MNAPENDA KUSOMA SHULE YA MAMA

 


Adeladius Makwega-MBAGALA

Jumamosi ya Septemba 21,2024 niliamka asubuhi sana huku nikigafirika nikidhani kuwa ni siku ya jumapili-siku ya dominika, hivyo nikamuita binti yangu aamke ili ajiandae tuelekee kanisa kusali ibada ya kwanza, binti yangu akanijibu,

“Baba leo siyo Jumapili, Baba Leo ni Jumamosi .”

Hiyo ni saa 11 .37 ya afajiri ya Septemba 21, 2024, kwa hiyo nikarudi kitandani kulala huku usingizi umekata. Nikiwa kitandani mawazo yangu yakarudi miaka mingi nyuma nadhani mwaka 1987 mwishoni, mimi na mdogo wangu anayeitwa Modestus Makwega tumetoka shuleni majira ya mchana, Shule ya Msingi Mnazi Mmoja  ambayo ipo wilayani Ilala Dar es Salaam (Katikati ya Jiji), siku hii ilikuwa ya jumanne tukafika kituo cha basi Mnazi Mmoja tukapanda UDA la Temeke kupitia Shimo la Udongo, tunawahi mafudisho ya Kamuniyo ya Kwanza–Kituo cha Kiroho Mbagala, huku Mwanakwetu anasomeshwa na Katekista Mbunda naye Modestus anasomeshwa na Katekista Kidiwa .

UDA lilipofika Uhasibu, huyu Modestus Makwega akamwambia Mwanakwetu .

“Kaka tutachelewa mafundisho, mwalimu wangu Katekista Kidiwa hana shida, ila Katekisa wako ni mkali, unatambua zile fimbo zake anazozificha nyuma ya kabati, leo ukichelewa utachapwa tena tushukie Mtoni Aziz Ali .”

Kweli tulipofika hapo Azizi Ali tukashuka.

Msomaji wangu nikurudishe nyuma kidogo, wanafunzi wa Komuniyo ya Kwanza walikuwa wanasoma siku mbili kwa wiki na kanisani wanatakiwa kuonekana kwa lazima mara nne, Jumanne mafundisho na kusali na Ibada ya Misa ya Mtakatifu Antony wa Padua .

“Eee Mtakatifu Antony wa Padua uliye Mpole sana zaidi ya watakatifu wote, Upendo wako kwa Mungu na kwa binadamu wote umekusahilisha sana ulipoishi hapa dunia...”

Kumbuka haya ni maneno ya awali ya saa ya Mtakatifu huyu.

Jumamosi mafundisho asubuhi na jioni tunasali rozari nje ya Kanisa Dogo a Mtakatifu Antony wa Padua alafu jumapili jioni misa ya watoto saa 10 .30 . Kumbuka msomaji wangu Mwanakwetu na mdogo wake Modestus wapo Mtoni Azizi Ali wanangoja basi ili wapande washuke Mbagala misheni maana mafundisho ni saa 9 30 alasiri, walitakiwa wawe katika chumba cha mafundisho kinachoungana na nyumba ya mapadri pale Kituo cha Kiroho Mbagala. Msomaji wangu hiyo sasa ni saa 9 na ushehe mabasi hakuna .

 

Tukiwa hapo basi zinapita zimejaa, kwa hiyo msaada wetu labda labda mabasi ya UDA tu na liwe tupo lakini basi hilo halitokei. Gafla ikasimama Land Rover ya Rangi ya Buluu ikiwa inasimama watu wazima wakakimbilia, walipofika wakaongea nao alafu watu wazima hawakuingia ndani ya gari hiyo iliyokuwa na dereva na mtu mmoja . Mara tukasikia sauti inaita;

“Nyie wanafunzi njooni mpande .”

Yesu wangu nilishutukia mimi na mdogo wangu tupo ndani ya Land Rover pamoja na wnafunzi wenzetu kadhaa ambapo watu wazima walikataliwa kupanda gari hiyo, huku wakituonea gere wanafunzi sie. Tulipokuwa garini huyu abiria pembeni ya dereva akawa anatuuliza majina yetu na shule tunazosoma. Alipouliza mimi na Modestus shule tunayosoma tulipojibu akauliza mbona mnasoma mbali? Kwanini msisome Mbagala ?

Modestus Makwega akajibu

“Tunasoma shule ambayo mama yetu anasomesha .”

