Adeladius Makwega -MBAGALA
“Ninayo
furaha kubwa sana kupata fursa ya kuadhimisha Ibada ya Ekaristi katika Kanda
hii ya Ziwa. Ninatoa shukrani kwa Askofu Mkuu Anthony Mayala kwa maneno
yake mazuri ya kunikaribisha, na ninawasalimu kwa upendo mkuu ndugu zangu
Maaskofu, mapadri, watawa na walei wote wa Jimbo Kuu la Mwanza na wa
Majimbo ya Bukoba, Geita, Musoma, Rulenge na Shinyanga. Pia ninawasalimu kwa
namna ya pekee viongozi wa Serikali na wa siasa, wawakilishi wa Jumuiya
mbalimbali za kikristo na wa madhehebu mengine na watu wote.”
Haya yalikuwa maneno
ya sentensi ya pili iliyozungumzwa kwa
Kiswahili na Baba Mtakatifu Yohane Paulo wa II(Mtakatifu Yohane Paulo II)
alipokuwa katika Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza Septemba 4, 1990. Akiendelea
kuongea katika ardhi ya mkoa wa Mwanza hapa hapa Tanzania, katika sehemu ya
mwisho ya mahubiri yake aya ya nne Baba Mtakatifu Yohane Paulo II alisema
maneno haya,
“Kwa kutii amri ya Bwana—‘Mpendane
kama nilivyowapenda ninyi’ nyinyi, Wakristo wa Kanda ya Ziwa, mnachangamoto ya
kufikiria kuhusu hali katika nchi yenu wenyewe. Je, wazee, wajane, walemavu na
wapweke hupata kati yenu uelewa na usaidizi wanaohitaji ? Je, utu wa kibinadamu
wa watu wote huheshimiwa sikuzote? Au je inatishwa na mazoea kama vile uchawi
au uchawi huwaongoza wale wanaojihusisha nayo kwenye aina za utumwa na ibada za
uwongo? Kadhalika pamoja na kwamba kuna maadili mengi ya kweli na yanayosifiwa
ya kibinadamu yanayohusiana na mila za ndoa za kimila kama vile mahari, je,
kukithiri kwa matumizi mabaya ya mila hizi hayasababishi mitazamo inayohukumu
utu na thamani ya mtu kwa misingi ya mali na mali tu? ”
Haya yote yanadokezwa na
Dkt Simeon Mesaki Raia wa Tanzania wakati akifanya utafiti wake wa Shahada ya
Uzamivu (PHD) wenye jina Uchawi na Mauaji ya wachawi Tanzania wa
Chuo Kikuu cha Minnesota mwaka 1993.
Mwanakwetu anajiuliza tangu
Baba Mtakatifu Yohane Paulo wa II afike Tanzania mwaka 1990 hadi leo si miaka
mingi? Jibu ni miaka 34 kama ni mingi au michache msomaji wangu jibu unalo.
Swali lengine la
Mwanakwetu je vijana waliozaliwa Mwanza/Tanzania baada ya ugeni huo je msimamo
huo wa Vatikani kwa Mwanza je wanaufahamu? Je ujumbe wa Vatikani kwa Mwanza umeweza
kuibadilisha jamii hii na kuachana na Imani za Kishirikina? Hilo ni swali
ambalo lazima liwe na majibu.
Kwa hakika Mwanakwetu yupo
mkoani Mwanza sasa kwa karibu mwaka mmoja na miezi sita hoja ya ushirikina bado
ipo na tena hata kwa vijana waliozaliwa baada ya ujio wa Baba Mtakatifu Yohane
Paulo wa II.
“Mtani hao mbuzi na
kondoo wako usipotumia dawa za jadi kwa hakika watakufa wote, jitahidi kutuona
wenyewji tukupatie dawa za mifugo za kimila ili mifugo yako ibaki salama. Hapa
watu wengine wanaiangalia kwa kijicho hakuna mtu anayependa wewe ufuge upate
mbuzi na kondoo wengi.”
