Adeladius Makwega-MBAGALA
Mwanakwetu nilikuwa nafanya kazi pahala fulani, siku moja nikiwa kazini nikamuona kijana mmoja mdogo wa kiume ambaye ilikuwa sura ngeni machoni mwangu, nikamsalimia;
“Wewe bwana mdogo hujambo? Kijana akajibu hajambo na kunipa shikamoo, nikaitikia marahaba nakuendelea na shughuli zangu za kila siku.”
Mwanakwetu ninaendelea na kazi zangu za kila siku huku ninamuona huju kijana kaka tu baada ya juma moja nikaamua kumuuliza, wewe kijana mbona unakaa tu hapa unafanya nini? Kijana huyu alivyokuwa mjanja na akili akaamka kitini kuja alipo Mwanakwetu, alafu akaanza kujieeza.
“Mzee mimi nimekuja hapa mazoezi ya vitendo nimemaliza cheti cha taaluma hii.”
Mwanakwetu akasema bwana mdog siku zote umekaa tu mbona ulikuwa hausemi?Kijana akawa anafanya kazi na Mwanakwetu japokuwa elimu yake ndogo sana lakini katka kufanya nae kazi kama mwezi nikabaini kijana huyu alikuwa na uwezo na kipaji kikubwa sana hilo likafanya hadi mkuu wa taasisi akawa anamuulizia na hata mkuu wa taasisi alipoambiwa kijana yupo mazoezi ya vitendo hakuamini.Kijana huyu alikuwa na kasoro moja
siyo kila mara anafika kazini.Mwanakwetu akawa anamkokota maana akiwa hayupo Mwanakwetuaakawa anasema kaz hii ingependeza afanye fulani lakini losalale hayupo kazini akawa anakokotana naye aweze kufika kazini kila siku na akawa karibu Mwanakwetu .
Baada ya kuwa nafanya nae kazi kwa karibu mama aliyemsaidi kupata field akaambiwa Kijana wako uliyemleta anaelewana sana na Makwega kwa hiyo uwe na amani kijana wako yupo katika mkono salama. Huyu mama akapata zile kesi za hujumu uchumi- kibarua kikapotea na baadaye mama akafariki dunia, kazini hata watu wasema wewe ni mbaya namna gani lazima utakuwa na marafiki ya huyu mama rafiki zake wakubwa kabisa wakamfuata Mwanakwetu,
“Makwega tunatambua wewe ni hondohondo mlezi wa wana, tunashukuru, endelea kumsaidia huyu kijana, japokuwa mwenzetu ndiyo hayo yamemkuta.Sote tumezaa endelea na moy huo.”
Kazini pale palikuwa na vijana wengi wale wanaokaa naye jirani huyu kijana wanakwenda kumfuatilia muda mwingine wanamkuta na muda mwingine wanamkosa wakisema hapo anapokaa hajaonekana siku tatu hadi nne na hata hapo anapokaa alikuwa anasaidiwa na watu wanaotoka kijiji kimoja na baba yake.