Huyu abiria pembeni akawa anatutania .

“Kumbe Nyinyi Mnapenda Kusoma Shule ya Mama .”

Karibia na Mbagala Misheni tukawaomba hawa jamaa siye tunashuka, Land Rover Defender ikasimama tukashuka, wanafunzi wenzetu waliobaki ndani wakaufunga Mlango na ubavuni gari hiyo iliandikwa ubavuni maneno haya MBUNGE JIMBO LA TEMEKE ambaye alikuwa jamaa mmoja mfupi , mweupe kama chotara hivi, mchangamfu sana .

Tuliposhuka tukakimbia haraka kanisani na kufika chumba cha mafundisho Katekista Mbunda akawa anaitwa majina na jina la kwanza na Mwanakwetu-Adeodatus Makwega nikajibu nipo . Katekista Mbunda alikuwa analikosea jina langu anaita Adeodatus badala ya Adeladius. Huku akisema,

“Leo mwanafunzi wa Mnazi Mmoja kawahi .”

Wanafunzi wa mafundisho wanacheka, akiwamo rafiki wa Mwanakwetu ndugu Edwin Ngutu ambaye siku hizi ameokoka . Tukasoma mafundisho vizuri baadaye kusali ibada ya misa ya Mtakatifu Antony wa Padua ilipokwisha tukawa tunarudi nyumbani. Tukawa tunasimulia yaani leo katuokoa Mbunge wa Temeke Masoud Ali Masoud, vingenevyo ningechapwa kama ilivyokuwa jumanne iliyopita. Kwa hakika jumanne iliyotangulia Mwanakwetu alichelewa mafundisho, utetezi ulikuwa nasoma mbali, katekista katika kuliamua hilo akauliza;

“Humo yumo Mwanafunzi mwingine anayesoma Mnazi Mmoja?”

Catherine kutoka Mtoni Mtongaji aliyekuwa anakaa jirani na Mtongani Treni Juu Magari Chini akanyoosha mkono, na yeye alikuwa amewahi, kwa hiyo Mwanakwetu hakuwa na utetezi alicharazwa bakora, maana mbona Catherine kawahi?


 

Wakati tunarudi nyumbani Edwin Ngutu akasema

“Adeladius ameonewa maana Catherine analetwa na gari ya baba yake hadi kanisani tofauti na Adeladius anapanda UDA .”

Baadaye sku hiyo kila mmoja alifika nyumbani kwake. Kumbuka hayo yote Mwanakwetu anayakumbuka na yupo nyumbani kwake afajiri Septemba 21, 2024 .

Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?

Shabaha ya makala haya zipo tele lakini siku ya leo Mwanakwetu anakupa moja tu-Mbunge wa Temeke wakati huo marehemu Masoud Ali Masoud aliwasaidia akina Mwanakwetu wakiwa wadogo ambapo tukio hilo lipo katika kumbukumbu ya Mwanakwetu hadi leo hii. Mwanakwetu anasema ndugu zangu ambao ni wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hapa dunia hatuishi mara mbili alafu utaenda utarudi, dada yangu Dkt Tulia angalieni sana, maneno yenu yanarekodiwa na watu, michango yenu vikaoni, sheria zenu mnazopitishe msipokuwa makini jamii itawananga na kuwasimanga mno hapo kesho hata vizazi vyenu.Kwa tekinojia ya sasa mnarekodiwa mara mbili kuweni makini, kama ukijaliwa uhai unajua unaweza hata ukaomba urudi ukaweka mambo sawa katika cheo ulichokuwa nacho lakini nafasi hiyo hautoipata tena, wabunge wote na viongozi wote wa Bunge tumieni nafasi hiyo vizuri, wakati haurudi nyuma . Jaribuni kulirejeshea Bunge letu heshima maana wanaona maandamano ndiyo suluhu wakati Bunge lipo Je Bunge linatimiza wajibu wake?Ndiyo yale yale anayosimulia jaji Warioba .Jiulize hivi nikiwa sipo katika kiti hiki watu wakipitia maamuzi yote niliyofanya  Mungu wangu itakuwaje?


 


.

Mwanakwetu Upo?

Kumbuka

“Kumbe Nyinyi Mnapenda Kusoma Shule ya Mama”

Nakutakia Siku Njema .

makwadeladius@gmai .com

0717649257

 





 


0/Post a Comment/Comments