Haya maneno anaambiwa
mtayarishaji wa makala haya mapema Januari 2024 imani ya ushirikina bado
imekita kambi.Isitoshe hata kitendo cha Padri wa Kanisa Katoliki wa Kanda ya
zimwa kukamatwa kwa tuhuma za mauwaji ya binti mwenye ualibino hiyo ni kengele
inayoonesha ushirikina umekita kambi katika ardhi ya Tanzania. Mwanakwetu
akiishia kuitazama mifano ya Kanda ya ziwa tu hilo halitokuwa haki, ebu tilia
maanani kisa hiki,
“Nikiwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Halimashauri ya Lushoto mwaka wa 2017. Siku moja niliamka asubuhi
na kukuta mifugo yangu kadhaa imeuwawawa ikiwamo mbuzi, kuku paka na ngombe. Hili
lilikuwa tukio la kushangaza inakuje mifugo hiyo ife kwa wakati mmoja?Je
imelishwa sumu. Nikajitahidi , nikavijulisha vyombo vya Ulinzi na Usalamana
baadaye kuelekea kazini na nilipofika katika jengo la Halmashauri baad ya
kushuka katika gari nikakuta kundi la wafanyakazi wapo mlangoni, wakisita
kuingia ofisini , maana wamekuta damu zimemwagwa katika mlango. ‘Mkuu damu
zimemwagwa koridoni usivuke ngoja kwanza .’ Mkurugenzi akasema labda mbwa
alikuwa anawinda usiku akabeba windo lake akalila katika sakafu za Halmshauri.Wafanyakazi
hawaamini hicho kinachosemwa na mkurugenzi.’ Wafanyakazi wanajibu hapana huu ni
ushirikina.Mkurugenzi kasahau kwake mifugo yake imeuwawawa. Usafi ukafanyika
huku mkurugenzi Mtendaji akiingia kupitia mlango wa dharula.
Jambo hilo likaleta taharuki
kubwa wengine wakisema wanyama waliuwawawa nyumbani kwa kiongozi damu yake
ndiyo iliyomwagwa sakafuni ofisini nia ni kumroga Mkurugenzi Mtendaji, kwa kuwa
washirikina hao waliamini mnapotaka kumroga mtu wa PWANI Tanzania basi kumroga
ili alorogeke vizuri unamroga kwa wanyama wake mwenyewe.”
Mkurugenzi Mtendaji
husika aliongezwa Ulinzi. Hili ni tukio la Lushoto mkoani Tanga.
“Oktoba 2024 huko Ruvuma
Tanzania familia moja imemzika akiwa hai Baba yao mzazi kisa kwa kumtuhumu kumuua
kwa kumroga mwanawe wa kumzaa.”
Haya ni ya Tanzania ya
hivi sasa, Mwanakwetu bado imani katika ushirikina imekita mizizi.
Dkt Simeon Mesaki katika
utafiti wake anarejea visa vingi vya masuala ya kustajabisha wakati wa ujamaa
ambayo yanalingana na hata visa vya leo hii.
Kujishughulisha sana na
uchawi kumefanywa kuwa suala la kitaasisi hivi hata mtoa maoni mashuhuri
ameinua hali hiyo hadi kufikia kiwango cha ‘utamaduni’ (Okema, Business Times,
Agosti 4, 1989). Baadhi ya Vipindi
tofauti vina vilivyorekodiwa kwa namna ya kipekee mno mathalani;Mnamo Aprili
1992, mamlaka za Mkoa wa Kilimanjaro ziliwekwa katika hali mbaya sana zilipolazimika
kuamua kumruhusu mganga wa kimila kuendelea na kuwaokoa vijana waliotekwa
nyara. na mchawi kama Zombi katika msitu karibu na mji wa Moshi. Kwa mshangao
wa watu wengi, Mkuu wa Mkoa wa Mkoa huo wakati huo alimruhusu mganga huyo
kufanya kazi yake (kufanya vitu vyake) vya kuwarudisha wahanga hao kwa gharama
za serikali.’Haya ni Daily News Aprili 16, 1992 na Uhuru Aprili 16, 1992 haya
ni yalikuwa magazeti serikali ya Tanzania wakati huo. Katika kufanya uamuzi huo
usio wa kawaida, alisema kuwa serikali ‘ haikuamini uchawi’ na kusema kuwa
ingawa ‘haikuondoa ukweli unaowezekana wa jambo hilo na inahitaji ushahidi
madhubuti na kupata ripoti ya mwisho juu ya kesi hiyo.’ Mwishowe, hakuna
waathiriwa wanaodaiwa kupatikana, wala serikali haikumshtaki mshukiwa wa uchawi,
kwa sababu ya kutokuwa na ushahidi wa kutosha. Kweli, mtuhumiwa wa mchawi,
Rehema Daudi, alijigamba kwa kuifungulia serikali mashtaka ya kumkashifu. Hapa msomaji
wa Mwanakwetu unaweza kurejea gazeti la Mzalendo, Septemba 20, 1992.
Kwa upande mwingine,
katika kesi isiyo ya kawaida ya mwaka 1991, mahakama ya mwanzo katika manispaa
ya Tabora ilitoa uamuzi wa kumlipa fidia mwanamke mmoja wa mjini Tabora aliyedai
kuwa tawi la chama tawala.