“Vijana wangu walikuwa wananiheshimu sana , hilo hata kesho, nikawa nawaambia huku serikalini nyinyi wenye ajirani ya kudumu pendaneni bila kujali huyu yu mazoezi huyu ana ajira- kikubwa ni upendo, hawa ambao wako mazoezi ukiona anavaa shati moja hadi linanuka kikwapa usimcheke, wewe kusanya mashati nyumbani kwako weka kwenye mfuko na kesho yake njoo nayo kazini mpe na mwingine atampa pesa ya sabuni ,ndugu huyu akinuka kikwapa hapa hapa hapa hata mkisema mtakuwa na haki kinyume na hapo ni dhambi.Jambo Unalolisema Kwanza Lipatie Suluhu. ”
Vijana wangu wakanielewa vizuri, shida ikabaki kwa maudhurio ya yule kijana. Kijana akarudi na kuendeea na mazoezi huku akiwa a uwezo mkubwa lakini ukimfuatilia unabaini kuw a bwana mdogo anashida, baadaye akapotea tena hakuonekana kama juma zima ikabidi mtu mzima niende kwao, nikafika kwa bahati mbaya sikumkuta lakini hii nyumba anayokaa wakinipa kijana akaniongoza kumtafuta alipo njiani nikiwa katika harakati hizo nikakutana na mwanahabri Alvar Mwakyusa wa TSN mwandishi mzuri habari za kimombo, huyu alikutana na Mwanakwetu pae KULIKONI&THISDAY nikamwabia nipo kwenu kuna kijana wangu nimekuja kumfuata, siku hii Alvar Mwakyusa nilimkuta mkononi kabeba magazet yake kando yuko na mrembo mmoja , baadaye nikampata huyu kijana nikaongea naye vizuri kijana akasema;
“Mzee nashukuru kwa kuja, mzee inakuwa ngumu kuja kila siku maana yule mama aliyenitafutia field tangu apate shida kazini na kufariki sina msaada na hata hapa ninakaa kwa hisani tu hawa jamaa, marehemu mzee wangu alikuwa jirani nao na pia yule mama aliyefariki-mzee alikuwa mtumishi katika vyombo vya ulinzi na usalama alifariki, sasa mzee kila Alhamisi, ijumaa, Jumamosi, Jumapili na siku za sikukuu huwa nina dili la uchoraji wa tatooo hasa akina mama, huwa ndiyo linaloniweka mjini kwenye hizi kasino kwa hakika Napata pesa ila kazi yenyewe ni ngumu na ulevi na ushawishi wa kila aina.”
Kumbuka alipokuwa anakaa huyu kijana ni jirani na mwanahabari TSN Alvary Mwakyusa lakini mwanahabraia Mwakyusa hamfahamu huyu kijana. Mwanakwetu hapa hapa akapata kitu kipya lakini maelezo ya huyu kijana yalimyima amani pale alipomdokeza juu ya uchoraji wa tattoo hizo namna zinavyochorwa;
“Kwenye manyonyo, mapaja, sehemu za siri ,vifuani na mgongoni,mikononi lakini wanachorwa sana hizi tattoo ni akina mama wenye uwezo wao.”
Kijana huyu aliongeza kuwa asipokuwepo simu zinakuwa nyingi na nikiwa hapo matumizi a pombe na madawa ni jambo la kawaida. Akili ya Mwanakwetu aliyetoka Mbagala kumtembeea bwana mdog huyu imechanganyikiwa, bwana mdogo akaulizwa je picha gani ambazo umechora mara nyingi,kijana akajibu;
“Nge, Ngandu, Kaa, Nyoka,Alama ya Hatari, Mifupa ya Bindamu, Mafuvu, Visu, Panga, Bunduki ,Wanyama kama Simba na Chui ”
Kijana akaulizwa wewe unasali wapi? Kijana akajibu yeye ni Mkatoliki.
Mwanakwetu akasema maneno haya;
“Mimi Mkatoliki lakini sifahamu Kanisa linamsimamo gani juu TATOO lakini kwa mazingira uliyonisimulia na kwa michoro unayochora mimi ninaona hapo kuna shida-hiyo siyo sehemu salama.”
Huyu kijana anasikiliza na nipo kijiweni nilipomkuta na wenzake wapo kando kama hatua tano, nikamsimulia kisa;
“Mwanangu mimi nilipokuwa mdogo nasoma Shule ya Msingi Mkuranga nadhani mwaka 1985-1986 nilikuwa na rafiki yangu anaitwa Shah Uwanga-Shahaulanga Huyu Shah jina Shah neno la Kiarabu linalomaanisha mfalme, miaka tuliyozaliwa sisi katika Ulimwengu wa Kiisilamu hasa Iran walikuwa Mfalme wao aliyefahamika kama Mohammad Reza PAHLAVI SHAH, huyu Shah wa Iran alipinduliwa na mapiduzi ya Irani ambapo Ayatollah Mkuu Khomein akanyakuwa madaraka mwka 1979. Kwa hiyo Shahulanga alipewa jina kwa heshima na Mfalme huyu-Hata Uimwengu wa Kristo utakuta majina fulani ya watoto wanaobatizwa miaka fulani ni wengi wanapenda jina fulani na ni kutokana na umaarufu wa watu fulana mathalani watakatifu wa karne hiyo.”
