JAJI MKUU LAZIMA ANUKIE MARASHI YA MAHAKAMA

Adeladius Makwega-MBAGALA MAKUKA

Mwanakwetu alikuwa na nywele nyingi hivyo akaamua kwenda kwa kinyoozi, kutoka kwake hadi hapo mwendo wa dakika tatu kwa miguu, alipofika hapo alikutana na binti mmoja mdogo amejilaza katika benchi la wateja, akamuuliza mama naweza kunyoa? Binti huyu mrembo mwenye miguu ya bia juu ya benchi akajibu kuwa leo hii mnyoaji hayupo na hata simu yake anampigia hapatikani, aliipoteza lakini alisema angenunua simu nyingine nadhani bado hajainunua.

Huyu binti kazi yake katika saloon hii ya kiume ni kuwaosha wateja wake nywele zao baada ya kunyoa ambacho kitendo hicho Mwanakwetu huwa hafanyi kila akienda kunyoa katika saloon.

Mwanakwetu akamuuIiza juu ya saloon nyingine, akaeIekezwa vizuri na kwenda kunyoa, ambapo ipo katika mazingira ya barabarani Iakini ni vigumu sana mtu kutambua kama pana kinyoozi, aIipofika hapo akasubiri jamaa mmoja akanyoa alafu akafuata yeye, anayenyoa ni fundi mzuri kuliko hata iIe saIoon ya awali, wakati Mwanakwetu anaingia saIoon ambayo ipo barabarani kuIisikika sauti za watu wazima wawiIi wanaongea habari kadhaa za Tanzania juu ya uteuzi wa Rais Samia SuIuhu Hassan .

Mwanakwetu ananyoa huku anayasikia mazungumzo haya

“Eti kwani Mwanasheria Mkuu wa Serikali anapochanguliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa, amepanda au ameshushwa cheo?”

Jibu kwa aliyeulizwa Mwanakwetu hakulisikia kabisa maana huyu kinyozi alikuwa anaongea na mteja wake Mwanakwetu kumpa maelekezo ya namna nzuri ya kukaa wakati anamnyoa, baada ya Mwanakwetu kukaa vizuri kinyozi anaendelea na kazi yake, masikio ya Mwanakwetu yakasikia maneno haya;

“Yule atakuwa anaandaliwa kuwa Jaji Mkuu.”

Kumbuka Mwanakwetu yupo saloon na huyu kijana kinyonzi yupo makini na kazi yake na haelewi kama Mwanakwetu anayasikiliza kwa umakini mazungumzo ya jamaa wa nje sa loon hii .


Mazungumzo yanaendelea huku bodaboda na baiskei zinapita na jamaa wanaopita wakiwasa limu hao ndugu , Mwanakwetu akang’amua kuwa hawa jamaa wanamzungumizia juu ya mhe Jaji Dkt Eliezer Mbuki Feleshi ambaye alichaguliwa kuwa jaji wa mahakama ya rufaa, Gafla zinasikika kwa mbali sauti za gari kubwa ikipiga honi, hawa ndugu wawili wakasema tusogea kando, madereva wengine wahuni, baada ya lori hilo kupita jamaa mmoja akasema,

“Kituo cha Polisi kimekamilika ili tufungwe, kwanini asingeboresha kituo ch afya kiwe Hospitali ya Wilaya?”

Jamaa hao huko nje mmoja kando anacheka alafu anasema mnajenga vituo vya polisi ili tufungwe, kwanini asingeboresha Shule ya Sekondari ya Malya? Sauti ya jamaa ya kando inasema nyie Wasukuma hamna shukurani

Huku Kijana wa sa loon na Mwanakwetu kinyozi anaendelea na kazi

“Je Unanyoa Masharafa na Masharubu?”

Mwanakwetu akasema yapunguze tu hayo masharafa na masharubu

Haya maswali ya kijana kinyozi yakasabisha Mwanakwetu akawa hayasikii mazungumzo ya hawa ndugu nje ya saloon na baada ya dakika kadhaa kijana wa saloon akauliza kama Mwanakwetu anachonga nywele akajibu hapana, huku nje sasa ikawa hazisikiki kabisa sauti zao naye Mwanakwetu akamaliza kunyoa akalipa sh 2000/- na kutoka zake na nje, akitamani kuwafahamu hawa jamaa lakini hakuona mtu, hivyo alitoka zake akapita mkahawani ili kunywa chai .