(Chama Cha Mapinduzi-CCM)kilimtuhumu kwa uwongo kuwa anafanya uchawi na kumlazimisha kuhama mjini, haya
unaweza kurejea gazeti la Mfanyakazi la Juni 13, 1992. Mwanzoni mwa mwaka 1992,
wanavijiji wengi wa wilaya ya Songea walipitisha njia mpya za kutumia haki zao
za kidemokrasia kwa kufanya mikutano na kupiga kura ili kubaini nani kati yao
ni mchawi. Kutokana na hali hiyo, michango ilitolewa ili kuwawezesha waliotajwa
kuwa wachawi kusafiri hadi kwa Bibi Kalembwana, mtaalamu wa masuala ya uchawi huko
Mahenge Wilayani Ulanga, kwa ajili ya ibada za ‘kusafisha’
Mwezi Aprili mwaka huo
huo, vijana thelathini na sita wenye umri kati ya miaka 16 na 30 wa kijiji cha
Namabengo, wilayani Songea, walikabiliwa na kesi ya mauaji kwa kumuua Gabriel
Malembo (65) ambaye walidai.alihusika na vifo vya vijana wengi kijijini kwao
haya yamenukuliwa kutoka gazeti la Uhuru la Aprili 7, 1992. Hatua hizi na zile
zinazomhusisha Bi Kalembwana, zilizua taharuki katika duru za serikali za
wilaya, si tu kwa sababu ya uvunjifu wa moja kwa moja wa amani bali pia
kutokana na athari mbaya za kiuchumi za wateja ambazo Bibi wa Mahenge
aliwavutia.
Mnamo Februari 1992
polisi wa Mbeya mjini walilazimika kutuliza ghasia za watu takriban 2,000
waliokuwa wamekusanyika kurusha mawe kwenye nyumba na gari la mtu maarufu mjini
hapo. Uvumi kwamba mkazi huyo alikuwa amehifadhi mafuvu ya kichwa na mifupa ya
binadamu ambayo inadaiwa alikuwa akiitumia kwa ajili ya uchawi haya
yaliripoyowa na gazeti la uhuru la Februari 27, 1992.
MAREHEMU ASKOFU MKUU WA ZAMANI WA MWANZA MHASHAMU ANTONY MAYALA.
Huko hapa mkoani Mwanza kulikuwa
na hekaheka ya kuwaondoa watuhumiwa wa uchawi katika mikoa ya kanda ya ziwa hasa
Mwanza na Shinyanga kama ilivyoripotiwa na Daily News Septemba 5, 1990. Kwa
hakika haya mambo ni mazito hata katika utafiti wake wa Wazaramo wa
Dar-es-Salaam, Lloyd Swantz mwaka 1990 aligundua
kuwa waganga 700 wa dawa za kienyeji waliorodhesha uchawi kuwa wa pili kwa
wateja wao. tatizo kubwa zaidi. Kulingana na uchunguzi wake,
"...karibu kesi
5,000 kila siku huko Dar-es-Salaam zilihusu shutuma za uchawi na ulozi"
Swantz alichukulia
takwimu hizi kuwa zenye matatizo sana katika jiji la Dar-es-Salaam. Wasiwasi
wake ulirudiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar-es-Salaam
alipokuwa akiwaonya wakazi wa jiji hilo kwa kuambiwa bahati zao na wapiga
ramli, wapiga ramli au wapiga ramli. Badala yake, aliwataka kutumia huduma za
bure zinazotolewa na hospitali za serikali haya ni ya Uhuru Mei 23, 1990.
Haya ndiyo mambo ya
ushirikina nchini Tanzania ambayo waamini wake ni wengi hata wasomi ,
wanasiasa, viongozi ,viongozi wa dini huu mchanganyiko maalumu.
Mwanakwetu anasema nini
siku ya leo?
Msomaji wangu huo ndiye
ushirikina na mahusiano yake katika shughuli za kiserikali na za kijamii. Kwa
Tanzania ya leo suala la ushirikina na mauwaji ya watu yanakwenda sambamba na masuala
ya watu wasiojulikana.
Hili ni jambo jipya na
geni. Je wanaotekwa, na kuuwawa siyo kwamba mtu anakwenda kupiga chabo
sehemu(ramli) akishajua huko na kupata jawabu fulani ni mbaya ndiyo anateka na
kumfisha?
Hilo ni swali, swali lengine
la kujiuliza je kwanini haya matukio yanatokea sambamba?Je watu wasiojulikana
ni kundi jipya la aina ya ushirikina wa kisasa? Kwa hakika Watanzania tunalo
jukumu la kujiuliza na kupata majibu.
Kama Baba Mtakatifu
Yohane Paulo wa II angekuw a hai mpaka leo alafu angekuja Tanzania kwa hakika
angeiambia Tanzania.
“Wapendwa katika Kristo
sasa mna aina upya ya Ushirikina ambayo ni watu wasiojulikana.”
Mwanakwetu Upo?
Kumbuka- Wasiojulikana Aina
Mpya ya Ushirikina.
Nasema,
Ahlan Wa Sahlan.
0717649357
Post a Comment