JAMII YENYE CHUKI AU FURAHA

 


 

Lucas Masunzu- Shinyanga.

IMEKUWA kawaida kwa Nduguyetu kuwa shahidi wa kuona nduguze wakisaliti ukaperana kufunga ndoa takatifu na safari ya maisha ya ndoa kianza. Kumbukumbu zanduguyetu zilimpeleka hadi kwenye ndoa takatifu ya ndugu Baraka Masatu iliyofungwakatika kanisa mojawapo la Waadventista wa Sabato, na leo hii wanapongezwa kwakitimiza miaka mitano kavu ya ndoa yao. Nduguyetu alikumbuka namna watuwalivyoshiriki katika ibada hiyo ya ndoa takatifu huku akikumbuka vizuri maneno ya

Mchungaji alivyopigia mstari kuwa

 “nanyi waume endeleeni kuwapenda wake zenukama vile Kristo   alivyolipenda kanisa” siku hiyo hilo halikuwa la bwana harusi pekee bali darasa pia lilikuwepo kwa waume wote waliohudhuria.

Nduguyetu anakuuma sikio siku ya leo kuwa siku ya harusi ni siku ya furaha mno kwa Wasabato, watu wengi huhudhuria na walivyowakarimu hata kama hujaalikwa ukiwezakujialika una uhakika wa kuingia mesini na kushiriki mlo kikamilifu. Kwa sababu ya uhakika huo nduguyetu amekuwa na mahudhurio mazuri kila panapotokea tukio la namna hiyo.



 Mahudhurio mazuri yakafanya nduguyetu ajenge ukaribu na udugu na watu wengi wa kanisa hilo akiwamo mpiga kinanda wa kanisa hilo Benjamin Kasonde. Ikafika kipindi akawa anashirikishana, na kushauriana mambo mbalimbali na mpiga kinanda huyo na hivyo ndivyo maisha yanavyokwenda. Ukaribu huo ukafanya ndugu yetu apatemajibu ya maswali mengi kutoka kwa huyo huyo mpiga kinanda likiwamo; Kwa nini kila harusi kanisani wimbo uitwao “Panapo Pendo” huimbwa? Kuna siri gani katika wimbo huo?

Hapo hapo Ben akaanza kuimba wimbo huo kwa mluzi;Furaha i nyumbani, panapo pendo, Hapana machukizo, panapo pendo, Chakula ni kitamu, mashamba yasitawi,Maisha ni kamili, panapo pendo.

Baadaye akasema; Wimbo huo “Panapo Pendo” ni wimbo 184 katika kitabu cha nyimbo za

Kristo, ulitungwa na James McNautghton ambaye ni Mkanada. Ni wimbo wenye ujumbe wa pekee sana kwa familia zetu. Tafakari za kina alizokuwa nazo James kuhusu umuhimu wa upendo na amani katikafamilia zilimfanya atunge wimbo huu unaoimbwa leo hii na maelfu duniani. Kuna familia ambazo hazina amani kabisa, upendo haupo, baba akiingia watoto wote huchagua kujificha ama hukaa kimya bila kuongea.

Tena kuna familia ambazo baba na mama ni akina Evander na Tyson, mpaka watoto wanajuta kuzaliwa kwenye familia hizo kwa sababu upendo haupo. Tunaimba huu wimbo mara kwa mara ili ujumbe wake ufike kwa wanandoa na familia zote. Siri kubwa ni kwamba ikiwa upendo utatawala nyumbani watoto watakuwa na furaha, kuna umuhimu mkubwa mno wa kuwa na upendo na furaha katika familia zetu kwa sababu familia ni karakana pekee ya kuandaa jamii yenye chuki au furaha.

Usikubali kuwa mzazi ambaye utapoteza furaha ya familia yako.

Nakutakia siku njema, Kwa heri.

 

theheroluke23@gmail.com,

0762663595



0/Post a Comment/Comments