Akiwa anakunywa chai Mwanakwetu mawazo yake yalikuwa hasa juu ya mambo mawili ya kitaifa nayo ni;

“Eti kwani Mwanasheria Mkuu wa Serikali anapochanguliiwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa amepanda cheo au ameshushwa cheo?- Yule atakuwa anaandaliwa kuwa Jaji Mkuu.Yule atakuwa anaandaliwa kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.”

Mwanakwetu akajiuliza je ni kweli Jaji Mhe. Dkt Eliezer Mbuki Feleshi anaweza kuwa anaandaliwa kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania? Maana hapa Malya Kwimba mkoani Mwanza ni kwao .

Hilo kwa hesabu za Mwanakwetu aliona kuwa Jaji Mhe. Dkt Eliezer Mbuki Feleshi amefanya kazi kwa karibu na Rais Samia Suuhu Hassan kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali tangu Septemba 2021 hadi Septemba 2024 ambapo Jaji Dkt Feleshi amefanya kazi na huyu mwanasiasa wa CCM kutoka huko Kizimkazi Zanzibar kwa siku zinazokaribia 1000 kwa karibu mno ambapo majaji wengine kwa hakika hawana sifa hiyo .


 

Kumbuka Mwanakwetu anakunywa chai yake mkahawani, haya anayafikiria tu, hapo hapo Mwanakwetu tena akajiuliza swali jengine je Rais Samia Suluhu Hassan akifanya hivyo atakuwa amefanya maamuzi sahihi?

Mwanakwetu akajibu majibu kuwa jibu lake inaweza kuwa Ndiyo au Hapana. Sahihi kwa Rais Samia mwenyewe lakini hapana ya Mwanakwetu, hapo hapo Mwanakwetu akamaliza kunywa chai sasa anatoka zake kurudi kwake .

Akasema Je kwanini Jaji Mhe. Dkt Eliezer Mbuki Feleshi hapaswi kuwa Jaji Mkuu?

“Huyu jamaa akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameshauri mambo mengi katika masuala ya mikataba ya Serikali, kwa hiyo inawezekana mambo haya yakaleta migogoro na baadaye watu wakaenda mahakama, huko wakamkuta Jaji Mkuu yule yule yule, hilo linaweza kutokea hata huku UJAJINI alipo mahakama ya RUFAA, hata sasa wapangaji wa mashauri mahakama ya rufaa wawe makini katika hili. Kibinadamu hawezi kuwa na nguvu ile kama majaji wengine.

Ndiyo kusema Mhe. Dkt Eliezer Mbuki Feleshi alitakiwa kubaki kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali amalizane na manukato ya serikali kama haya yanayosema na Mwanakwetu mathalani mkataba wa DP WORLD. Hata kama Jaji huyu atabadili gia angani wanasiasa aliofanya nao kazi katika Baraza la Mawaziri, watamnanga si tulikuwa naye barazani sasa anaamua nini mahakamani ? Hilo la kunanga hadharani itakuwa haki hata mbele ya Mungu kama atabadili gia angani.”

Mwanakwetu kumbuka yu njiani kwenda kwake, hapa Malya Mwanza Tanzania akitoka kwa kinyozi asubuhi hiyo .


 

Mwanakwetu akasema ngoja amuume sikio mhe Jaji Dkt Eliezer Mbuki Feleshi mwenyewe,

“Kwa hakika Jaji Feleshi unapendwa sana na ndugu zako hapa Malya Mwanza Tanzania, Mwanakwetu ametambua hili, anakuomba siku nyingine, kama

mwanawe au ndugu yake yoyote anaweza pengine akakutana na dada yako au nduguyo wa Kisukuma akampenda, akataka kuoa/kuolewa usikatae kwa chukizo kuandika makaa haya na ndiyo makala haya yameandikwa kwa heshima zote kwako na kwa Jmahri ya Muungano wa Tanzania kama ushauri wa Mwanakwetu.”

Mwanakwetu akafika nyumbani kwake salama salimini; Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?

Kwa sasa Tanzania inahitaji Jaji Mkuu Mpya lakini ambaye hanukii manukato ya Serikali ambaye ataweza kuiongoza vema mahakama yetu,kuongeza imani zaidi kwa Watanzania katika chombo hiki cha kinachoshika hatamu ya haki Tanzania.


 

Mwanakwetu upo?

Kumbuka,

“Jaji Mkuu Lazima Anukie Marashi ya Mahakama”

 

Nakutakia Siku Njema

makwadeadius@gmaili com

0717649257




 

 


0/Post a Comment/Comments