Msomaji kijana ananisikiliza kikubwa jina Shaha Uwanga ametajwa,
“Shah Uwanga jina lake halisi ni Shah Mohamed na mwka 1985 (Darasa la tatu) 1986 (Darasa la nne) .
Huyu Shah jina la UWANGA alilipata kwa kuwa alikuwa muuzaji maarufu wa UWANGA ambapo n kama bwimbwi (unga) la mmea Uwanga unajiotoea porini alafu unaweka kiazi chini yake ukichimba kinatwangwa na kuwa unga alafu unaweka sukari, kwa hiyo Shah Mohammed kwao walikuwa hodari wa kutengeneza Uwanga huo anauweka katika mfuko anakuja nao shuleni anatuuziawanafunzi kwa siri darasani na saa nne anauza wazi wazi hapo ndipo akabatizwa jina Shah Uwanga kwa hiyo tukiwa wadogo tunajifunz a kuchora akawa anatuambia kuwa msipenda kuchora chora na hasa picha ambazo hazieleweki hizo picha mnazochora mwisho wa siku zitawagarimu maana zitakuwa roho na wewe unayechora utadaiwa hizo roho.”
Kumbuka Mwanakwetu yupo anaongea n a huyu kijana aliyemfuata kwake.
SHAH WA MWISHO WA IRAN
Nikamwabia hata wewe unaoshinda kasino unachora hayo mapicha tena mapicha mabaya utadaiwa hizo roho- nikwamwambia mimi sifahamu juu ya kanisa katika haya lakini ninavyoona maelezo ya rafiki yangu Shah hapa yatakuwa na kweli nakuomb achana na hiyo kazi alafu tuone kama Mungu atakutupa tilia maanani hii kazi unayojifunza sasa. Nikaagana na huyu kijana na kuondoka zangu kurudi nyumbani kwetu Mbagala njiani nilikutana na Alvar Mwakyusa wa TSN nakumuaga.
Kijana huyu kweli aliachana na uchoraji wa tattoo hizo na safari za kasino ziliishia hapo hapo akawa mtu mzuri sana sasa ni baba na familia yake kwa wakati nayatayrisha makala haya nikakumbuka Mei 18, 2019 nikiwa nanatoka Mbozi narudi zangu Tanga baada ya Kutumbuliwa na Mzee Magufuli kijana huu analinitumia shilingi 53,000 akisema mzee nimesikia yaliyokupata pole sana, hiyo pesa naomba uitumia kula chakula cha mchana safarini na kweli pesa hiyo tulipofia Morogoro Mjini Mwanakwetu , mkewe na jamaa wengine wawili tulikula chakula kando ya karakana ya Kanisa Anglikana Morogoro Mjini .
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Kikubwa vijana wa Kitanzania wanapitia changamoto kubwa ambazo lazima viongozi na wenye mamlaka watambue hilo viongozi waache ubinafsi, jamani tunatakiwa kutilia maanani masuala ya watu.Hususani vijana na yatima maana wengine wazazi wao wamefariki katika utumishi wakiijenga hii hii Jamhuri.
Pili imani ya Shah Mohammed-Shah muuza uwanga pae Shule ya Msingi Mkuranga juu ya Vikaragosi ni dhambi, ambapo imani hiyo unaweza kuona kwa upande mwingne iliwakatisha tamaa akina Mwanakwetu kuendeleza kipaji cha uchoraji lakini hii imani inalinda uhai wa binadamu maana kama kuchora tu kunafanya udaiwe roho je kumfisha mtu itakuwaje? Imani hii inajenga utu kwa binadamu mwenzao na viumbe wengine, kwa hiyo fikiria wewe ni kiongozi pahala fulani mtu kafishwa wewe kama kiongozi mwenye dhamani unawajibika leo hii na hata kesho hapo kesho lazima utadaiwa roho ya huyu aliyefishwa.
Mwanakwetu Upo?
Kumbuka,
Kijana Mchora TATOO
Inawezekana Timiza Wajibu/
makwadeladius@g mail com
0717649257
ALVAR MWAKYUSA KATIKA AKIWA KAZINI TSN
ALVAR MWAKYUSA AKIMUHOJI MAKONGORO NYERERE
PICHA ZINGINE ZOTE NI ZA MAKTABA
Post a Comment