na kutiwa korokoroni katika mahabusu na magereza ya Israel, mama huyu ni miongoni mwa waandishi wachache wa Kipalestina wenye heshima kubwa Ukanda Gaza.

 Suha Arafat aliingia katika masuala haya ya kiharakati kutokana na mama yake mzazi Bi Raymonda Hawa Rawi aliwahi kufanya kazi katika jarida la Propaganda za Kipalestina huku Yerusaleem ya Mashariki ambapo jarida hilo lilipinga ukandamizaji wa Wayahudi kwa Wapalestina nyakati hizo.”

 

Suha Mke wa Yasser Arafat alisoma shule ya Masista wa Kikatoliki inayofahamika kama Rosary’s Sisters School iliyopo Beit Hanina huku huko Yerusalem, alipofikisha miaka 18 akaenda kusoma Paris Ufaransa ambapo huko dada yake mkubwa alikuwa ameolewa na Ibrahim Souss ambaye wakati huo ndugu Souss alikuwa ni Balozi la Palestina nchina Ufaransa.


 

Kwa hakika Mwanakwetu yu nyumbani kwake anamkumbuka Yasser Arafat tu huku akitambua kuwa anayeyasoma makala haya anajiuliza ndoa baina ya Yasser Arafat Muisilamu wa dhehebu la Sunni na Bi Suha Daoud Tawil Mkristo Mkatoliki inakuwaje?

Kwa hakika Mwanakwetu akiwa kwake aliona kuwa itakuwa vema pia kueleza namna Yasser Arafat na Suha binti Daoud walikutana wapi na hiyo ndoa ilifungwaje?

Msomaji wangu majibu ni haya,

“Suha akiwa Ufaransa Arafat alikuwa na mawasiliano ya karibu na Balozi Palestina nchini Ufaransa Balozi Souss ndipo huko Arafat wakafahamiana na Suha, Yasser Arafat akamuomba Suha aende kufanya kazi naye huko Tunisia baada ya kumaliza Chuo Kikuu, ambapo PLO walikuwa na ofisi zao huku huko Suha na Yasser Arafat wakafunga ndoa kwa siri. 

Suha akiwa na miaka 27 tu  kumbukumbu zinaonesha kuwa Suha alizaliwa Julai 17, 1963 na wakati wanafunga ndoa alikuwa na Uraia wa Ufaransa, baadaye akawa na uraia wa Tunisia na pia Mpalestina, wakati wa ndoa hii Babu Yasser Arafat akiwa na miaka 61. Maisha ya ndoa yao baadaye wakajaliwa kuzaa binti Zahwa (1995) ambapo hilo ni jina la mama wa Yasser Arafat.”

 

Mwanakwetu akiwa kwake alibaini kuwa hajajibu juu ya ndoa baina ya Msunni na Mkatoliki ilikuaje?

“Je binti Mkatoliki msomi, Mkatoliki tajiri alibadilisha dini? Inadaiwa kuwa Suha alibadilisha dini na kuwa Muisilamu wa dhehebu la Sunni lakini Wapalestina wengi hadi kesho wanaamini kuwa Suha hakubadilisha dini yake hiyo ilikuwa geresha tu na ndiyo maana ndoa yao ilifungwa kwa siri.”

Wapalestina wengi wanaamini kuwa Suha amebaki na mipesa mingi kutoka kwa marehemu mumewe ambayo aliificha katika akaunti za siri huko ughaibuni.

Suha Arafat

 

Msomaji wangu kumbuka Mwanakwetu yuko kwake akakumbuka tukio la pili;Yasser Arafat akiwa hai, siku moja alikuwa anasafiri katika ndege akashuka katika uwanja mmoja wa ndege ili kubadilisha ndege, waandishi wa habari wa kimataifa wakamuona wakamuuliza, mzee siku ya leo ni sikukuu Krisimasi ambapo Wakristo ulimwenguni wanasherehekea kuzaliwa kwa mwokozi wao, wewe unasemaje? 

Kiongozi huyo wa PLO wakati huo akajibu kwa maneno haya,

“Ninawapongeza Wakristo kusherekea kuzaliwa kwa Masihi lakini mimi nina furaha zaidi kwa maana huyo wanayemsherehekea yaani Masihi Yesu Kristo alizaliwa Bethehemu kwa  hiyo Yesu alikuwa Mpalestina .”

Baada ya tukio hilo vyombo vya Habari vya Ulaya vikaripoti

“Jesus Was Palestinian-Yasser Arafat.”

Jambo hilo likawa kero kwa mayahudi.

Kumbuka Msomaji wangu Mwanakwetu yupo nyumbani kwake Kijiji Chamwino Ikulu, gafla akapigiwa simu na mama mmoja wale Wizarani akimwabia Nyaraka ziko tayari, hivyo njoo uchukue, Mwanakwetu akatoka kwake kuelekea Mtumba Mji wa Serikali, kuzifuata nyaraka hizo.

Akiwa anatoka kwake tu umbali kama mita 400 akakutana jamaa wa CCM, jamaa mmojawapo  anayefahamianaye, Mwanakwetu akajibu kwema. Jamaa akanadi biashara fulani  Mwanakwetu akasema hana pesa mimi nipo mufulisi.Jamii huyu ana baiskeli aina ya Sports akashuka kwenye baiskeli huku ana bahasha ya karatasi  mkononi wakawa wanatembea huku wanaongea bei hiyo bizaa.

Jamaa huyu baadaye akasema,

“Jirani mimi mwenzako nimepata bahati, nagombea ujumbe serikali ya Kijiji, nipo katika mchakato huu wa uchaguzi wa sasa.(Mwanakwetu akampa heko)

Tunachopambania sasa ni kura ya Ndiyo CCM au Hapana CCM maana hakuna wapinzani. Hapa Kijijini Chamwino Ikulu yupo mama(Rais Samia) wapinzani hawana nafasi na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi kasisitiza sana hilo kutomuangusha mama.”

Mwanakwetu akampa tena hongera  jamaa huyu akamwambia kuwa mimi hapa sipigi kura maana sijajiandikisha. Akilini mwa Mwanakwetu anajiuliza huyu Katibu wa CCM ni nani Je Nchimbi au katibu Mkoa? Mwanakwetu akamjibu ndugu huyu nitakuletea pesa ya kununua maji wakati wa kampeni, jamani akasema asante sana jirani.Mwanakwetu akavuka barabara na huyu jamaa naye  kwenda Ofisi ya CCM ya Kijiji Cha Chamwino Ikulu. Hapo Mwanakwetu akapanda basi kwenda Mtumba akafika kuchukua nyaraka zake zile alizopigiwa simu, akafika akazipokea na kuanza kurudi Kijijini Chamwino Ikulu.


 Arafat akiwa katika kambi ya wakimbizi

Akiwa anarudi akakumbuka maisha ya Yasser Arafat tangu anazaliwa Cairo Misri, akawa mwanamgambo wa Udugu wa Kiisilamu akawa Kiongozi wa PLO hadi anakutana na Suha Daoud mama wa Kikatoliki. Mwanakwetu akakumbuka namna Yasser Arafat alivyodiriki kumuita Tunisia Suha nakufanya naye kazi, baadaye kumpenda mwanamke huyu wa Kiikristo na baadaye kumuoa kwa siri na hadi kuzaa naye mtoto mmoja.

Mwanakwetu akatazama katika simu yake mwaka 1980-1990 huko Palestina idadi ya Waisilamu ilikuwa karibu asilimia 90 na wakristo ni asilimia ndogo sana. Yasser Arafat aliwaacha mabinti wa Kiisilamu na kufunga ndoa na Binti wa Kikristo ambaye ni sehemu ya jamii yake, amekaa naye hadi Kifo kilipowatenganisha. 

Mwanakwetu kumbuka yupo ndani ya basi la Makole Chamwino Ikulu, hapo hapo akammkumbuka yule mgombea ujumbe Serikali za Kijiji cha Chamwino alivyokuwa anaongea naye akisema kuwa hapa Kijiji Chamwino Ikulu yupo mama, Wapinzani hawana nafasi.


 

Mwanakwetu moyoni akapinga hilo kabisa akisema moyoni siyo kweli, tena ilitakiwa vyama vya upinzani vingejitokeza vyote vyenye usajiri wa kudumu na kuwa na wagombea wao katika kijiji cha Chamwino Ikulu na majina yao yangerudishwa na wangefanya kampeni huku viongozi wa kitaifa wa hivyo vyama wangefika hapa kijijini kuomba kura.

Wakati wa Kampeni kwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni mkazi wa hapa na anapiga kura Kijijini Chamwino Ikulu, ungetengenezwa utaratibu Rais Samia mwenyewe angesikiliza mikutano ya Kampeni ya vyama hivyo hapa Kijijini hata vyama pinzani viwili tu, huku huku akikaa upande wa wananchi, huku akiwa mvumilivu na mstamilivu hata kama wangemsema vipi mkutanoni, huku vyombo vya habari vya kitaifa vingeripoti tukio hilo. Tukio hilo lingeupa uhai mkubwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ungeupa uhai mkubwa uchaguzi mkuu wa 2025 na ungempa heshima kubwa Rais Samia Suluhu katika ulimwengu wa siasa za Tanzania na kimataifa.

Kumbuka msomaji wangu Mwanakwetu yu basini anarudi kwake akasema kama alivyomtazama Yasser Arafat maisha yake ndivyo hapo baadaye Rais Samia atatazamwa namna alivyoishi na jamii ya wapinzani.

 Hivi kweli ukizatama vyama kadhaa vyenye usajili wa kudumu kweli kijiji cha Chamwino Ikulu watu wanaikubali CCM 100 kwa 100? Jibu lake hapana.

 Kwa utafiti mdogo wa Mwanakwetu vijana wengi wanaunga mkono hizo siasa za upinzani. Hata kama mpinzani kashinda kuwa mwenyekiti wa Kijiji Chamwino Ikulu, kila shughuli za Ikulu anaalikwa akiwa na mavazi ya sare za chama chake hilo linajenga ujamaa na udugu baina ya walio wengi na wachache na hicho ndicho kilichofanywa na TANU dhidi ya ASP wakaungana, Tazama Tanganyika lilivyo kubwa wakaungana na Zanzibar yenye eneo dogo dogo wakawa katika hadhi sawa na hivyo ndivyo alivyofanya Yasser Arafat Msunni dhidi Suha Arafat Mkatoliki.

Baadaye Mwanakwetu alifika nyumbani kwake salama.

Ndugu zangu kwa leo inatosha sana.

Kumbuka,

“Toeni Hadhi Sawa Kwa Wote.”

Nakutakia heri ya Krisimasi na Mwaka mpya wa 2025.

makwadeladius@gmail.com

0717649257

 

 

 


 


 

 


Arafat mwenye koti jeusi akiwa na dada yake mkubwa na mdogo wake hapo ni Cairo Misri/

 

0/Post a Comment/Comments